Klabu ya Manchester United imekuwa ikishindwa kufunga magoli ya kutosha kwenye michezo yke mbalimbali hali iyozua taharuki kwa mashabiki, wachezaji wa zamani na hata wachambuzi mbalimbali wa masuala ya yoka duniani wamekuwa wakikosa hali hiyo.
Mambo yameenda mbali zaidi hadi kufikia kukosoa mbinu na mfumo wa kocha mkuu wa klabu hiyo Lois Van Gaal wakidai haziendani au hazifit kwenye klabu ya United kwasababu mbinu hizo zimeshindwa kuzaa matunda kwenye kikosi hicho cha Old Trafford.
United ipo nafasi ya tatu kwenye msimamo wa gili ikiwa na pointi 28 pointi moja nyuma ya vinara wa ligi hiyo Man City pamoja na Leicester City walio nafasi ya pili wakilingana kwa pointi na Man City lakini wakitofautiana wastani wa magoli ya kufungwa na kufunga.
Kikiwa kimecheza michezo 14 ya EPL, kikosi cha United kimefunga magoli 20 magoli 10 nyuma ya Man City na magoli tisa nyuma ya Leicester City.
Mchambuzi wa michezo hususan soka Shaffih Dauda yeye amefanya uchambuzi na kubaini ni kwanini timu ya Manchester United inashindwa kupata magoli mengi, ungana naye kwenye uchambuzi huu ili uelewe yeye mtazamo wake ni upi, je unaendana na wa kwako au mko njia mbili tofauti? Huyu hapa Dauda…
Kwanza kabisa mimi ambacho naweza kukizungumzia kutokana na namna ambavyo naifahamu klabu ya Manchester United katika kipindi cha miaka ya karibuni baada ya watu wengi kuanza kuifaatilia. Mimi nakumbuka kwenye miaka ya tisini (1990s) wakati yupo Eric Kantona, Mark Hughes Brian McClair walivyotoka hao wakaja akina Teddy Sheringham, Dwight Yorke Andy Cole, Ole Gunnar Solskjæ walikuwepo washambuliaji wengi sana.
United imekuwa na washambuliaji wengi sana hata kwenye zama za kina Ruud van Nisterlrooy, wanakuja akina Luis Saha, Cristiano Ronaldo, Carlos Tevez , Dimitar Berbatov. United ni klabu ambayo kwa kipindi cha muda mrefu imekuwa na hazina ya washambuliaji kitu ambacho kimekuwa ni utamaduni wa timu.
Wakati mwingine ilikuwa inawasaidia wao kwa wao kuweza kutengeneza ari ya ushindani kugombania namba na vitu kama hivyo. Kwa wenzetu hiyo ilikuwa ni changamoto chanya timu kuwa na wachezaji wengi kwenye nafasi moja tofauti na Bongo ambapo wakiwepo washambuliaji wanne wenye uwezo mkubwa wanaanza kupigana ‘misumari’ si dhani kama wenzetu wanafanya hivyo, Ulaya ni mtu kupambana kupata nafasi.
Ukirudi leo Manchester United, ina straiker gani ambao tunawazungumzia kwamba hawafungi? Wana mwangalia Wayne Rooney, lakini Rooney amebaki yeye kubebeshwa mzigo mkubwa, Antony Martial ni mchezaji mpya ambaye bado anahitaji muda wa kuzoea. Mchezaji mwngine mbaye yupo ni Memphis Depay naye yupo kwenye msimu wake wa kwanza hata nusu haujafika, nani mshambuliaji mwingine kwenye kikosi cha United? Ni Wayne Rooney tu, amekuja Jese Lingard ambaye wakati mwingine anatumika kama striker kipindi ambacho timu haina washambuliaji.
Kwahiyo mimi kiwepesi kabisa nasema Manchester United haifungi kwasababu haina washambuliaji na wakati Rooney anafunga magoli mengi alikuweo Ronaldo, Tevez Berbatov, hebu niambie Rooney anafanyaje kwa kiwango alichonacho Bebertov akigeuka huku kuna Tevez anapasha pembeni kuna Cristiano Ronaldo ananjaa, na yeye lazima ajitume uwanjani.
Lakini leo yeye ndiyo Captain nani anayempa changamoto kwenye kikosi cha United? Hiyo ilikuwa najaribu kuangalia tu kwa ujumla wake.
Ukirudi kwenye mambo ya mfumo ambayo watu wengi wamekuwa wakimshutumu Louis van Gaal kwamba mbinu zake haziwatengenezei mazingira rafiki washambuliaji wa Manchester United, unarudi palepale washambuliaji wapi? Hamna washambuliaji Manchester United.
Ukisema mbinu za Van Gaal ni mbaya kumbuka kocha huyu amefanya vizuri akiwa na vilabu vingi yeye hajifunzi pale United historia inambeba, amekuwa kocha wa Bayern Munich ikiwa na washambuliaji kama Mario Gomes na Luca Toni walikuwa wanafunga, na wale washambuliaji ni aina ya washambuliaji wasio na mambo mengi uwanjani lakini kwasababu kuna watu walikuwa wanatengezeneza nafasi wao wakawa wanaweka kambani.
Mpaka Luca Toni akaamua kundoka Bayern kutokana na competition ya namba kati yake na Gomes.
Lakini wakati Van Gaal yupo Ajax alikuwa na Patric Kluivert akiwa anachipukia, Nwanko Kanu lakini akaenda Barcelona akakutana na na washambuliaji wengi na wote walikuwa wanafunga. Kwahiyo mimi nadha United inamatatizo kwenye kikosi kwenye idara ya ushambuliaji kwa kutokuwepo washambuliaji wa kutosha ambapo automatically wangeweza kutengeneza upinzani ndani yao.
Kwa hadhi ya klabu kama ya Manchester United ilitakiwa kuwa na washambuliaji kuanzi watatu hadi wanne wa kiwango cha dunia, lakini leo hii kuna straiker gani pale? Baada ya kuondoka kwa Falcao ambaye hakutengenezewa mazingira ya kuaminika akaonekana kama bidhaa ya ziada akashindwa ku-perfom lakini siamini kwamba Falcao sio mshambuliaji mzuri.