Jumamosi, 29 Novemba 2014
BUNGE LAHIRISHWA TENA ASUBUHI HII
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Anne Makinda akifafanua jambo wakati akiendesha Bunge hilo
Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Anna Makinda Amelazimika Kuliahirisha Bunge Asubuhi Kwa mara ya Pili mara baada ya Kuliahirisha Saa tatu Asubuhi Hadi saa Kumi Jioni .
Hali hiyo Imetokana na Mazungumzo yanayoendelea kwajili ya Wabunge Kuridhiana Maendekezo ya Kamati ya PAC yaliyokuwa yanataka Baadhi ya Viongozi Kuwajibika.Hali iliyosababisha Bunge hilo kutokuelewana la Kulazimika Kuhairishwa jana Saa nne Usiku.
Jumanne, 25 Novemba 2014
DR.SLAA AKIWA NYUMBANI KWAKE.
Dk Slaa akiwa nyumbani kwake pamoja na wanafamila wengine
Dk SLAA akiendelea na maongezi na wanafamila akiwa nyumbani kwake
DK SLAA akicheka baada ya mtoto wake kumfurahisaha
Hapa Slaa akiongea na mgeni wake
Waandamanaji wafanya vurugu St.Louis
Mji wa St Louis limeshuhudia maandamano na vitendo vya uporaji baada ya jaji kupitisha uamuzi wa kumshtaki aliyemuua kijana mweusi Michael Brown.
Polisi mjini humo wamesema vurugu zimeleta madhara makubwa zaidi kuliko ya mwezi Agosti baada ya kuuawa kwa kijana huyo.
Kamanda wa Polisi wa St Louis, Jon Belmar amesema alisikia milio ya risasi takriban 150 kutoka kwenye makundi ya watu.
Brown alifyatuliwa risasi na Polisi tarehe 9 Mwezi Agosti, hali iliyoibua ghadhabu na maandamano.
Watu wengi wa jamii ya Afrika na Marekani walitoa wito wakitaka Afisa Polisi Darren Wilson ashtakiwe kwa mauaji.
Rais wa Marekani Barack Obama alitoa wito kwa wamarekani kuwa watulivu na kukubali maamuzi ya Jaji kuhusu kesi hiyo.
Miili yatelekezwa Sierra Leone
Wafanyakazi ambao huzika miili ya Watu waliokufa kwa Ebola, mjini Kenema nchini Sierra Leone wamegoma kwa sababu hawajalipwa marupurupu yao.
Miili 15,kati ya hiyo mingi inahitajika kuzikwa,imetelekezwa katika hospitali kuu mjini humo.
Mwili mmoja unadaiwa kutelekezwa kwenye Ofisi ya Meneja wa Hospitali hiyo, huku miili miwili ikiwa imetelekezwa kwenye mlango wa kuingilia Hospitali hapo.
Wafanyakazi hao wameiambia BBC kuwa hawajalipwa marupurupu ya waliyoyaita ya hatari kama walivyoahidiwa kwa ajili ya Mwezi Oktoba na Novemba.
Kenema ni mji wa tatu kwa ukubwa nchini Sierra Leone na Mkubwa katika eneo la Mashariki mwa nchi hiyo ambako ugonjwa huo uligunduliwa kwa mara ya kwanza.
Takriban Watu 5000 wamepoteza maisha kutokana na ugonjwa huu katika nchi za Magharibi mwa Afrika, Guinea,Liberia na Sierra Leone.
SAKATA LA MADAWA YA KULEVYA LINALOMKABILI MFANYABIASHARA MAARUFU DAR LACHUKUA SURA MPYA!
Mfanyabiashara maarufu jijini Dar es Salaam, Muharani Mohammed Abdallah, maarufu kama Chonji(mwenye suti), akiwa chini ya ulinzi. Vyanzo vyetu makini kutoka jeshi la polisi zinasema kuwa mali zinazochunguzwa kutokana na tuhuma hizo nzito ni maghorofa, fedha pamoja na magari anayomiliki. “Tuliambiwa kuwa huyu bwana alikuwa akiishi maisha ya hali ya juu, sasa kutokana na tuhumza zake polisi wameanza kuchunguza kila alichonacho ili kujua uhalali wake,” kilisema chanzo. HALI tete, siku chache baada ya mfanyabiashara maarufu jijini Dar es Salaam, Muharani Mohammed Abdallah, maarufu kama Chonji kukamatwa na kutupwa gerezani kwa tuhuma za kukamatwa na dawa kulevya, sasa mali zake zimeanza kuchunguzwa.
Chanzo hicho kiliendelea kusema kuwa, kuna baadhi ya watoto wa vigogo akiwemo mtoto wa meya mmoja wa zamani (jina tunalihifadhi), jijini Dar es Salaam ambaye anadaiwa kuwa alikuwemo katika mkumbo wa kukamatwa Chonji lakini alitoroka na sasa anasakwa na polisi.Kamanda wa Kikosi cha Kudhibiti na Kupambana na Madawa ya Kulevya nchini, SACP Godfrey Nzowa alipotafutwa na gazeti hili ili afafanue madai hayo alisema uchunguzi wa mali za wote wanaotuhumiwa kukamtwa na dawa za kulevya ni lazima ufanyike.
Chonji akiwa chini ya ulinzi mkali na wenzake mahakamani. “Tunachunguza mali zao wote waliokamatwa na tuhuma za dawa za kulevya na siyo kwa Chonji peke yake, inapodhihirika kuwa ni za madawa huwa wanafilisiwa,” alisema Kamanda Nzowa. Chonji na wenzake wanne walikamatwa usiku wa manane Oktoba 21, mwaka huu nyumbani kwake Magomeni Mtaa wa Kondoa jijini Dar na inadaiwa walikuwa na mzigo wa unga uliokuwa ukifungwa katika vifurushi vidovidogo pia anadaiwa kukutwa na sare za jeshi (JWTZ) na bastola
MUOKOE MTANZANIA 15456 BBA MPIGIE KURA.
PIKA KURA KUMTOA IDRISA KATIKA DANGER ZONE BBA 15456 MTANDAO WOWOTE.
Jumatatu, 24 Novemba 2014
MAREKANI: WAZIRI WA ULINZI CHUCK HAGEL AJIUZULU
Barack obama amekubali Jumatatu Novemba 24 ombi la kujiuzulu kwa waziri wake wa ulinzi, Chuk Hagel.
Waziri wa ulinzi wa Marekani Chuck Hagel, amewasilisha barua yake ya kujiuzulu Jumatatu Novemba kwenye Ikulu ya Washington. Kujiuzulu huko kumetangazwa na Chuck Hagel wakati wa mkutano na vyombo vya habari, mkutano ambao umehudhuriwa na barack Obama.
Kulingana na kauli ya Barack Obama, Chuk Hagel ndiye ametaka mwenyewe kutamatisha muhula wake kwenye wadhifa aliyokua akishikilia. Kati ya wawili hao hakuna aliyetoa maelezo zaidi kuhusu uamzi huo wa kujiuzulu. Lakini kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Marekani, waziri wa ulinzi alikua alipewa shinikizo.
Gazeti la New York Times limebaini kwamba kujiuzulu kwa Chuk Hagel kunahusiana na hali ya kutoelewana iliyojitokeza katika vita vinavyoendeshwa na Marekani dhidi ya kundi la wapiganaji wa Dola la Kiislam nchini Iraq na Syria.
Inasadikiwa kuwa Ikulu ya washington huenda ilikua ikitathmini mkakati wake dhidi ya wanajihadi na ilikua inahitaji mkakati huo uanze kutekelezwa na waziri mpya wa ulinzi. Chuck Hagel awali alikuwa na wajibu wa kusimamia uondoaji wa majeshi kutoka Iraq na Afghanistan, wala si kusimamia operesheni ya kijeshi.
Washirika wa karibu wa Barack Obama wamekanusha hoja ya kujiuzulu kutokana na kushinikizwa. " Hakuna tofauti ya maoni ambayo imesababisha Chuk hagel anachukua umazi huo wa kujiuzulu", maafisa wa Ikulu ya Washington wamesema. Maafisa hao wamebaini kwamba mazungumzo ya kujiuzulu kwa Chuk Hagel yalianza wiki mbili zilizopita.
Waziri wa Ulinzi ataendelea kushikilia wadhifa huo hadi atakapopatikana mrithi wake. Majina kadhaa tayari yameanza kutajwa, ikiwa ni pamoja na Michèle Fournoy, aliyekuwa naibu waziri wa ulinzi.
MAHARUSI WAOANA NDANI YA BWAWA LA MAJI
Maharusi wawili walifanya harusi yao katika bwawa lenye lita milioni 1.5 za maji ya bahari .
Bi Dorota Bankowska mpiga mbizi mzoefu aliolewa na mpenzi wake ambaye ni mwalimu James Abbot nyumbani kwao mjini Plock , Poland mwezi jana lakini akataka sana kufanya jambo la kipekee wanakoishi kama ishara ya kusherehekea harusi yao.
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)