Social Icons

Jumatatu, 9 Novemba 2015

ALAMA ZA KUKUONYESHA KUWA MPENZI WAKO SIO MWAMINIFU (some signs of cheating)




 Mabadiliko katika tendo la ndoa:
Jambo hili laweza kujidhihirisha katika picha mbili tofauti. Kwa kawaida wapenzi huwa na mazoea fulani katika tendo la ndoa, kwa muda waliokaa pamoja kila mmoja humfahamu mwenzake kwa kiasi fulani. Inawezekana likawa jambo la kushangaza pale ambapo gafla unamuona mpenzi wako anapoteza kabisa hamu ya tendo la ndoa, au hata mnapokuwa katika tendo hilo humuoni akifurahia bali anakuwa kama anayelazimishwa au kutohamasishwa na chochote. Kwa upande mwingine unaweza ukakuta mpenzi wako anakuja na ujuzi wa gafla katika mahusiano yenu ya tendo landoa, hali yake ya kukutamani inazidi gafla, anahitaji mapenzi mara kwa mara na hata mnapokuwa katika tendo hilo anadhihirisha utaalamu wa tofauti na ule uliouzoea. Hali hizi mbili zifanyike tahadhari katika kukusaidia kuyatazama mahusiano yenu.

 Marafiki wa mpenzi wako kukukwepa:
Ni hali yakawaida kuwa karibu au kuzoeana na marafiki wa mpenzi wako, maranyingine mtawasiliana nao kutaka kujua aliko mpenzi wako au kinachoendelea kwao. Inabidi ujiulize sana pale inapotokea gafla wale marafiki wa mpenzi wako uliowazoea, uliokuwa unawapigia simu wakati wowote leo wana kukwepa, na hata simu hawapokei na maranyingine wakipokea hawakupi taarifa yakueleweka au wanakudanganya. Hii yote inawezekana wanamlinda rafikiyao, au wanakosa cha kujibu maana wanajua uhalisia wa kinachoendelea.

Kuzungumza sentensi za kutatanisha:
Kama nilivyosema awali, wapenzi wengi hujuana kwa mengi, 
ikiwemo pia namna ya kuzungumza au kuonyesha hisia. Unaweza kukuta katika mapenzi yenu mpenzi wako anaanza kuwa na sentensi ngumu na zisizo kuwa na msingi kwa mfano anasema “kwa jinsi hii sidhani kama tutafika” “mi siamini kama mapenzi yanadumu” “yani ndio maana watu wanashindwa kukaa na mpenzi mmoja” na maranyingine anaweza kukuuliza baadhi ya maswali moja kwa moja ili kukuona utajibuje. Sentensi hizi zina chanzo moyoni, kuwa macho.

 Kuzidi kwa tabia za kutoonekana au kuponyoka:
Yawezekana mpenzi wako alikuwa na tabia ya kuwepo nyumbani mida isiyokuwa ya kazini au wikiendi, muda mwingi alipenda kuwa na wewe na akiaga basi atasema anakwenda wapi na akimaliza hurudi mapema kwa sababu anakiu ya kuwa nawewe, mara gafla sikuhizi haagi anakwenda wapi, ukiuliza inawezakuwa vita. Anakuwa na vijisafari vingi na vijisababu visivyoisha vya kumuwezesha kuponyoka. Sehemu ya kwenda na kurudi lisaa limoja anaweza kuchukua nusu siku, kila ukiuliza atakwambia nakuja, niko njiani, kuna foleni, nimekwama, na sababu nyingine nyingi sana. Ukiona haya yanazidi ujue kuna la zaidi ya foleni, na hizo sababu zote zinazotolewa zinafunika jambo.

Tabia za kuficha fedha:
Ninafahamu fika kwamba suala la uwazi katika mambo yanayohusiana na fedha na matumizi ni tatizo kubwa kwa wapenzi wengi, wengi wamegombana na hata kuachana kuhusiana na jambo hili. Japokuwa hili ni tatizo kwa wengi lakini wako wapenzi ambao wamekuwa na tabia ya kuambiana kwa uwazi matumizi na mapato yao, hakuna kitu wamefanya kuhusu fedha zao pasipo kuambiana na hivi ndivyo mlivyozoeshana, mara ghafla mmoja anaanza kuwa na siri kuhusu fedha zake au matumizi yake, na wala hapendi kuulizwa ulizwa kuhusu suala hilo. Tabia hii ikidhihirika katika mapenzi yenu usichelewe kuchunguza maana kwa kukaa kimya unaweza kujikuta umechelea mwana na maji ya moto.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

 
 
Blogger Templates