Kuna dalili zenye uwezo wa kukusaidia kubaini mtu anayejitambua katika maisha yake. Unapokosa dalili hizi ujue kabisa kuwa bado hujafikia ngazi ya juu kabisa ya kujiweza kujitambua na kuweza kuleta mabadiliko makubwa katika maisha yako. Ninapozungumzia mabadiliko nikiwa na maana ni kuwa na uwezo wa kupanga malengo na kuyafanikisha na kuishi kwa amani na furaha bila kutegemea mambo ya nje.onaviews.blog
Huenda dalili hizi zinaweza zikawa nyingi zaidi lakini kwa leo nitakutajia chache tu baadhi ambazo zitaweza kukusaidia moja kwa moja. Ukiona una dalili hizi au jamaa yako ana dalili hizi, huna budi kuanza kujua kwamba, uko kwenye kiwango cha juu cha kuweza kutumia nguvu zako za ndani na kuweza kufikia mafanikio yoyote makubwa unayoyahitaji katika maisha yako ya kila siku.
Kwanza, ni mtu anayepokea mambo katika hali halisi. Haathiriwi na mazoea, bali kile kilichopo, kinachopaswa kuona na kuchambuliwa, ndicho anachokipokea. Ina maana huchambua, bila kujali mazingira au mazoea yanasema nini. Unapokuwa unaona mtu ana dalili kama hiyo, elewa kabisa mtu huyo anajitambua katika maisha yake.
Pili, ni mtu anayejikubali yeye kama yeye, hataki wala hatamani kuwa kama wengine. Ameridhika na kukubaliana na alivyo na maisha yake yalivyo. Lakini pia ni mtu anayekubali wengine kama walivyo na kutokutaka wengine wawe kama yeye. Vilevile ni mtu anayekubaliana na maumbile na uhalisia wake katika maisha yake.
Tatu, ni mtu ambaye hahitaji sana usiri na faragha. Mtu anayejitambua huzidi sana kujiondoa kwenye hali ya kuhitaji faragha sana kama ndiyo jambo la lazima. Kwa kujitambua, mtu huwa huru zaidi na hakuna jambo ambalo linaweza kuhitaji faragha. Kama yapo ni machache sana ambayo ni ya maana na sio kila jambo ni usiri na faragha.onaviews.blog
Nne, ni mtu ambaye huridhika na kutambua mchango wa mwingine au wengine na kukubaliana na yale yenye kumtokea. Kwa hali hiyo ni mtu ambaye hahemkwi. Majibu yake kwa mambo yanayomtokea yametulia sana, hasa kwenye suala la hisia zake. Anayejitambua hudhibiti hisia, na siyo hisia kumdhibiti yeye.
Tano, ni mtu ambaye hayuko tayari kuwa mtiifu, ni mtu ambaye hayuko tayari kuwa mtiifu tu bila kujua sababu. Kama ni kufuata jambo, hajiulizi maswali mengi sana kabla hajaamua. Hii ina maana kwamba, haendeshwi na mazoea, bali hutumia tafakari kwanza.
Sita, ni mtu mwenye uwezo wa kujibainisha na binadamu mwingine. Aliyejitambua huamini kwamba, kile ambacho kinamfurahisha yeye, kinaweza kumfurahisha binadamu mwingine hivyohivyo kama alivyo yeye kilimvyomfurahisha.
Saba, ni mtu ambaye anapata uwezo mkubwa wa ubongo, mawazo ya kufanikisha na kufanya hali iwe bora zaidi. Kwa hiyo, ni mtu ambaye ana uwezo wa kubuni na kufanya mabadiliko mahali. Siyo mabadiliko ya kuleta fedha tu, bali mabadiliko ya kuwafanya binadamu wengine kujisikia vizuri.
Kwa kifupi, hizo ndizo dalili ambazo mtu anayejitambua anaweza kuwa nazo katika maisha na kuzitumi kuweza kuleta mabadiliko chanya katika maisha yake na jamii kwa ujumla.