Nusu ya wanawake wote wajawazito hupatwa na tatizo la kujisikia kichefu chefu na kutapika; ni mojawapo ya dalili kuu za ujauzito.
Husababishwa na kuongezeka kwa hormone mwilini, mara nyingi huanza katika wiki ya sita ya ujauzito na huweza kutokea muda wowote wa siku.
Madaktari wengine huwa wanaamini ya kuwa ni dalili nzuri kwani humaanisha ya kuwa placenta inafanya kazi vizuri.
Kwa wanawake wengine tatizo hili huisha katika wiki ya kumi na mbili ya ujauzito. Lakini kwa wengine huweza kuendelea kwa kipindi kizima cha ujauzito.
Mara nyingi ni kitu cha kawaida ambacho kinakuja na kuondoka lakini pale ambapo mama anatapika kupita kiasi mpaka anashindwa kubakisha chakula au maji mwilini basi anahitaji kumuona daktari.
Vitu vya kufanya kusaidia au kupunguza tatizo hili:
- Kula milo mingi midogo mara kwa mara badala ya kula milo mikuu mitatu kwa siku. Hii itasaidia kwasababu wakati mwingine tatizo hili linasababishwa na kutokuwa na sukari ya kutosha kwenye damu(low blood pressure). Sukari hii ndio chanzo cha nguvu mwilini. Ukila mara kwa mara chakula kitapokelewa mwilini na kutengenezwa sukari na mwili kuwa na nguvu ya kutosha.
- Kunywa vinywaji nusu saa kabla au baada ya chakula. Usinywe vinywaji na kula chakula kwa wakati mmoja.
- Kula mkate wa kukausha(toast au crackers) au matunda yaliyokaushwa dakika 15 kabla ya kumka asubuhi.
- Kunwya maji mara kwa mara ili kuzuia mwili kuishiwa na maji (dehydradtion). Jaribu kunywa litre 2.5 kwa siku ikiwa pamoja na maji, chai au juice natural zisizo na sukari ya kuongeza.
- Jitahidi usile au kupita sehemu zenye harufu ya chakula zinazozidisha tatizo hili.
- Pumzika vya kutosha na pata usingizi wa mchana.
- Usikae sehemu zenye joto jaribu kukaa ndani kwenye feni au ac au nje sehemu zenye upepo. Kwasababu joto huzidisha tatizo hili. Pia usiende sehemu zenye watu wengi.
- Ndimu, tangawizi zinasaidia, pia unaweza kunywa maji ya ndimu au kula tunda la tikiti maji (watermelon) kupunguza kichefu chefu.
- Kula viazi vya kukausha na chumvi.
- Fanya mazoezi.
- Usilale baada ya mlo
- Usiache kula
- Usile au kupika vyakula vyenye pili pili (spicy) au mafuta mengi.
- Usinywe kahawa au vinywaji vikali
- Kula vyakula vya protein kabla ya kwenda kulala usiku
- Fungua madirisha au Tembea nje ili kupata upepo na oxygen ya kutosha.
- Weka kijiko kimoja cha maji ya Apple Cider Vinegar kwenye 8 ounces ya maji ya uvuguvugu kisha kunywa asubuhi kabla ya kuamka.
18. Kunywa chai za Rasberry leaf, Spear mint/ pepper mint, Anise seed, Fennel seed kabla ya kuamka asubuhi.
Umwone daktari kama:
Unatapika kupita kiasi mpaka unashindwa kubakisha chakula au maji tumboni au kama kutapika kunaambatana na homa au maumivu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni