Social Icons

Jumatano, 8 Julai 2015

Dilma Rousseff asema kamwe hatishiki

Rais Rousseff amewataka wapinzani wake watafute ushahidi dhidi yake
Huku kukiongezeka tuhuma kuhusu mustakabali wa serikali yake, rais Dilma Rousseff ameliambia gazeti la Folha de Sao Paulo kwamba 'hatoanguka' n kwamba hakuna msingi wa yeye kuachishwa kazi na bunge.
Ikiwa ni miezi saba baada ya kuingia katika muhula wake wa pili wa uongozi , serikali yake inatikiswa na kashfa ya rushwa katika kampuni kubwa ya mafuta nchini Petrobras.
null
Waandamanaji dhidi ya serikali ya Rousseff
Tuhuma za hivi karibuni zinadai kwamba kampeni yake ya kuwania urais ilifadhiliwa kwa pesa haramu kutoka kampuni hiyo.
Umaarufu wa Rousseff umedidimia kwa kiwango ambacho hakijawahi kushuhudiwa cha asilimia 9.
Siku ya Jumanne ameliambia gazeti hilo la Folha de Sao Paulo kwamba hatishiki.
Amekana kufanya makosa yoyote na amesema hivi ni vita vya kisiasa na amewataka wapinzani ake watafute ushahidi dhidi yake.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

 
 
Blogger Templates