Ripoti za vyombo vya habari kutoka nchini Uingereza na Ujerumani zimelilaumu shirikisho la riadha duniani IAAF kwa kuhujumu utafiti ambao uligundua kuwa thuluthi moja ya wanariadha walikiri kuvunja sheria za matumizi ya dawa za kusisimua misuli.
Kulingana na gazeti la Sunday Times na kituo cha ARD cha Ujerumani ni kuwa mamia ya wanariadha waliwaambia watafiti kuwa walitumia dawa za kuongeza nguvu zilizopigwa marufuku walipohojiwa miaka minne iliyopita.
Chuo cha Ujerumani kilichoongoza utafiti huo kinasema kuwa IAAF imezuia kuchapishwa kwa takwimu hizo.
IAAF inasema kuwa bado mazungumzo yanaendelea.
Mapema mwezi huu IAAF ilikataa madai ya vyombo hivyo vya habari kuwa kuna matumizi makubwa ya dawa za kuongeza nguvu katika riadha.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni