Social Icons

Jumapili, 24 Mei 2015

JWTZ WAVAMIA MITAANI SONGEA WAKIWA NA SILAHA ZA KIVITA

Askari wa JWTZ katika mojawapo ya mafunzo yao. 
 Wananchi wa Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma jana walikumbwa na taharuki baada ya askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kuvamia mitaa, ofisi za Serikali na binafsi, benki, nyumba za ibada na katika maeneo ya biashara wakiwa na silaha huku magari yao yakiranda kila kona na kuanza kuwapekea watu wote waliyekutana naye huku wakidai kuonyeshwa vitambulisho.
Hata hivyo, hiyo ni mara ya kwanza kwa wanajeshi hao kuchukua hatua hiyo ambayo ilielezwa kuwa ni sehemu ya mazoezi na mafunzo kwa vitendo.
Wananchi waliohojiwa na gazeti hili kwa nyakati tofuti kufuatia kizaazaa hicho akiwamo Anastazia Mhale alisema alikutana na wanajeshi hao alipokuwa akielekea benki, walimsimamisha na kumuuliza maswali kisha wakamfanyia upekuzi.
“Nilishangaa kusimamishwa na wanajeshi na kutuhoji maswali huku wakitutaka tuwaonyeshe vitambulisho, hali hii iliwakuta hata watu waliokwenda wanakwenda sokoni,” alisema Mhale.
Alisema mbali ya kuwakagua raia, pia walisimamisha kila gari barabarani na kulifanyia upekuzi sambamba na abiria waliokuwa ndani ya magari hayo.
Erasto Haule alisema: “Hata kama hakuna madhara yoyote wangetutangazia kama wanafanya mazoezi, wametutia hofu kubwa,” alisema.
Alisema baadhi ya watu jana walishindwa kutoka kwenda kuendelea na shughuli zao wakihofi kukamatwa na wanajeshi hao.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, Mihayo Msikhela alipoulizwa alisema zoezi hilo ni la kawaida na aliwataka wakazi mjini humo kuwa na amani na waendelee kufanya shughuli zao kama kawaida.
Gazeti hili pia liliwashuhudia askari hao wa jeshi wakiwa wametanda eneo lote la ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, lilipotaka kwenda kuonana na mkuu wa mkoa ili atolee maelezo zoezi hilo.
Alipoulizwa Brigedia Jenerali wa Kamandi ya Kusini, John Chacha alisema hiyo ni sehemu ya mafunzo kwa wanajeshi hao.
Alisema JWTZ hufanya mafunzo mbalimbali ya kujiimarisha ikiwamo ya kulinda miji, maporini na mengineyo.
“Mazoezi haya yameanza leo (jana) na tutamaliza usiku. Mafunzo hayo ni muhimu kwetu, yanatoa mbinu za kujihami na uvamizi wa adui yeyote anayeweza kuingia ndani ya mipaka yetu na kuteka viwanja vya ndege, ofisi nyeti za Serikali, benki au hospitali kubwa, ndiyo maana tunayafanya mahali popote,” alisema.
Hata hivyo, Brigedia Chacha alisema kabla ya kuanza kwa zoezi hilo, walitoa taarifa katika ofisi zote kuanzia ngazi ya kata hadi wilaya kwa lengo la kuondoa hofu ambayo ingeweza kutoa kwa wananchi.

KWA NINI ALIYECHELEWESHA FEDHA ZA WANAFUNZI HAJAGUSWA?

Wiki hii Serikali ilikuwa kwenye mapambano mengine na wanafunzi wa vyuo vikuu ambao waliamua kugoma wakishinikiza kulipwa fedha zao za kujikimu ambazo kiutaratibu zinatoka Bodi ya Mikopo ambayo imedaiwa kuchelewesha fedha hizo kwa zaidi ya wiki 11.
Mbali na kugoma, wanafunzi hao walifanya fujo kwenye Kampasi ya Mabibo na kuharibu vitu kadhaa ambavyo wanatakiwa kuendelea kuvitumia baada ya mgomo kumalizika.
Naibu Waziri wa Fedha (Sera), Mwigulu Mchemba alitoa tamko kwa niaba ya Serikali akiomba radhi kwa kuchelewesha fedha hizo na kuwahakikishia wanafunzi kuwa fedha hizo zitaingia mara moja kwenye akaunti zao na kuwasihi kuendelea na masomo.
Hata hivyo, wanafunzi hao waliendelea na mgomo hadi utashi wao ulipotimizwa. Mgomo huo haukuhusu wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam pekee, bali ulisambaa sehemu nyingine zote, wakiwamo wanafunzi 15 wa Chuo Kikuu cha Dodoma waliokamatwa baada ya kufanya fujo wakati wakidai haki zao.
Pia wanafunzi 400 wa Chuo Kikuu cha Mt Joseph cha jijini Dar es Salaam pia walisimamishwa masomo baada ya kuingia kwenye mgomo wakidai fedha zao za kujikimu zilizocheleweshwa.
Mara kadhaa matatizo haya ya wanafunzi kucheleweshewa fedha zao yamekuwa yakiibuka na imekuwa ni kawaida kwa Serikali kutumia vyombo vyake vya dola kuwatuliza, huku baadhi wakikamatwa na kufunguliwa kesi au kuachiwa kwa tuhuma za kukiuka sheria wakati wa kudai haki zao.
Hata hivyo, matatizo yanapoisha na jitihada za kutafuta suluhisho la kudumu la matatizo yao huishia hapo hapo hadi tatizo jingine linapozuka. Kibaya zaidi ni pale Jeshi la Polisi linalolazimishwa kutumia nguvu za ziada katika kudhibiti wanafunzi na kusababisha baadhi kujeruhiwa, kupotezewa muda zaidi wa masomo na hata kujenga chuki dhidi ya Serikali yao.
Tunadhani kuwa hiyo siyo sahihi kwa sababu haki ya kugoma na kuandamana ni haki ya kimsingi ya kila raia pale anapotaka jamii ijue kile kinachomkera au kumfurahisha. Kwa maana hiyo, maandamano yote ya kupinga au kupongeza, mgomo ni haki ya kila raia, lakini inatakiwa iwekewe utaratibu tu wa kuitekeleza.
Kuzuia maandamano hakutatui matatizo ya wanafunzi na kutumia nguvu za ziada kudhibiti wanafunzi wanaogoma hakutatui matatizo yao. Kinachotakiwa ni Serikali kujipanga kuhakikisha matatizo hayo hayaibuki na kusababisha wanafunzi watumie haki yao ya kugoma au kuandamana.
Wanafunzi kukaa wiki 11 bila ya kupata fedha za kujikimu siyo kitu kidogo na kwanza walistahili kupongezwa kwamba waliweza kuvumilia kwa kipindi kirefu kuishi bila ya fedha za kununulia hata sabuni. Hapa waliosababisha tatizo hilo ndiyo walistahili kuchukuliwa hatua kwanza badala ya wanafunzi.
Hawa watu waliotakiwa kupeleka fedha za wanafunzi lakini wakachelewa kwa wiki 11, wanaendelea kufanya kazi zao wakilipwa mishahara kutokana na kodi za wananchi bila ya kuguswa na kirungu wala kufunguliwa mashtaka, badala yake waziri anajitokeza kuwaombea radhi. Utamaduni huu hauwezi kutuletea mabadiliko.
Inashangaza kuona kwamba hadi leo aliyechelewesha fedha hizo ameachwa bila ya hata kutingishwa wakati waliogoma hadi kufanya fujo kutokana na kucheleweshwa kwa fedha hizo wamesimamishwa masomo, kupigwa na hata kufunguliwa mashtaka. Kwa utamaduni huu nchi itakwenda kweli?

Pamoja na hayo, wanafunzi pia wanatakiwa waanike matatizo yao kwa njia ambayo haitaharibu miundombinu ambayo wanaitumia kwenye masomo na ambayo itatumiwa na vizazi kadhaa vijavyo. Kufanya fujo na uharibifu ni kutowajibika pia kwa nchi yao na vizazi vinavyowafuata.

Ireland yahalalisha ndoa za jinsia moja

Raia wa Ireland
Waziri mkuu nchini Ireland Enda Kenny amesema kuwa Ireland ni nchi ndogo iliyo na ujumbe mkubwa baada ya kupiga kura kwa wingi kuhalalisha ndoa za wapenzi wa jinsia moja.
Mabadiliko hayo ya katiba yaliungwa mkono na zaidi ya asilimia 60 ya wapiga kura kwenye kura ya maoni ya siku ya Jumamosi.
Kanisa katoliki lilifanya kampeni ya kupinga kura hiyo.
Askofu wa mji wa Dublin Diarmuid Martin
Askofu mkuu wa mji wa Dublin Diarmuid Martin alikubali kushindwa na kusema kuwa matokeo hayo ni ishara ya mabadiliko ya kijamii nchini Ireland.
Wale waliokuwa wakiunga mkono ndoa za wapenzi wa jinsia moja waliitaja siku ya jana kuwa ya kihistoria nchini Ireland.

Kiongozi wa upinzani auawa Burundi

Maandamano Burundi
Kiongozi wa chama kidogo cha upinzani nchini Burundi ameuawa kwa kupigwa risasi.
Mwili wa Zedi Feruzi pamoja na wa mlinzi wake ulipatikana nje ya nyumba yake kwenye mji mkuu Bujumbura.
Maandamano Burundi
Mauaji ya mwanasiasa huyo yanafanyika wakati wanaharakati wa upinzani nchini humo wamesitisha kwa siku mbili maandamano yao dhidi ya rais Pierre Nkurunziza kupinga uamuzi wake wa kuwania urais muhula wa tatu.
Uamuzi huo ambao wengine wanasema kuwa unaenda kinyume na sheria umesababisha kuwepo kwa jaribio la kumpindua,maandamano ya wiki kadha na kuhama kwa zaidi ya watu 100,000 kutoka nchini humo.

Jumanne, 5 Mei 2015

Korti yamruhusu Nkurunziza kuwania urais

Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza
Mahakama ya kikatiba nchini Burundi imemruhusu rais Pierre Nkurunziza kuwania muhula wa tatu.
Kulingana na vituo vya redio nchini humo,Jaji wa mahakama hiyo alitoa uamuzi huo mapema leo asubuhi .
Hapo Jana makamu wa mahakama hiyo Jaji Sylvere Nimpagaritse ,alilitoroka taifa hilo akidai kuwa walikuwa wakishinikizwa kutoa uamuzi utakaompendelea rais Nkurunziza.
Rwanda imethibitisha kuwa jaji huyo yuko mjini Kigali.

UMOJA WA ULAYA, UN; TUTAPIGANIA UHURU WA HABARI SIKU ZOTE

IMG_0062

Meza kuu katika maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Habari Duniani. Kutoka kushoto ni  Makamu wa Rais wa Umoja wa Vilabu vya waandishi wa Habari nchini (UTPC), Jane Mihanji, Mkurugenzi wa Mfuko wa Vyombo vya Habari Tanzania (TMF), Bw. Ernest Sungura, Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini Filiberto Sebregondi na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akizungumza katika maadhimisho ya Uhuru wa habari duniani yaliyofanyika mkoani Morogoro.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akizungumza katika maadhimisho ya Uhuru wa habari duniani yaliyofanyika mkoani Morogoro.
Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini Filiberto Sebregondi akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Habari Duniani.
Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini Filiberto Sebregondi akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Habari Duniani.
Meza kuu katika maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Habari Duniani.
Meza kuu katika maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Habari Duniani. Kutoka kushoto ni  Makamu wa Rais wa Umoja wa Vilabu vya waandishi wa Habari nchini (UTPC), Jane Mihanji, Mkurugenzi wa Mfuko wa Vyombo vya Habari Tanzania (TMF), Bw. Ernest Sungura, Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini Filiberto Sebregondi na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez.
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Absalon Kibanda akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Habari Duniani.
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Absalon Kibanda akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Habari Duniani.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari, Maelezo, Assah Mwambene akizungumza katika maadhimio hayo.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari, Maelezo, Assah Mwambene akizungumza katika maadhimio hayo.
Kaimu Meneja wa Uhuru FM, Angela Akilimali (kulia) pamoja na wadau wa vyombo vya habari katika maadhimisho ya siku ya uhuru wa habari duniani.
Kaimu Meneja wa Uhuru FM, Angela Akilimali (kulia) pamoja na wadau wa vyombo vya habari katika maadhimisho ya siku ya uhuru wa habari duniani.
Kutoka kushoto ni Mshauri wa Masuala ya Habari Umoja wa Ulaya, Susane Mbise na Mshauri wa Masuala ya Mawasiliano Umoja wa Mataifa (UN), Hoyce Temu akifuatilia mijadala katika mkutano huo.
Kutoka kushoto ni Mshauri wa Masuala ya Habari Umoja wa Ulaya, Susane Mbise na Mshauri wa Masuala ya Mawasiliano Umoja wa Mataifa (UN), Hoyce Temu wakifuatilia mijadala katika mkutano huo.
Mwanahabari na Bloga, Majid Mjengwa akizungumza katika mkutano huo.
Mwanahabari na Bloga, Maggid Mjengwa akizungumza katika mkutano huo.
Mkurugenzi wa Jamii Media, Maxence Mello akizungumza.
Mkurugenzi wa Jamii Media, Maxence Mello akizungumza.
Meza kuu katika maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Habari Duniani.
Meza kuu katika maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Habari Duniani.
Na Joachim Mushi, Morogoro
UMOJA wa Nchi za Ulaya nchini Tanzania (EU) umepinga vikali vitendo vya kikatili na unyanyasaji ambavyo wamekuwa wakifanyiwa waandishi wa habari na vyombo vya dola vya Serikali wanapokuwa wakitekeleza majukumu yao ambapo ilitokea mwanahabari mmoja kuuwawa. Alisema hawatachoka kukemea matukio hayo ya unyanyasaji kwani yanafifisha uhuru wa habari.
Akizungumza jana mjini Morogoro katika Maadhimisho ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani, Kiongozi Mkuu wa Mabalozi hao, Balozi Filiberto Sebregondi alisema EU itaendelea kupinga namna yoyote ya unyanyasaji kwa wanahabari makundi yote wakiwemo wa mitandao ya kijamii hadi utakapo kuwepo uhuru kamili wa vyombo vya habari.
"...Tulifanya hivyo kwa mauaji yalipotokea na tutaendelea kufanya hivyo siku zote watakapo kamatwa na kupigwa wakiwa kazini...Tunajua huenda haitoshi lakini hii ni kutokana na tofauti mbalimbali za kiutendaji," alisema Balozi Sebregondi.
Alisema kupinga unyanyasaji kwa wanahabari haina maana wanachoandika wanahabari mara zote ni cha kweli lakini ipo namna nzuri ya kushughulikia mvutano kama huo na kusaidia kupata taarifa za kina zaidi zitakazofikia muafaka.
Aidha kwa upande wake Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez ambaye alikuwa mgeni rasmi wa maadhimisho hayo alisema Tanzania inaongoza Afrika kwa kushindwa kuweka utaratibu mzuri wa udhibiti mawasiliano.
Alisema vyombo vya habari ni muhimu katika taifa na hasa kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Taifa unaotarajia kufanyika Oktoba, alisema vyombo vya habari vinaweza kubomoa au kujenga taifa lolote. "...Waandishi ni watu muhimu katika kudumisha demokrasia nchini hivyo kuna kila sababu ya kuendelea kujifunza zaidi.
Maadhimisho ya uhuru wa vyombo vya habari duniani kitaifa yamefanyika mkoani Morogoro na kuhudhuriwa na wanahabari mbalimbali, wakongwe, wadau anuai wa vyombo vya habari huku yakiwa na kauli mbiu ya Usalama wa Vyombo vya Habari katika Dijitali: Uhandishi Mzuri unaozingatia, Usawa wa Kijinsia na faragha.

UBAGUZI WA RANGI, MGOGORO WA KITAIFA MAREKANI

Spika wa Bunge la Baraza la wawakilishi nchini Marekani, John Boehner.
Kufuatia kuongezeka ghasia zitokanazo na ubaguzi wa rangi Marekani, Spika wa Bunge la Baraza la Wawakilishi nchini humo amesema uhusiano baina ya Wamarekani wenye asili ya Afrika na maafisa wa polisi sasa umegeuka na kuwa mgogoro wa kitaifa.
Waandamanaji wakiharibu gari la polisi.

John Boehner katika mahojiano na Televisheni ya NBC amesisitiza kuwa maafisa wa usalama wa umma hawapaswi kujihusisha na vitendo vya utumiaji mabavu. Marekani hivi sasa imekumbwa na mgogoro wa kitaifa. Hiyo ni kauli ya kiongozi nambari tatu Marekani baada ya rais na makamu wake.
Katika mgogoro huo, mamilioni ya Wamarekani weusi au wenye asili ya Afrika daima wananyanyaswa na kufanyiwa ukatili wa maafisa wa usalama na polisi wazungu. Katika kipindi cha mwaka moja uliopita, kumeshuhudia visa kadhaa vya polisi wazungu wakiwafyatulia risasi na kuwaua kiholela Wamarekani wenye asili ya Afrika.
Katika vitendo hivyo vya unyama na ukatili, polisi huwalenga na kuwafyatulia risasi washukiwa ambao aghalabu huwa vijana na mabarobaro. Katika kitendo cha hivi karibuni cha ukatili huo wa polisi Freddie Gray, Mmarekani mweusi baada ya kutiwa nguvuni na polisi mzungu alipigwa na kuadhibiwa vikali ndani ya gari la polisi na kisha kukimbizwa hospitali kutokana na majeraha aliyoyapata.
Akiwa hospitalini alifariki dunia. Kufuatia tukio hilo, mji wa Baltimore umeshuhudia machafuko makali zaidi ya mitaani ambapo wananchi wenye hasira wamejitokeza kulaani ukatili wa polisi wa Marekani. Machafuko hayo yametajwa kuwa mabaya zaidi katika miaka ya hivi karibuni.
Waandamanaji wakiwa na mabango.

Ikumbukwe kuwa katika historia ya Marekani kumeshuhudiwa uasi na maandamano ya Wamarekani weusi wakilalamikia ubaguzi wa rangi nchini humo. Kilele cha malalamikio hayo kilikuwa katika miongo ya 1950 na 1960 ambapo mashinikizo yalipelekea kuidhinishwa sheria kadhaa ikiwemo sheria ya kuwapa Wamarekani weusi haki ya kupiga kura.
Pamoja na hayo, hivi  sasa baada ya kupita zaidi ya miaka 50 tokea kuibuka mapambano ya haki za kijamii Marekani, Wamarekani wenye asili ya Afrika wangali wanakabiliwa na ubaguzi mkubwa na dhulma zisizo na kikomo. Hali imekuwa mbaya kiasi kwamba hivi sasa maafisa kadhaa wazungu katika kikosi cha polisi Marekani wamefyatuliwa risasi katika kile kinachotajwa kuwa ni ulipizaji kisasi.
Weledi wa mambo wanasema hali kama hivyo itaitumbukiza Marekani katika mgogoro mkubwa sana wa kiusalama. Marekani ni moja za nchi zenye idadi kubwa zaidi ya silaha ndogo ndogo miongoni mwa raia. Inakadiriwa kuwa katika kila Wamarekani watatu, mmoja au wawili kati yao wana silaha.
Polisi wakiimalisha ulinzi.

Idadi kubwa ya silaha hizo pia ziko mikononi mwa Wamarekani wenye asili ya Afrika na wasiokuwa wazungu. Kwa msingi huo inadokezwa kuwa iwapo maandamano hayatapelekea kumazilika vitendo vya ubaguzi wa rangi na ukatili wa maafisa wazungu katika vikosi vya usalama, basi natija itakuwa ni kuanza mapambano ya silaha mitaani.
Jamii ya Marekani hivi sasa katika upande moja inakabiliwa na matatizo makubwa ya ubaguzi wa rangi na katika upande wa pili inakumbwa na mgogoro wa kiuchumi na kupungua kiwango cha maisha bora katika jamii na hayo yote yamepelekea kuongezeka mashinikizo ya kila aina.
Ni kwa sababu hii ndio weledi wa mambo wanasema Marekani sasa iko katika dimbwa kubwa la mgogoro wa kijamii ambao unaweza kuwa hatua ya kwanza ya mapinduzi au hata vita vya kitabaka na kirangi. Hatua ya John Boehner, Spika wa Baraza la Wawakilishi ambaye ni kiongozi nambari tatu nchini Marekani kutumia ibara ya ‘mgogoro wa kitaifa’ katika kufafanua kuhusu machafuko ya ubaguzi wa rangi hivi sasa nchini humo ni kengele ya hatari kuhusu kuibuka umwagikaji damu nchini humo.

GOMO WA MADEREVA WAINGIA SIKU YA PILI LEO

Taswira nzima ya mabasi yaendayo mikoani katika Stendi ya Ubungo.MGOMO wa madereva umeingia siku ya pili leo baada ya kuanza jana asubuhi huku wakazi mbalimbali wakiwemo wa jijini Dar wakilazimika kutembea kwa mguu kwenda kwenye maeneo yao ya kufanyia shughuli za kila siku.

Wananchi wakiwa wametaharuki katika eneo la Ubungo kutokana na mgomo unaoendelea.Mitaa mbalimbali ya Jiji la Dar asubuhi hii imeonekana kujaa magari binafsi huku bajaji na bodaboda zikionekana kuwa nyingi kuliko siku nyingine.
Katika Kituo cha mabasi yaendayo mikoani Ubungo, mabasi matatu ya Kampuni ya Shabiby Line yameripotiwa kuondoka kituoni hapo kuelekea Morogoro na Dodoma yakiwa chini ya ulinzi mkali wa eskoti ya askari polisi.

Ijumaa, 1 Mei 2015

Dan Sturridge huenda akafanyiwa upasuaji

Mshambuliaji wa Liverpool Dan Sturridge
Mshambuliaji Liverpool Dan Sturridge huenda akafanyiwa upasuaji ili kutibu tatizo la nyonga linalomsumbua.
Mshambuliaji huyu ameelekea nchi Marekani kwenda kuonana na madaktari Peter Asnis ili kujua kama anahitaji kufanyiwa upasuaji kutibu tatizo lake.
Majeruhi yamekua yakimuandama mshambuliaji huyu katika msimu huu na kushindwa kuonyesha cheche zake za kuzifumania nyavu.
Aliumia mguu mwezi September wakati wa michezo ya kimataifa na kabla ya kuumia misuli akiwa mazoezini.
Akapata maumivu tena mwezi November , yaliyo,muweka nje ya dimba mpaka January 31 ambapo alirud uwanjani kucheza mchezo dhidi ya West Ham na kufunga mabao mawili.
Sturridge alijiunga na Liverpool kwa usajili wa kiasi cha pauni milioni 12 mwezi January mwaka 2013 na amefunga mabao 24 katika michezo yote aliyoichezea timu hiyo
 
 
Blogger Templates