Social Icons

Jumatano, 1 Julai 2015

FACEBOOK YAFUNGUA OFISI AFRIKA KUSINI

Kwa mara ya kwanza Facebook imefungua ofisi yake barani Afrika, Johannesburg nchini Afrika kusini ikiwa ndio makao makuu.
Mwanadada Nunu Ntshingila ndiye atakae ongoza ofisi hiyo itakayo jikita katika kutafuta njia mbali mbali za kuongeza ushirikiano na wafanya biashara wa barani humo.
Tayari watumiaji wa facebook barani Afrika ni milioni 120, ofisi hiyo mpya inalenga kuongeza idadi ya watumiaji wake nchini Kenya, Nigeria na Afrika Kusini.
Nunu Ntshingila ndiye mkurugenzi mkuu wa ofisi hiyo ambae amesema kuwa mkakati wa kupanua uwekezaji wao hasa katika matangazo ni mipango mikubwa ya kutanua biashara pamoja na bara la Ulaya na maeneo ya Mashariki ya Kati.
Barani Afrika kuna mtumiaji mmoja kati ya watano wa intanenti na inatarajiwa idadi hiyo kukua mara mbili zaidi kwa watumiaji wa simu za mkononi ifikapo mwaka 2020.
Asilimia 80% ya wanao tumia facebook ni wale wenye kupata huduma hiyo kupitia simu zao za mikoni.
Facebook anasema pia ina mipango madhubuti ya kuongeza wateja kutoka nchi za Senegal, Ivory Coast, Ghana, Tanzania, Rwanda, Uganda, Zambia, Msumbiji na Ethiopia ili kufikia malengo yake.
Kwa msaada wa mtandao.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

 
 
Blogger Templates