Andy Murray anaungana na Waingereza wenzake watatu kucheza hatua ya pili ya michuano ya tenis ya Wimbledon inayoendelea jijini London, baada ya kumcharaza Mikhail Kukushkin wa Kazakhstan.
Murray, wa tatu kwa ubora duniani alishinda kwa seti 6-4 7-6 (7-3) 6-4 katika mchezo uliodumu kwa saa mbili na dakika 13 wakati hali ya hewa ikiwa nyuzi joto 41 za Selisyasi.
Murray anasema ilikuwa mechi ngumu. Na yeye ndiye aliyeifanya iwe hivyo katika seti ya pili ya mchezo.
Kuingia raundi ya pili Murray anaungana na Waingereza wenzake Liam Broady, Aljaz Bedene na James Ward kutinga raundi ya pili, akiwemo pia Heather Watson namba moja kwa ubora nchini Uingereza kwa upande wa wanawake akimbwaga Caroline Garcia wa Ufaransa kwa seti 1-6 6-3 8-6 .
Hii ni mara ya kwanza kwa Waingereza wanne kwa pamoja kutinga raundi ya pili tangu mwaka 2006. Katika raundi hiyo Murray atakabiliana na Mholanzi Robin Haase, ambaye alimbandua Alejandro Falla wa Colombia kwa seti nne.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni