Aliyekuwa mgombea wa kura za maoni kupitia chama cha mapinduzi jimbo la mtama SELEMANI METHEW amekihama chama hicho na kuondoka na wana CCM wapatao 704 na kuhamia chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA kwa kile anachodai hakutendewa haki katika mchakato mzima wa kura za maoni.
METHEW amesema kuondoka ndani ya CCM kumetokana na maamuzi ya wananchi ambao wameona haiwezekani na haitawezekana kiongozi wanayemuitaji kufanyiwa hila na mizengwe,kudhulumiwa haki yake ya msingi ya kuwaongoza wananchi wa jimbo la mtama.
Amesema jimbo la mtama halihitaji usanii bali linaitaji mgombea shupavu atakayeweza kupambana na mgombea wa CCM Nape Nnauye huku akisisitiza uwezo huo anao.
Mkutano huo umeudhuriwa na wanawake wengi ambao kwa sehemu kubwa ndiyo waliorudisha kadi za CCM.
Mkutano huo ulipambwa na vimbwanga mbalimbali likiwemo tambiko rasmi lililotumika kumzindika mgombea huyo ikiwa ni pamoja na kumpa nguvu na kumkinga na majanga ili aweze kufanikisha kampeni na kuibuka na ushindi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni