Bomu kubwa limelipuka karibu na makao makuu ya usalama kaskazini viungani mwa mji mkuu wa Misri, Cairo.
Watu 29 walijeruhiwa katika mlipuko huo ikiwemo maafisa sita wa polisi.
Bomu hilo lilisikika katika maeneo mengi ya mji huo na mwandishi wa BBC anasema kuwa hayakuwepo majeraha mengi kwa kuwa mlipuko huo ulitokea usiku.
Eneo hilo kwa sasa limefungwa na kuna maafisa wengi wa polisi katika barabara za mji huo.
Kundi la wapiganaji wa Islamic State limekiri kutekeleza shambulizi hilo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni