Social Icons

Jumamosi, 28 Novemba 2015

JUST A SONG...............



Kujisikia Kichefu chefu na Kutapika wakati wa ujauzito (Morning Sickness)



Nusu ya wanawake wote wajawazito hupatwa na tatizo la kujisikia kichefu chefu na kutapika; ni mojawapo ya dalili kuu za ujauzito. 

Husababishwa na kuongezeka kwa hormone mwilini, mara nyingi huanza katika wiki ya sita ya ujauzito na huweza kutokea muda wowote wa siku. 

Madaktari wengine huwa wanaamini ya kuwa ni dalili nzuri kwani humaanisha ya kuwa placenta inafanya kazi vizuri.

Kwa wanawake wengine tatizo hili huisha katika wiki ya kumi na mbili ya ujauzito. Lakini kwa wengine huweza kuendelea kwa kipindi kizima cha ujauzito.

Mara nyingi ni kitu cha kawaida ambacho kinakuja na kuondoka lakini pale ambapo mama anatapika kupita kiasi mpaka anashindwa kubakisha chakula au maji mwilini basi anahitaji kumuona daktari.


Vitu vya kufanya kusaidia au kupunguza tatizo hili:

  1.  Kula milo mingi midogo mara kwa mara badala ya kula milo mikuu mitatu kwa siku. Hii itasaidia kwasababu wakati mwingine tatizo hili linasababishwa na kutokuwa na sukari ya kutosha kwenye damu(low blood pressure). Sukari hii ndio chanzo cha nguvu mwilini. Ukila mara kwa mara chakula kitapokelewa mwilini na kutengenezwa sukari na mwili kuwa na nguvu ya kutosha. 
  2. Kunywa vinywaji nusu saa kabla au baada ya chakula. Usinywe vinywaji na kula chakula kwa wakati mmoja.
  3. Kula mkate wa kukausha(toast au crackers) au matunda yaliyokaushwa dakika 15 kabla ya kumka asubuhi.
  4. Kunwya maji mara kwa mara ili kuzuia mwili kuishiwa na maji (dehydradtion). Jaribu kunywa litre 2.5 kwa siku ikiwa pamoja na maji, chai au juice natural zisizo na sukari ya kuongeza.
  5. Jitahidi usile au kupita sehemu zenye harufu ya chakula zinazozidisha tatizo hili.
  6. Pumzika vya kutosha na pata usingizi wa mchana.
  7. Usikae sehemu zenye joto jaribu kukaa ndani kwenye feni au ac au nje sehemu zenye upepo. Kwasababu joto huzidisha tatizo hili. Pia usiende sehemu zenye watu wengi.
  8. Ndimu, tangawizi zinasaidia, pia unaweza kunywa maji ya ndimu au kula tunda la tikiti maji (watermelon) kupunguza kichefu chefu.
  9. Kula viazi vya  kukausha na chumvi.
  10. Fanya mazoezi.
  11. Usilale baada ya mlo
  12. Usiache kula
  13. Usile au kupika vyakula vyenye pili pili (spicy) au mafuta mengi.
  14. Usinywe kahawa au vinywaji vikali
  15. Kula vyakula vya protein kabla ya kwenda kulala usiku
  16. Fungua madirisha au Tembea nje ili kupata upepo na oxygen ya kutosha.
  17. Weka kijiko kimoja cha maji ya Apple Cider Vinegar kwenye 8 ounces ya maji ya uvuguvugu kisha kunywa asubuhi kabla ya kuamka.


18. Kunywa chai za Rasberry leaf, Spear mint/ pepper mint, Anise seed, Fennel seed kabla ya kuamka asubuhi. 



Umwone daktari kama:

Unatapika kupita kiasi mpaka unashindwa kubakisha chakula au maji tumboni au kama kutapika kunaambatana na homa au maumivu.

Watatu wauawa katika shambulio la kambi ya UN

Image copyright
Image captionMali kambi ya vikosi vya umoja wa Mataifa
Watu 3 wamefariki katika shambulio la roketi katika kambi moja ya vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Mataifa kaskazini mwa Mali,Umoja wa mataifa umesema.
Wanajeshi wawili wa Umoja huo kutoka Guinea na mjenzi mmoja wameuawa katika shambulio hilo la mji wa Kidal kulingana na maafisa.
Ujumbe huo wa kulinda amani nchini Mali uliidhinishwa mwaka 2014 baada ya Ufaransa kuongoza kampeni za kijeshi kuwafurusha wapiganaji wa kiislamu kutoka eneo la Kaskazini.
Jeshi hilo kwa jina Minusma linajumlisha wanajeshi 1000 kutoka mataifa mbali mbali wengi wakiwa ni majirani wa taifa la Mali.
Wapiganaji wa kiislamu wanashukiwa kutekeleza shambulio hilo ambapo watu 14 walijeruhiwa huku watu kadhaa wakijeruhiwa vibaya.
''Kambi yetu ya Kidal ilishambuliwa mapema asubuhi na wapiganaji waliotumia makombora ya roketi'', alisema mmoja wa maafisa kutoka kwa kikosi hicho cha Minusma.

