skip to main |
skip to sidebar
Joyce Kiria: Niliamua kuolewa kwa kukosa kodi ya nyumba,TAFAKARI WA KWAKO ANAKUPENDEA NINI?
Ijumaa: Historia yako inaonesha uliwahi kuwa ‘house girl’, je ulishawahi kukutana na ishu ya kubakwa?
Joyce: Namshukuru Mungu nilikutana na mitihani mingi lakini sikuwahi kubakwa, ila katika kazi yangu nimekuwa nikikutana na wadada wengi waliofanyiwa hivyo na kuwasaidia.
Ijumaa: Mume wako amepita kwenye kura za maoni na kuelekea kwenye ubunge, unalizungumziaje hilo?
Joyce: Nimefurahi sana, namuombea kila la heri avuke katika hatua inayofuata.
Ijumaa: Hivi ni kwa nini uliachika kwenye ndoa ya mwanzo?
Joyce: Niliachika kwa sababu sikuwa nimempenda mwanaume niliyekuwa naye bali niliingia kwenye ndoa kwa sababu ya kitu na hili ni fundisho kwa wanawake.
Ijumaa: Ina maana wewe uliolewa na mwanaume wa kwanza kwa sababu ya pesa zake?
Joyce: Kiukweli nisiwe mnafiki nakumbuka mwanaume wangu wa kwanza alinioa kwa sababu sikuwa na kodi ya nyumba na sikuwa na pa kuipata, nikaona kwa sababu mimi mwanamke bora niolewe maisha yaniendee, lakini nilipoingia ndani mambo yalikuwa tofauti sana, nikaamua kuachika.
Ijumaa: Mume wako wa pili unakumbuka mara ya kwanza mlikutana wapi?
Joyce: Nilikutana naye kwenye harakati zangu, wakati huo naye alikuwa akifanya siasa zake ndipo penzi jipya likazaliwa.
Ijumaa: Ukiwa na mumeo chumbani au unapikapika unapenda kuvaa nguo gani?
Joyce: Napenda kuvaa nguo za kumhamasisha siyo madira wala kanga ila vinguo flani vya kunifanya niwe ‘sexy’.
Ijumaa: Wewe ni mwanaharakati, mara nyingi wanawake wenye misimamo huwa hawadumu kwenye ndoa, unadhani yako itadumu?
Joyce: Unayoyasema ni kweli wanaume hawapendi wanawake wenye misimamo, mimi na mume wangu tunaelewana ingawa kuna wakati tunatofautiana kwa sababu yeye ni mwanaume na mimi ni mwanamke, mwisho wa siku tunamalizana.
Ijumaa: Kwa sasa ni mama wa watoto wawili, je unatarajia kuwa na watoto wangapi katika maisha yako?
Joyce: Kutokana na maisha kulielezea hilo ni ngumu ila kwa sasa bado najipanga kuwalea hawa nilionao kwanza.
Ijumaa: Unawaambiaje mashabiki na wasikilizaji wako wa Kipindi cha Wanawake Live?
Joyce: Nawasisitiza wanawake wenzangu wafanye kazi kwani inatufanya tuheshimike.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni