Social Icons

Jumatatu, 27 Julai 2015

Rais Obama awasili nchini Ethiopia


Rais Barack Obama wa Marekani hatimaye amewasili nchini Ethiopia katika ziara yake ya pili ya nchi za Afrika.
Ni mara yake ya kwanza tangu aongoze taifa la Marekani akiwa raisi kuhutubia wanachama hamsini na mbili wa umoja wa Afrika katika makao makuu yake yaliyoko Addis ababa.Mazungumzo yao yakiwa yamelenga kutafuta suluhu ya kutokomeza migogoro ya vita za wenyewe kwa wenyewe sudan ya kusini.
Raisi Obama,aliwasili nchini Ethiopia akiwa anatokea mjini Nairobi ambako aliwaambia wakenya kuwa amna kikomo cha kile wanachokihitaji na kusisitiza kwa kutoa angalizo katika athari za ukabila na rushwa. Tamaduni mbaya kama unyanyasaji wa kijinsia,ndoa za kulazimishwa ,tohara kwa watoto wa kike na kutopeleka watoto shuleni.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

 
 
Blogger Templates