Mfanyikazi wa huduma za misaada kutoka Marekani ambaye aliuawa mnamo mwezi februari akiwa mateka wa kundi la Islamic State nchini Syria alinyanyaswa kijinsia na kiongozi wa kundi hilo Kulingana na maafisa wa Marekani.
Kayla Mueller mwenye umri wa miaka 26 aliripotiwa kubakwa mara kadhaa na Abu Bakr al Baghdadi.
Maafisa wa kukabiliana na Ugaidi walielezea familia yake mnamo mwezi Juni.
Mueller alitekwanyara wakati alipokuwa akifanya kazi mjini Allepo nchini Syria mwaka 2013.
Wapiganaji wa IS wanasema kuwa aliuawa katika shambulizi la angani lililotekelezwa na Jordan ,lakini Marekani inalilaumu kundi hilo kwa kifo chake.
''Tuliambiwa kwamba Kayla aliteswa na kwamba alikuwa mali ya Baghdadi. Tuliambiwa mnamo mwezi Juni na serikali'',wazazi wake Carl na Marsha waliliambia shirika la habari la ABC.
Inadaiwa kuwa Baghdad alimchukua afisa huyo wa misaada kwa nyumba ya mwanachama mwengine wa IS Abu Sayyuf ambaye alikuwa akisimamia kitengo cha mafuta na gesi hadi kifo chake katika oparesheni ya vikosi maalum vya Marekani mnamo mwezi May.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni