Chelsea wanaonekana kuishinda kasi Manchester United katika kumsajili Pedro baada ya timu hiyo ya London kukubali kutoa kitita cha paund milioni 21 kwa mchezaji huyo mwenye miaka 28.
Pedro kwa sasa yupo katika hatua za mwisho kukamilisha usajili wake huku mashabiki wa Chelsea wakiwa na msisimko mkubwa kumtizama mchezaji huyo akiwaruudhisha katika mbio za ubingwa wa mataji mbalimbali.
Pedro anatazamiwa kujijengea umaarufu kwa mashabiki wa Chelsea kutokana na kuwa msikivu na mnyenyekevu huku pia akiwa na shauku ya kucheza ambapo mashabiki wa Uingereza hupenda watu kama hao.
Atapata ukaribisho mzuri pia katika vyumba vya kubadilishia nguo vya Chelsea kutoka kwa wachezaji wenzake kwa sababu sio mbinafsi,ni mpambanaji na mkarimu ambaye anaweka mahitaji ya timu mbele kuliko ya kwake binafsi.
Pedro wakati akiwa Barcelona, alikua akitumika zaidi kama mchezaji wa akiba licha ya kuifanyia makubwa timu hiyo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni