Social Icons

Jumapili, 19 Januari 2014

MAWAZIRI WAPYA HAWA HAPA.

Katibu Mkuu Kiongozi,Balozi Ombeni Sefue.akitangaza baraza la mwaziri leo.
Hakuna Mabadiliko Ofisi ya Rais
Ofisi ya Makamu Wa Rais - Naibu Waziri Kitwanga amehamishwa na nafasi yake imejazwa na Mhe. Ali Mwalimu
Mwigulu Nchemba amekuwa Naibu Wizara ya Fedha (Sera). Aliyekuwa nafasi hiyo sasa ni Waziri Kamili
Uchumi na Mapato sasa anatoka Janet Mbene na inajazwa na Adam Malima
Dr. Asha rose Migiro sasa ni Waziri wa Katiba na Sheria
Kwenye Ulinzi na Kujenga Taifa ni Dr. Hussein Mwinyi
katika Mambo ya Ndani - Mathias Chikawe
Afya na Ustawi wa Jamii - Naibu wake sasa ni Waziri Kamili; naibu wa sasa ni Dr. Kebwe S. Kebwe
Waziri Mulugo amepigwa chini rasmi . Nafasi yake imejazwa na Jenista Muhagama
D. Sophia Simba amebaki na naibu wake akiwa ni Pindi chana katika wizara ya Jinsia na watoto.
Katika wizara ya Mifugo na Maendeleo yake ni Dr. Titus Kamani mbunge wa Busega atakuwa Waziri mpya. Naibu wake ni Saning'o Kaika Telele na hivyo Wizara nzima imepata mawaziri wapya
Mhe. Ole Medeye Amepigwa chini na nafasi yake kuchukuliwa na George Simbachawene katika wizara ya Ardhi ila bado waziri wake ni Prof. Tibaijuka)
katika kilimo na Chakula waziri ni yule yule na Naibu wake ni Godfrey Zambi.
Wizara ya Habari na michezo waziri ni yule yule Dr. Fenella Mukangara ila naibu wake ni mpya , Mtangzaji wa zamani na mbunge wa Singida Bw. Juma Nkamia.
Maliasili na Utalii Nyalandu amekuwa Waziri Kamili. Naibu ni Mahmood Hassan Mgimwa
Katika Nishati na Madini ni Prof. Sospeter Muhongo na Naibu wake ni Charles Kitwagwa akiichukua toka kwa Simbachawene



THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
Telephone: 255-22-2114512, 2116898
E-mail:  ikulumawasiliano@yahoo.com
    press@ikulu.go.tz             

Fax: 255-22-2113425


    PRESIDENT’S OFFICE,                          THE STATE HOUSE,
         DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL                         COMMUNICATIONS,
           P.O. BOX 9120,  
            DAR ES SALAAM.
                 Tanzania.
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
UHAMISHO NA UTEUZI WA MAWAZIRI NA NAIBU MAWAZIRI
______________________________________________
            Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, amewahamisha na kuwateua baadhi ya Mawaziri na Naibu Mawaziri kama ifuatavyo:-
1.0              OFISI YA RAIS
Hakuna mabadiliko.
2.0              OFISI YA MAKAMU WA RAIS
2.1  Waziri wa Nchi (Muungano) - Hakuna mabadiliko
2.2   Mhe. Eng. Dr. Binilith Satano MAHENGE (Mb)
            Waziri wa Nchi (Mazingira).
2.3    Mhe. Ummy Ali MWALIMU (Mb)
                                                Naibu Waziri                            
3.0              OFISI YA WAZIRI MKUU
Hakuna mabadiliko
            4.0       WIZARA
           
                        4.1  WIZARA YA FEDHA
4.1.1        Mhe. Saada Mkuya SALUM (Mb)
            Waziri wa Fedha
                                    Mhe. Mwigulu Lameck NCHEMBA (Mb)           
                        Naibu Waziri wa Fedha
4.1.2        Mhe. Adam Kighoma Ali MALIMA (Mb)
                                                Naibu Waziri wa Fedha
                       
4.2              WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA
Hakuna mabadiliko
           
4.3       WIZARA YA KATIBA NA SHERIA
4.3.1    Mhe. Dkt. Asha-Rose Mtengeti MIGIRO (Mb)
                        Waziri wa Katiba na Sheria
4.3.2        Naibu Waziri - Hakuna mabadiliko
4.4      WIZARA YA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI
Hakuna mabadiliko
            4.5       WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA
           
4.5.1    Waziri - Hakuna mabadiliko
4.5.2    Mhe. Janet Zebedayo MBENE (Mb)
                                                Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara
            4.6       WIZARA YA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA
            Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi (Mb)
                                                Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa
           
4.7        WIZARA YA UJENZI
Hakuna mabadiliko
4.8       WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
4.8.1    Mhe. Mathias Meinrad CHIKAWE (Mb)
                        Waziri wa Mambo ya Ndani
                       
4.8.2        Naibu Waziri - Hakuna Mabadiliko
           


4.9       WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII
4.9.1        Mhe. Dkt. Seif Seleman RASHIDI (Mb)
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii
4.9.2        Mhe. Dkt. Kebwe Stephen KEBWE (Mb)
Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii
4.10     WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI
4.10.1  Waziri:  Hakuna mabadiliko
4.10.2  Mhe. Jenista Joakim MHAGAMA (Mb)
                                                Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi
14.11   WIZARA YA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA NA WATOTO
14.11.1  Waziri: Hakuna mabadiliko
14. 11.2 Mhe. Dkt. Pindi Hazara CHANA (Mb)
Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto
14.12  WIZARA YA MAENDELEO YA MIFUGO NA UVUVI
14.12.1 Mhe. Dkt. Titus Mlengeya Dismas KAMANI (Mb)
Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi
14.12.2 Mhe. Kaika Saning’o TELELE (Mb)
Naibu Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi
14.13      WIZARA YA KAZI NA AJIRA
Hakuna mabadiliko
                                                              
14.14      WIZARA YA MAWASILIANO, SAYANSI NA TEKNOLOJIA
Hakuna mabadiliko
14.15   WIZARA YA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI
14.15.1  Waziri - Hakuna mabadiliko
14.15.2  Mhe. George Boniface Taguluvala SIMBACHAWENE (Mb)
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi
14.16   WIZARA YA MAJI
14.16.1  Waziri - Hakuna mabadiliko
14.16.2  Mhe. Amos Gabriel MAKALLA (Mb)
Naibu Waziri wa Maji
14.17  WIZARA YA KILIMO, CHAKULA NA USHIRIKA
14.17.1  Waziri - Hakuna mabadiliko
            14.17.2   Mhe. Godfrey Weston ZAMBI (Mb)
Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika
            4.18     WIZARA YA UCHUKUZI
            Hakuna mabadiliko
4.19     WIZARA YA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO
4.19.1  Waziri -  Hakuna mabadiliko
4.19.2  Mhe. Juma Selemani NKAMIA (Mb)
Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo
4.20     WIZARA YA MALIASILI NA UTALII
4.20.1 Mhe. Lazaro Samuel NYALANDU (Mb)
Waziri wa Maliasili na Utalii
                        4.20.2 Mhe. Mahmoud Hassan MGIMWA (Mb)
                                                Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii
4.21     WIZARA YA NISHATI NA MADINI
4.21.1    Waziri - Hakuna mabadiliko
4.21.2    Naibu Waziri (Madini) - Hakuna mabadiliko
4.21.3  Mhe. Charles Muhangwa KITWANGA (Mb)
Naibu Waziri (Nishati)
           
Balozi Ombeni Y. Sefue
KATIBU MKUU KIONGOZI

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

 
 
Blogger Templates