Afisa Mtendaji Mkuuwa EAG Group Imani Kajula Akimwelezea Jambo Rais wa Simba Sport Club Evans Aveva (Aliyekaa) Wakati wa Uzinduzi wa Tovuti ya Club Hiyo Anayeshuhudia ni Makamu wa Rais wa Club ya Simba Geofrey Nyange ‘Kaburu
Simba Sports Club leo hiiimezindua tovuti yake Ili kukuza mawasiliano na wadau wake mbalimbali hususani; wanachama, wapenzi, vyombo vya habari na wadau wengine muhimu.
Akizungumza wakati wauzinduzi huo Rais wa Simba Evans Aveva alisema ‘’Katika dunia na zama za utandawazi tovuti ndio na mitandao ya jamii ndio njia kuu ya mawasiliano. Sisi tuliliona hili na leo hii nafurahi kuwa Simba Sports Club itazindua rasmi tovuti yake ambayo itakuwa jukwaa kuu la mawasiliano na utoaji wa taarifa zake za club ya Simba. Natarajia wengi wenu mtaitumia kikamilifu na muhimu zaidi mtatupa mrejesho chanya kuhusu tovuti yetu’’.
AfisaMtendajiMkuuwa EAG Group Imani Kajula ambao ni washauri watekeleza ji wa Masokona Biashara wa Simba alisema ‘’Tovuti hii sio tuitaiwezesha Simba kuwapa wadau wake taarifa mbalimbalibali pia itatumika kwa ajili ya uuzaji wa vifaa vya Simba, Bidhaa mbalimbali mpya na muhimu zaidi kuwaunganisha wanachama, mashabiki na wapenzi wa Simba kutumia mitandao ya jamii iliyo rasmi ya Simba Sports Club’’.
Mkutano huo wa wandishi wa habari ulitumika kutaarifu Wanachama, Wapenzina Vyombo vya habari juu ya kocha mpya wa Simba. Alizungumza wakati wakumtambulisha kocha mpya wa Simba, Rais Aveva alisema ‘’Baada ya kupitia vyeti na maombi ya makocha mbalimbali, Napenda kuwa taarifu kuwa Klabu ya Simba imeingia kwenye mkataba wa kuifundisha na kocha Dylan Kerr raia wa Uingereza. Ni kocha mwenye uzoefu wa zaidi ya miaka 30, akiwa amefanya kazi Nchi mbalimbali zikiwemo Uingereza, Scotland, Vietnam na AfrikayaKusini’’.
Aliendelea kusema ‘’Tunaamini ujuzi na uzoefu wake wa ukocha na pia kama mchezaji wa kiwango cha juu utakuwa chachu ya kuifanya Simba ifanye vizuri’’
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni