Mabingwa wa Ulaya, FC Barcelona wamepoteza kwa kipigo kikali mechi ya kwanza ya Spanish Super Cup dhidi ya Athletico Bilbao.
Wakiongozwa na mchawi wao, Lionel Messi, Barca wamedundwa 4-0.
Aritz Aduriz ameingia kwenye vitabu vya kumbukumbu vya mashabiki wa Barcelona kufuatia kupiga mabao matatu peke yake 'Hat-trick' katika dakika za 53, 62, 68, huku Mikel San Jose naye akifunga goli moja dakika ya 13 kipindi cha kwanza.
Nyota anayewaniwa na Manchester United, Pedro alianza kikosi cha kwanza, lakini alishindwa kabisa kupenya ngome ya Bilbao.
Aduriz akicheka na nyavu
Wakitokea kushinda 5-4 dhidi ya Sevilla katika mechi ya fainali ya Uefa Super Cup iliyochezwa kwa dakika 120, kocha wa Barca, Luis Enrique hakuwaanzisha Gerard Pique, Sergi Busquets, Andres Iniesta na Ivan Rakitic.
Wakati huo tayari alikuwa anawakosa wachezaji wanaosumbuliwa na Majeraha, Jordi Alba na Neymar.
Ili kupindua kichapo hicho, Barcelona wanahitaji kushinda 5-0 nyumbani Camp Nou.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni