Social Icons

Jumatatu, 29 Juni 2015

Uchaguzi wa ubunge wafanyika Burundi

Uchaguzi wa ubunge unaendelea nchini Burundi licha ya wiki ya maandamano ya ghasia dhidi ya uamuzi wa rais Pierre Nkurunziza wa kutaka kuwania muhula wa tatu.

Baadhi ya vituo vya kupigia kura vilifunguliwa kuchelewa baada ya maguruneti kurushwa.
Upinzani umesusia uchaguzi huo.Muungano wa Ulaya unasema kuwa uchaguzi huo utazidisha mgogoro uliopo.
Umoja wa Afrika umekataa kutoa waangalizi ukisema kuwa baadhi ya masharti yaliowekwa hayajaafikiwa kwa uchaguzi kuwa huru na haki.
Zaidi ya watu 70 wameuawa tangu mgogoro huo uanze.Karibu watu 130,000 wamelitoroka taifa hilo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

 
 
Blogger Templates