KWANINI WANAUME WENGI WALIOKO KWENYE NDOA WANAKUFA MAPEMA NA KUWAACHA WAKE ZAO?




COFFIN



1. Umri mdogo wa kikomo cha maisha “life expectancy” – Kama unafahamu hili jambo linaloitwa “life expectancy” utakubaliana na mimi kwamba umri wa mwanaume wa kuishi ni mdogo sana ukilinganisha na mke wake, hususani kusini mwa jangwa la sahara. Kwa hiyo wanawake wanapewa nafasi kubwa ya kuishi muda mrefu kuliko waume zao.
2. Ugumu katika kufunguka –j Utakubaliana na mimi kwamba wanaume ni wagumu sana ten asana kufunguka na kushirikisha mambo yao, wao wako tayari wafe na tai shingoni wakijifanya hawaumii au hawasikii shida. Mkiwa na ishu kwenye ndo mkaitwa sehemu muyaongee yeye kamwe hamumpati, anakwambia mambo yetu tutasuluhisha wenyewe wakati ndani yanamla na kummaliza. Na kwa mtai huu watakufa sana tu
3. Ugumu katika kusamehe – Kusamehe sio tu kwa faida ya anayesamehewa bali pia kwa afya yaw ewe unayesamehe. Mzigo unaotokana na kusamehe hutuumiza sana mioyo yetu, hata kama mara nyingine tunajifanya hatuna shida yeyote. Unaposamehe unaachilia mzigo mkubwa, wanaume wao ni wagumu sna kusamehe. Wako tayari wakubebe moyoni miaka, na tena watakukumbusha uchungu wao kila wanapokuona. Hii inawala sana bila wao kujua.
4. Tabia hatarishi – Wanaume wengi kwenye ndoa ndio wanaoongoza kushiriki tabia hatarishi kama vile ulevi, anasa, ngono holela na hii huwaweka karibu zaidi na jeneza kuliko wake zao waliowaacha nyumbani wakiwadanganya kuwa wako mkutanoni mkoani.
5. Ugumu katika kujali afya – Ni rahisi sana mwanaume akajisikia vibaya lakini asiende hospitalini kuangalia afya, hata pale anapohimizwa kwenda bado anaweza kukwepa au kubisha au hata kusema kuwa ameshakwenda au ameshakunywa dawa kumbe mwongo. Wako pia ambao wanaweza kupewa dawa na wasizitumie.
6. Msongo wa mawazo – Wanaume ndio wabebaji wakubwa wa shehena za msongo wa mawazo “stress” ingawa kwa nje wanajitahisi sana kuonyesha kuwa mambo yako shwari wakati wanatafunwa ndani. Kaulize hospitalini, wanaokufa kwa presha ya kupanda au ya kushuka, stroke, kusimama kwa moyo, kupasuka kwa mishipa ya damu, matatizo ya mifupa, au kuumwa sana kichwa, halafu uliza ni jinsia gani.

Pellegrini:''Guardiola hanitishi''

Image copyrightPA
Image captionPellegrini
Mkufunzi wa kilabu ya Manchester City Manuel Pellegrini amesema kuwa hana wasiwasi na ripoti zinazomuhusisha mkufunzi wa Bayern Munich Pep Guardiola na kazi yake.
Guardiola alifanya kikao cha habari na waandishi siku ya ijumaa huku kukiwa na tetesi kutoka kwa magazeti kwamba ataelekea City na nyota wa Barcelona Lionel Messi.
''Ni uvumi ambao umekuwa ukiendelea katika misimu miwili na nusu sasa'', alisema Pellegrini ambaye aliajiriwa na City mnamo mwezi Juni alipoulizwa kuhusu uvumi huo.''Sina tatizo na hilo''.
Image copyright
Image captionGuardiola
Ripoti zimedai kwamba Guardiola mwenye umri wa miaka 44 amekubali kuondoka Bayern mwishoni mwa msimu huu ili kuichukua Manchester City.
Mwenyekiti Karl-Heinz Rummenigge amesema kuwa tangazo kuhusu siku za usoni za mkufunzi huyo litafanywa kabla ya mwisho wa mwaka huu.

Watu 3 wauawa katika shambulio Colorado

Image copyright
Mshambuliaji akamatwa Colorado
Watu 3 wameuawa baada ya kupigwa risasi na mtu mmoja aliyevamia kituo cha kupanga uzazi katika eneo la Colorado Springs nchini Marekani.
Mtu mmoja aliyeshukiwa kufyatuliana risasi na maafisa wa polisi ametiwa mbaroni.
Kituo hicho kinasimamiwa na shirika la kitaifa la afya la Planned Parenthood ambalo limekuwa likilaumiwa na baadhi ya watu kwa kutoa mimba.
Risasi za kwanza zilisikika mapema asubuhi na kuendelea kwa saa tano polisi wakifyatuliana risasi na mtu huyo.
Image copyright
Image captionMaafisa wa polisi wanaimarisha usalama katika eneo la tukio
Wakati huo wote taasisi za kukabiliana na hali ya dharura zilikuwa karibu kukiwa na ambulansi ambazo zilikuwa zimesubiri katika theluji iliyotanda eneo hilo.
Polisi walifyatuliana risasi na mtu huyo walipokuwa wakiwaokoa watu waliokuwa wamekwama katika jengo hilo.
Wengine wao walikuwa na majeraha.
Afisa wa polisi wa kutoa usalama katika Chuo Kikuu, Garrett Swasey, mwenye umri wa miaka 44, alikuwa miongoni mwa waliouawa asubuhi.
Image captionAfisa wa polisi
Alifariki na raia wengine wawili.
Alikuwa na mke na watoto wawili.
Watu wengine tisa, kukiwemo maafisa wengine watano wa polisi walipelekwa hospitalini na inasemekana kuwa hali yao inaendelea kuimarika.
Baadaye mwanamume mmoja alijisalimisha na kutiwa mbaroni na kuelekezwa kwenye kituo cha polisi.
Image copyright
Image captionShambulio la kliniki Colarado
Shirika linalosimamia kliniki hiyo ya kupanga uzazi, Planned Parenthood, limekuwa likishutumiwa na baadhi ya makundi yanauyopinga uavyaji mimba kama njia ya kupanga uzazi.
Hata hivyo kufikia sasa lengo hasa la shambulio hilo halijulikani.

Alhamisi, 26 Novemba 2015

NEY AZUNGUMZIA WENZIE.....................YEYE JE?



Umeshawai kujiuliza kwa tabia au sifa ya mtu flani angeweza kufanya kazi gani kutokana na sifa hizo. Sasa Nay wa Mitego ameweza kuzungumzia watu maarufu wenzake watano kwa jinsi anavyowajua wangeweza kufanya kazi hizi zaidi ya wanazofanya sasa hivi.
Wema Sepetu
Kwa jinsi ninavyomjua Wema nadhani angekua customer care mzuri sana kwenye kampuni yoyote na sauti yake ile angewafurahisha wateja wengi sana. Lakini pia angeweza kuwa mhudumu mzuri tu kwenye hotel flani hivi nzuri nzuri na watu wangeenda kwenye hiyo hotel kwa sababu ya Wema. Anajua kuongea na watu, smile na sauti nzuri.
JB
Huyu jamaa na ule mwili wake ni mpishi mzuri sana zaidi ya kuwa muigizaji alivyo sasa. Pia mapenzi yake kwenye kula msosi basi inaonyesha jinsi gani yeye na msosi ni marafiki kuanzia jikoni hadi mezani.
TID
Huyu jamaa ni muongeaji pia ni mcheshi sana, ukitoa kuwa msanii mzuri basi angeweza kuwa muuza chips mzuri sana maeneo ya kwao Kinondoni na banda lake lingejaa wateja wengi sana kwasababu ya kuongea kwake.
Diamond
Licha ya kufika hapo alipofika Diamond bado uswahili wake wa Tandale anao kama kawaida. Sasa napata picha huyu jamaa awe konda, itakua fujo sana kwenye hilo daladala na abiria wake. Nadhani maneno ya mtaani yatakua mengi na vichambo kama kwenye nyimbo zake..atawanyoosha abiria wake.
Adam Mchomvu
Huyu jamaa ana kipaji sana cha kuongea maneno ambayo huwezi kutegemea akaongea ghafla yani yakafurahisha na ku-make sense. Sasa Mchomvu ile kazi ya uswahilini kwetu ya kuuza dawa ya panya,mende,kunguni,viroboto angetisha sana. Hatakua na haja ya kujirekodi sauti na kile ki-speaker atakua anapiga free style tu.

Matola Asaini Timu ya daraja la kwanza


Aliyekuwa kocha msaidizi wa Simba SC Selemani Matola amesaini mkataba wa mwaka mmoja kuifundisha timu ya Geita Gold Sc. Baada ya Selemani Matola kujiuzulu nafasi yake kama kocha msaidizi wa Simba kwa kinachodaiwa kutoelewana na kocha mkuu wa timu hiyo Dylan Kerr, hatimaye kocha Selemani Matola ameingia mkataba wa mwaka mmoja kuifundisha timu ya Geita Gold SC inayoshiriki ligi daraja la kwanza Tanzania bara.
Akizungumza  baada ya kuachana na Simba matola alisema kwamba alipata offer kutoka timu nyingi ila offer ya Geita Gold SC ilikuwa nzuri zaidi.

“Kwanza nikueleze nilipata offer nyingi sana kabla ya kuja Geita lakini niliweza kuangalia sera za timu zinakwenda vipi, baada ya kuongea na uongozi wa Geita hasa mwenyekiti Bw. Salum kiukweli niliona ni watu wenye mwelekeo mzuri katika hali ya kupandisha timu. Kwahiyo siku zote mwalimu unategemea kwenda sehemu ambayo unaona inamwelekeo mzuri”.
“Mimi nimeichagua Geita kwasababu ni timu inayoonekana inamalengo ya baadae, nitajitahidi kwa uwezo wangu kwa kushirikiana na viongozi wa hapa tufanye kile kinachowezekana kuhakikisha timu inapanda ligi kuu”.
Mwenyekiti wa chama cha mpira wa miguu mkoa wa Geita Bw. Salumu Kulunge amesema wameamua kumtafuta Matola kwasababu anauwezo mkubwa wa kazi hiyo na wanaamini ataipandisha timu hiyo kucheza ligi kuu msimu
ujao.

“Kuna mambo mengi ambayo yametokea na mpaka tumeamua kumleta yeye kwakweli kuna mapungufu mengi ambayo kama viongozi tumeyaona ndiyomaana tukaona ni vizuri kukawa na kocha ambaye tunaamini kabisa uwezo na jitihada zake za ushindani zinaweza zikatupeleka pale sisi tunapohitaji na hiyo ndiyo sababu kubwa iliyotufanya sisi tushawishike kumchukua Matola”.
“Tunamfahamu vizuri sana baadhi yetu tumechezanaye mpira lakini baada ya hapo mwenzetu aliendelea katika ngazi ya ukocha na sisi tukajiendeleza katika mambo mengine”.
Kwa upande wake kocha msaidizi wa timu hiyo Teru Yusuf Mpeka amesema anafarijika Matola kujiunga na Geita huku katibu mku wa timu hiyo Mnenge Suluja akisema wameamua kumuacha kocha Kim Kristopher kwakua hakuwa mkweli kipindi wanaingia mkataba kuinoa kikosi hicho.
“Tumefarijika sana kwa ujio wa kocha Selemani Matola katika timu yetu kuja kuongeza nguvu kwenye benchi la ufundi la timu yetu nafikiri itakuwa chachu ya maendeleo kwenye timu yetu, itabadilika sana kutoka hapa ilipo”.

Drogba anataka kuwa kocha wa Chelsea

Image captionMshambulizi wa zamani wa Chelsea na Ivory Coast Didier Drogba amesema kuwa atarejea Stamford Bridge kuwa kocha.
Mshambulizi wa zamani wa Chelsea na Ivory Coast Didier Drogba amesema kuwa atarejea Stamford Bridge kuwa kocha.
Drogba, ambaye kwa sasa anasakata soka ya kulipwa huko Canada, aliifungia the Blues mabao 164 katika enzi yake huko Stamford Bridge.
"Ningependa kuihudumia klabu hiyo hata baada ya kukamilika kwa kipindi changu cha uchezaji''
''Tayari nimekubaliana na wakurugenzi wa klabu hiyo kuwa ninaweza kurejea kuwa mkufunzi kwa sababu klabu hiyo ilinifaa sana nilipoanza'',alisema mshambulizi huyo mwenye umri wa miaka 37.
''Kwani siwezi kuwa meneja ? kwani siwezi kuwa mkurugenzi wa kiufundi,mkufunzi wa chuo cha mafunzo ya wachezaji ama hata mshauri wa washambuliaji ?
Image copyrightBBC World Service
Image captionDrogba anataka kuwa kocha wa Chelsea
Drogba ndiye aliyeifungia Chelsea bao lililoipa ushindi na taji la mabingwa wa bara Ulaya mwaka wa 2012.
Vilevile aliisaidia Chelsea kunyakwa mataji 4 ya ligi kuu ya Uingereza kabla ya kuhamia Canada kujiunga na Montreal Impact.
Chelsea haijakuwa na mwanzo mzuri katika msimu huu baada ya kushindwa katika mechi 7 kati ya 12 za kwanza msimu huu.
Mabingwa hao watetezi wanashikilia nafasi ya 15 katika jedwali la ligi kuu ya Uingereza.
Kumhusu kocha Jose Mourinho, Drogba anasema kuwa mreno huyo angali ana makali ya kuwa kocha wa mabingw hao watetezi.
Image copyrightAFP
Image captionDrogba ndiye aliyeifungia Chelsea bao lililoipa ushindi na taji la mabingwa wa bara Ulaya mwaka wa 2012.
''Kama halmashauri inayosimamia klabu inaimani naye inamaanisha kuwa mmiliki wa klabu Roman Abramovich ana imani naye.''
''Ninafikiri kuwa wachezaji wanaimani naye na kuwa anajitolea kwa kila hali ikizingatiwa hali ngumu iliyoko kwa sasa.''
''klabu inawachezaji wenye hadhi ya juu na wanauwezo wa kujifurukuta na kufufua kampeini yao.''Alisema Drogba

Papa Francis: Dini isitumiwe kuvuruga amani

Image caption
Papa Francis ameongoza ibada ya misa ambayo imehudhuriwa na maelfu ya watu uwanja wa Chuo Kikuu cha Nairobi ambapo amesisitiza umuhimu wa familia katika jamii.
Awali katika mkutano na viongozi wa dini mbalimbali, alisema dini haifai kutumiwa kuvuruga akisema “Mungu ni Mungu wa amani.”
"Jina lake takatifu halifai kutumiwa kutetea chuki na mauaji. Ninajua kwamba mashambulio ya Westgate, Chuo Kikuu cha Garissa na Mandera bado hayajasahaulika. Na sana, vijana wamekuwa wakiingizwa na kufunzwa itikadi kali kwa jina la jini kupanda woga na kuvunja umoja katika jamii,” alisema.
"Ni muhimu sana tuwe manabii wa amani, watu wa amani wanaokaribisha wengine kuishi na amani, umoja na kuheshimiana. Mungu na akaguze nyoyo za wanaohusika katika mauaji na ghasia, na azipe imani familia na jamii zetu."
Mkutano huo umehudhuriwa na viongozi wa makanisa mengine akiwemo kiongozi wa Kanisa la Kiangilikana Kenya Dkt Eliud Wabukala.
Viongozi wa dini ya Kiislamu Kenya pia wamehudhuria mkutano huo, wakiongozwa na Prof Abdulghaful El-Busaidy.
Papa Francis amesema amekuwa akihakikisha kila aendako anatangamana na watu wa dini na imani nyingine.
Misa
Image captionBaada ya misa, waumini waliendelea kupokea komunyo
"Huwa ni muhimu sana kwangu kwamba, ninapofika pahali kutembelea waumini wa kanisa Katoliki, ninakutana na viongozi wa makanisa mengine na dini nyingine. Natumai kuwa wakati ambao tumekuwa pamoja utakuwa ishara ya matamanio ya Kanisa kwa dini zote, ninaomba ikaweza kuimarisha urafiki ambao tayari tunajivunia,” amesema.
Wakati wa ibada ya misa ambayo ilianza saa nne asubuhi, Papa Francis alisisitiza umuhimu wa familia katika jamii na kupinga utoaji wa mimba.
“Afya ya jamii yoyote hutegemea afya ya familia. Kwa ajili yake, na kwa ajili ya jamii, Imani yetu katika neno la Mungu inatuita tuunge mkono familia katika jamii, kuwakubali watoto kama Baraka kwa ulimwengu, na kutetea hadhi ya kila mtu, kwa ndugu zetu wote katika familia moja ya binadamu,” amesema.
Image captionBaadhi ya waumini walitoka Afrika Kusini
“Kwa kutii neno la Mungu, tunahimizwa kuachana na matendo ambayo yanachochea udhalimu miongoni mwa wanaume, kuumiza au kudumisha wanawake, na kutishia maisha ya watoto ambao hawajazaliwa ambao hawana hatia.”
Watu waliohudhuria ibada hiyo walianza kuingia uwanjani mapema na walivumilia mvua ambayo ilianza kunyesha mapema asubuhi
 
 
Blogger Templates