Social Icons

Jumamosi, 27 Juni 2015

Tevez arejea nyumbani Boca Juniors

Straika wa Argentina Carlos Tevez amekamilisha Uhamisho wake kwenda Boca Juniors kutoka kwa Mabingwa wa Italy Juventus.

Tevez, mwenye Miaka 31, alianzia Soka lake huko kwao na Klabu ya Boca ambayo aliihama Mwaka 2004 kwenda Brazil kuchezea Corinthians na kisha kukaa Miaka 9 akichezea Klabu za Ulaya.
Huko Ulaya alizichezea Klabu za England, West Ham, Mwaka 2006-2007, Manchester United, 2007-2009, na Manchester City, 2009-2013, na kisha kwenda Italy kuichezea Juventus ambako msimu uliopita aliisaidia tena kutetea Taji lao la Ubingwa kwa kupiga Bao 20.
Majuzi Juventus walimbadili Tevez kwa kumsaini Straika wa Atletico Madrid ya Spain, Mario Mandzukic ambae anatoka Croatia.
Akithibitisha Uhamisho huu, Rais wa Boca Juniors Daniel Angelici alisema: "Ni Siku ya furaha sana na ya kuridhisha. Kurudi kwa Tevez akiwa kwenye kilele cha mafanikio ni habari njema kwa Washirika na Mashabiki wote wa Boca na Soka la Argentina!"

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

 
 
Blogger Templates