Social Icons

Jumatano, 2 Desemba 2015

Serikali ya Iraq yapinga kutumwa vikosi maalum vya marekani nchini humo


Serikali ya Iraq imeupinga mpango uliotangazwa na Marekani wa kutuma vikosi maalum kupambana na wanamgambo wa itikadi kali wa dola la kiislam-IS nchini humo.Kabla ya hapo wanamgambo wa kishiya wenye ushawishi mkubwa nchini humo walisema watapambana na vikosi hivyo vya Marekani vikiletwa Iraq.Waziri wa ulinzi wa Marekani Ashton Carter,alisema katika kikao cha masuali na majibu cha baraza la wawakilishi jana,vikosi maalum vya Marekani vitapelekwa Iraq.Lengo ni kuwasaidia wanajeshi wa Iraq na makundi ya wapiganaji wa kikurdi-Peshmerga katika juhudi zao za kupambana na wanamgambo wa itikadi kali wa dola la kiislam-IS.Kwa mujibu wa waziri wa ulinzi wa Marekani,wanajeshi hao maalum wa Marekani watakaowekwa Iraq wanaweza pia kusaidia nchini Syria.Wakati huo huo serikali ya Marekani inafikiria uwezekano wa kutuma vikosi maalum vyengine katika nchi jirani ya Syria.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

 
 
Blogger Templates