Madiwani 10 wa Halmashauri ya Bariadi kutoka Chama cha Mapinduzi na UDP wamesoma alama za nyakati na hatimaye wamejiunga na CHADEMA.
Mmoja wa madiwani hao Ruta Mahagija kwa niaba ya madiwani wenzake kutoka CCM alisema wamechoshwa na utawala wa CCM hivyo wameona njia pekee ya kulikomboa taifa ni kujiunga na chadema ili kwa pamoja tuiondoe CCM madarakani.
Madiwani hao wameapa kuisambaratisha CCM kwenye halimashauri yao katika uchaguzi wa mwaka huu mwezi Oktoba.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni