Social Icons

Alhamisi, 26 Novemba 2015

Papa Francis: Dini isitumiwe kuvuruga amani

Image caption
Papa Francis ameongoza ibada ya misa ambayo imehudhuriwa na maelfu ya watu uwanja wa Chuo Kikuu cha Nairobi ambapo amesisitiza umuhimu wa familia katika jamii.
Awali katika mkutano na viongozi wa dini mbalimbali, alisema dini haifai kutumiwa kuvuruga akisema “Mungu ni Mungu wa amani.”
"Jina lake takatifu halifai kutumiwa kutetea chuki na mauaji. Ninajua kwamba mashambulio ya Westgate, Chuo Kikuu cha Garissa na Mandera bado hayajasahaulika. Na sana, vijana wamekuwa wakiingizwa na kufunzwa itikadi kali kwa jina la jini kupanda woga na kuvunja umoja katika jamii,” alisema.
"Ni muhimu sana tuwe manabii wa amani, watu wa amani wanaokaribisha wengine kuishi na amani, umoja na kuheshimiana. Mungu na akaguze nyoyo za wanaohusika katika mauaji na ghasia, na azipe imani familia na jamii zetu."
Mkutano huo umehudhuriwa na viongozi wa makanisa mengine akiwemo kiongozi wa Kanisa la Kiangilikana Kenya Dkt Eliud Wabukala.
Viongozi wa dini ya Kiislamu Kenya pia wamehudhuria mkutano huo, wakiongozwa na Prof Abdulghaful El-Busaidy.
Papa Francis amesema amekuwa akihakikisha kila aendako anatangamana na watu wa dini na imani nyingine.
Misa
Image captionBaada ya misa, waumini waliendelea kupokea komunyo
"Huwa ni muhimu sana kwangu kwamba, ninapofika pahali kutembelea waumini wa kanisa Katoliki, ninakutana na viongozi wa makanisa mengine na dini nyingine. Natumai kuwa wakati ambao tumekuwa pamoja utakuwa ishara ya matamanio ya Kanisa kwa dini zote, ninaomba ikaweza kuimarisha urafiki ambao tayari tunajivunia,” amesema.
Wakati wa ibada ya misa ambayo ilianza saa nne asubuhi, Papa Francis alisisitiza umuhimu wa familia katika jamii na kupinga utoaji wa mimba.
“Afya ya jamii yoyote hutegemea afya ya familia. Kwa ajili yake, na kwa ajili ya jamii, Imani yetu katika neno la Mungu inatuita tuunge mkono familia katika jamii, kuwakubali watoto kama Baraka kwa ulimwengu, na kutetea hadhi ya kila mtu, kwa ndugu zetu wote katika familia moja ya binadamu,” amesema.
Image captionBaadhi ya waumini walitoka Afrika Kusini
“Kwa kutii neno la Mungu, tunahimizwa kuachana na matendo ambayo yanachochea udhalimu miongoni mwa wanaume, kuumiza au kudumisha wanawake, na kutishia maisha ya watoto ambao hawajazaliwa ambao hawana hatia.”
Watu waliohudhuria ibada hiyo walianza kuingia uwanjani mapema na walivumilia mvua ambayo ilianza kunyesha mapema asubuhi

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

 
 
Blogger Templates