Migahawa na biashara nyingine hapa Marekani Jumatano zinatoa punguzo la bei kwa bidhaa na huduma ikiwa ni siku ya mashujaa .
Hali hiyo ya shukran maalum inaendelea wakati wa maadhimisho ya kila wakati na kukiwa na yale ya huzuni ikiwa ni pamoja na kuwekwa kwa shada la maua katika kaburi la wale wanajeshi ambao hawakuweza kutambulika na Rais Barack Obama alifanya hivyo katika eneo la makaburi ya mashujaa huko Arlington Virginia, karibu kabisa na makao makuu ya nchi ya Marekani.
Siku hii ambayo ni maalum kabisa kutoa heshima kwa wale wote waliotumikia taifa katika jeshi la Marekani ilianza tangu 1919 wakati rais Woodrow Wilson alipotangaza Novemba 11 kama siku ya kusitisha mapigano kwa muda kusheherekea kumalizika mapigano ikiwa ni mwaka mmoja katika vita vya kwanza vya dunia “vita kumaliza vita vyote” kati ya Ujerumani na mataifa yalioungana ya Uingereza , Ufaransa na Marekani.
Sitisho la mapigano lilikamilika rasmi mwishoni mwa siku ya 11 katika mwezi wa kumi na moja.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni