Bunge la Ugiriki limeunga mkono kwa asilimia kubwa mapendekezo ya hivi punde ya serikali yenye lengo la kumaliza tatizo la deni la nchi hiyo
Baada ya kikao kilichoendeleka hadi usiku wabunge 252 waliipa serikali idhini ya kufanya mazungumzo na wakopeshaji wake.
Waziri mkuu Alexis Tsipras alishindwa kupata kura za wabunge kumi kutoka chama chake cha Syriza wakiwemo mawaziri wawili wa serikali na spika wa bunge.
Waziri wa zamani wa fedha Yanis Varoufakis hakuhudhuria kikao hicho.
Bwana Tsipras alikiri kuwa mabadiliko yaliyopendekezwa yalikuwa nje ya ahadi zilizotolewa na chama chake.
Mapendekezo hayo yatajadiliwa na mawaziri wa fedha wa nchi za ulaya hii leo na pia viongozi wa ulaya kesho jumapili.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni