Social Icons

Alhamisi, 3 Desemba 2015

Kenya yapanda nafasi 27 katika orodha ya FIFA

Image copyright
Image captionKenya yapanda nafasi 27 katika orodha ya FIFA
Licha ya kuondolewa katika kinyang'anyiro cha kufuzu kwa kombe la dunia Harambee Stars ya Kenya imepanda nafasi 27 katika orodha ya hivi punde ya Shirikisho la soka duniani FIFA.
Kenya iliyokuwa imeorodheshwa katika nafasi ya 125 iliwashangaza wengi ilipoilaza Cape Verde bao 1-0 katika mkondo wa kwanza wa mchujo wa kuwania kombe la dunia.
Kufuatia ushindi huo Kenya ilijizolea alama 345 na sasa inaorodheshwa katika nafasi ya 25 barani Afrika na 98 duniani.
Timu hiyo hata hivyo ililazwa 2-0 katika mechi ya marudiano na ikabanduliwa nje ya mchujo huo wa kufuzu kwa mashindanoa hayo.
Kichapo hicho kilifuatia purukushani iliyosababisha timu hiyo kukosa usafiri kwa zaidi ya saa 12 wakiwa katika angatua ya Wilson mjini Nairobi.
Kenya ilifika Cape Verde saa mbili tu kabla ya kuanza kwa mechi hiyo ya marudio na hivyo haikuwa ajabu ilipolazwa 2-0.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

 
 
Blogger Templates