Naibu Waziri wa Fedha Mh;Mwigulu Nchemba hii leo akiwa kwenye Ziara yake ya Kikazi Mkoani Njombe ameagiza Bodi na Mamlaka ya mapato Tanzania(TRA) Kuhakikisha Wanajenga Ofisi ndani ya Mkoa wa Njombe(M) haraka sana ilikuondoa Usumbufu Kwa Wafanyabiashara na Wananchi wanapohitaji huduma muhimu kama Leseni,Tin Number n.k.
Akizungumza na Wafanyabiashara Mkoa wa Njombe hii leo (30/01/2014) kwenye Ukumbi wa TURBO,Mh:Mwigulu Nchemba amesisitiza kuwa Ofisi yake imedhamiria kuhakikisha Njombe inapatiwa huduma zote zinazohusu TRA ilikuondoa usumbufu wanaoupata Wananchi hivi sasa kusafiri nje ya Mkoa kupata huduma.
Kwa muda mrefu Njombe kumekuwa na Ofisi ya TRA ambayo inatoa baadhi ya huduma kama Malipo ya Kodi,Kwenye Ulipaji wa Leseni,Tin No, n.k Wananchi wamekuwa wakilazimika kwenda Mikoa ya karibu kama Mbeya na Iringa kwaajili ya Kushughulikia huduma hizo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni