Serikali ya Ugiriki iko mbioni kuandika mapendekezo mapya yatakayo kwamua mazungumzo ya kutafutia ufumbuzi wa matatizo yake ya kiuchumi.
Hii inafuatia muda wa siku tano uliotolewa na viongozi wa Ukanda wa Ulaya mjini Brussels kwa nchi hiyo kuleta mapendekezo yake.
Kauli hiyo ya waziri mkuu wa Ugiriki Alexis Tsipras inafuatia tamko la Rais wa Baraza la Ulaya Donuld Tusk kwa bunge la Ulaya.
Bwana Tusk ameonya kuwa zimesalia siku tano tu ya kutatua mgogoro wa Ugiriki la sivyo mambo yote yaharibike.
Akizungumzo wakati wa mkutano na viongozi wa ukanda wa Ulaya, bwana Tusk amesema uwa huu ndio wakati mgumu zaidi kwa bara ulaya.
Ugiriki imepewa hadi Ijumaa , siku ya mwisho ya kuwasilisha mapendekezo yake ya kukwamua uchumi wake.
Bwana Tusk ameitisha kikao kamili cha muungano huo mwishoni mwa wiki akisema kuwa iwapo Ugiriki itaishia kufilisika, basi hatua hiyo itakuwa na athari kubwa kwa Ukanda mzima wa Ulaya
Kwa upande wake rais wa tume ya Ulaya Jean-Claude Juncker, ametahadharisha kuwa tayari wameandaa mpango mbadala iwapo Ugiriki itaondoka kutoka kwa Jumuiya hiyo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni