Baada ya kuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu golikipa mkongwe na mahiri Juma Kasejakuwa bila timu na kuhusishwa kujiunga na vilabu mbalimbali hatimaye uvumi huo umemalizika August 19 baada ya kusaini mkataba wa miezi sita wa kuitumikia klabu yaMbeya City kutoka Jijini Mbeya.
Mkataba wa Juma Kaseja wa kujiunga na klabu ya Mbeya City umesainiwa August 19 mbele ya meneja wake mpya Athumani Tippo hivyo huo ni mwisho wa uvumi wa habari za Juma Kaseja atacheza wapi msimu ujao, taarifa hizo zinakuwa pigo kwa kocha waMwadui FC ya Shinyanga Jamhuri Kiwelu ambaye alikiri katika vyombo vya habari kuwa ana hitaji huduma ya Kaseja kikosini mwake.
Kabla ya kusaini mkataba na Mbeya City Juma Kaseja alikuwa nje ya uwanja kwa kipindi cha zaidi ya miezi nane baada ya kuingia katika mgogoro wa kimkataba na iliyokuwa klabu yake ya zamani ya Yanga nakufanya kesi hiyo kutinga mahakamani.