Mawasiliano bora ni muhimu sana
kwa mafanikio yetu katika nyanja mbalimbali. Kama hatuna mawasiliano yaliyobora au hatuwezi kuwasiliana
inavyotakiwa basi itakuwa ngumu kwa watu wengine kutusaidia katika kile
tunachokihitaji. Mawasiliano yasiyo bora au kushindwa kuwasiliana vema
kunadumaza na mara nyingine kuua kabisa mahusiano baina yetu na
wengine. Kwa maana hii basi hauna budi kuzingatia sana maelezo na ushauri kutoka katika mada hii na kuyaweka
maelezo haya katika matendo ili yakusaidie maishani.
Vitu
vya kuzingatia.
Yatazame
au yachukulie mazungumzo yako na wale unaohusiana nao kama majadiliano ya
kawaida tu na sio mashindano.
Hii
itakusaidia kuwa na mahusiano na mawasiliano bora na wengine hususani pale
utakapoyaona yale mnayozungumza mara kwa mara kama majadiliano na siyo mashindano.
Majadiliano ni mazungumzo yenye kusudi la kufikia suluhisho au muafaka
fulani. Ni mazungumzo ambayo yanapotumika nia yake siyo kumuumiza,
kumuumbua mtu bali kutoa nafasi kwa pande zote kufikia matokeo bora.
Mazungumzo
ya yenye ushindani ni yale yenye nia ya kuumiza, kuumbua, kuaibisha, na
kudharaulisha, na ambayo nia yake ni kumuonyesha mshindi na aliyeshindwa
mwishoni mwa mazungumzo hayo.
Wale
wenye tabia ya kuzungumza kiushindani huyachukulia mazungumzo kama nafasi ya
kuonyesha ubabe au kunyanyasa wengine. Hata kama yule mnayezungumza naye
ana nia ya mashindano, wewe fanya majadiliano ya kawaida ili taratibu uweze
kumbadilisha mtazamo wake.
Kuwa
msikilizaji makini na hitaji kusikilizwa pia
Kati
ya alama za uonyesha kuwa wewe ni mwenye mawasiliano bora ni pamoja na uwezo wa
kuwa msikilizaji mzuri. Wako watu ambao hupenda kuongea tu na sio
kusikiliza. Sambamba na hilo, unatakiwa kuomba na wewe pia usikilizwe
vizuri. Muombe yule anayekusikiliza akuache umalize kuongea ndio na yeye aanze
kuongea. Kamwe hamtafikia muafaka wowote ikiwa wote wawili mnaongea kwa
wakati mmoja.
Yafuatayo
yatakuwezesha kuwa msikilizaji mzuri
- Msikilize yule anaeongea kwanza na
kumuelewa
- Fahamu fika kile kinachozungumzwa
elewa nia na dhumuni la majadiliano
- Uliza swali pale unapodhani
hujaelewa ili uweze kuelewa vema nia ya mzungumzaji
- Jaribu kuweka kwa kifupi au kwa
muhtasari kile kilichozungumzwa, mweleze anayezungumza unavyojihisi juu
ya alichokuwa akikieleza, na hakikisha ulimuelewa vema.
- Eleza unavyofikiri wewe.
Mweleze aliyekuwa anazungumza kama umekubaliana nae au la, toa sababu za
kukubaliana au kutokukubaliana.
Kuwa
mzungumzaji mwenye ujasiri.
ujasiri
katika mazungumzo huchochea uhalisi na kuaminika katika kile unachokisema.
Zifuatazo
ni tabia za mzungumzaji bora;
a) Tumia sentensi zinazokuelekea wewe
zaidi ya sentensi zinazo waelekea wengine. Jilenge wewe zaidi ya kuwalenga
wenzako unapozungumza. unapotumia sentensi za “ninyi” au “wewe”
mara nyingi unaweza kuonekana usiye na ujasiri, tofauti na pale unapotumia
sentensi zenye “mimi”. Unaweza kuonekana pia kama usiye yaamini
maneno yako.
Sentensi zenye ujasiri na zenye kukulenga wewe binafsi ni kama vile
“nimefurahi
kukuona”
“Ningependa
kuzungumza na wewe”
“Sijafurahishwa
na maneno yako”
b) Katika mazungumzo yako tumia
zaidi sentensi na siyo maswali. Hii itakuwezesha pia kuonyesha kuwa unaujasiri
katika kile unachokisema na unajiamini wewe mwenyewe pia.
Mfano
wa mazungumzo yakutumia swali: “Hivi ninyi mnamwonaje yule rafiki yetu?”
Badala
yake ungetekiwa kusema “mimi sifurahishwi na matendo ya huyu rafiki yetu”
Au
maranyingine baba wa nyumba anapouliza “Hivi mnadhani nani baba humu ndani?”
hii huonyesha kutojiamini kwake
“Hivi
unafikiri mimi njinga?”
“Hivi
jamani sisi hatupewi huduma?”
Namna
nyingine bora zaidi ya kuuliza swali
Je waweza kunisaidia tafadhali?
Je utakubali kuoana na mimi?
Namna bora ya kuzungumza katika sentensi
- nitafurahi sana ikiwa utakubali
kuoana namimi.
- Nitafurahi sana kupata msaada kutoka
kwako
c) Tumia zaidi sentensi zenye “kukiri”
na sio sentensi zenye lawama. Sentensi zenye ukiri au kukiri ni zile ambazo
anayezungumza anasema kile ambacho angetaka aone kikifanyika au kile ambacho
angependa akione kikitendeka.
Kinyume
chake ni sentensi zenye lawama; hizi ni zile ambazo mzungumzaji ana sema kile
asichotaka, au kile asichokipenda kitokee au kifanyike.
Mfano wa sentensi zenye lawama:
· Sipendi kabisa vile unavyonichukulia
· Sipendi kabisa unavyoniingilia
katika maongezi
Mfano
wa sentesi zenye kukiri; “Ningefurahi kama ungesubiri nimalize kwanza
kuongea halafu na wewe utaongea”
Sentensi
zenye lawama huonyesha ukosefu wa ujasiri kwa mzungumzaji, mbaya zaidi,
sentensi hizi hazisaidii chochote katika kubadili tabia ya yule anayeambiwa
maana hazionyeshi bayana ni nini kinachotakiwa kufanyika.
Sentensi
zenye lawama pia huonyesha wazi tabia yako sugu ya kulaumu, pia huonyesha vitu
usivyovipenda tu, na kuvisahau vile vizuri unavyovipenda. Ni ngumu sana
kumsaidia mtu ambaye analaumu usiku na mchana kuwa hapendi hiki, hapendi kile,
hataki hiki na wala hataki kile na bado hawezi kusema anapenda au kutaka nini
badala yake. Kwa hali hii watu hawa wanabaki kuwa walaumu mara dufu.
Lugha
ya mwili wako iwe nzuri (Positive Body language)
Lugha
ya mwili ni vile tunavyoweza kutumia miili yetu kuonyesha nia zetu. Mwili
ni kiungo muhimu sana cha mawasiliano. Tafiti zinasema kwamba, hata
wakati mtu anazungumza kupitia mdomo, asilimia 60 (sitini) ya ujumbe wake
kupitia au kueleweka sio kwa kupitia maneno ya kinywani mwake bali ni kwa
kupitia lugha ya mwili wake. Jambo hili ndilo hutiliwa mkazo na ule
usemi usemao “matendo husungumza zaidi kuliko maneno”
Lugha
ya mwili huusisha vitu kama vile; muonekano wa sura (facial impression),
mikunjo ya uso, macho yalivyowekwa, kinywa kilivyo tumiwa, pua inavyofanywa
wakati wa kuongea, mikono na pozi ya mwili ilivyo wakati wa kuzungumza.
Ni
vema kujikumbusha kila wakati kuhusu umuhimu wa lugha ya mwili ili itusaidie
kujijua sisi wenyewe na ule ujumbe tunaoutuma.
Hapa
nataka kujaribu kueleza baadhi ya maeneo ya lugha ya mwili ambayo yatakusaidia
kuweza kubadilika au kujirekebisha katika mchakato mzima wa mawasiliano kupitia
mwili wako.
a) Kutembea kwa hatua za kudunda au
kunesa
Kutembea
huku kuwasilisha hisia za ujasiri. Tabia hii huweza kuwa ya asili au ya
kujifanyisha hususani apale unapodhani kuwa unachofanya ni cha muhimu zaidi na
unapoamini kuwa wewe ni bora zaidi. Kutembea kwako kwaweza kuonyesha kila
kinachoendelea akilini mwako.
b) Kupanda au kushuka, uzito au wepesi wa sauti unapoongea
(Tone of voice)
Pale
unapojua hauna ugomvi au uadui na yeyote basi sauti yako itakuwa nzuri, na
yakiasi cha kusikika na yeyote. Vituo vyako na misemo yako itakuwa ya
kawaida na yenye uwiano. Pale unapohisi hofu, au kuwepo kwa wabaya wako, mara
nyingi sauti yako huwa chini na isiyo na ujasiri.
Unashauriwa
kwa hali yoyote ujitahidi kuzungumza kwa sauti ya kati, isiyo chini sana wala
juu sana.
c) Mavazi sahihi
Unapohisi
una nafasi fulani katika jamii au sehemu fulani utajikuta unajali sana
suala la kuvaa kwako. Mavazi huweza kuzungumza nia ya moyo na
huweza kuonyesha picha mbaya au nzuri kwa wanao kutazama. Mavazi ya aina fulani
huweza kukupa tafsiri mbaya kwa watu tofauti na vile ulivyo kihalisia, au kwa
upande mwingine mavazi mengine yamefanya wengine kuonekana kama vile ni wa
maana sana na wakutegemewa wakati uhalisi haukuwa hivyo
d) Pozi zuri la mwili
Kuketi
au kutembea katika mwili ulionyooka huonyesha ujasiri. Hii inamaana kifua
kinakuwa mbele na tumbo ndani kidogo. Hata askari waliojasiri huwa
hulazimika kuwa katika pozi hili. Pozi zuri ni ishara ya ukakamavu na
afya njema pia.
e) Muonekano wa macho
Muonekano
wetu machoni huweza huonyesha hofu, aibu au ujasiri, hususani tunapokutwa
katika maeneo au matukio ambayo hatukutarajia. Muonekano wa macho huthibitisha
ukweli au uongo wa kile tunachozungumza. Muonekano wa macho yetu huweza
pia kuthibitisha kumaanisha au kutokumaanisha, uhakika au kutokuwa na uhakika
katika kile tunachokizungumza. Wako wengine wasioweza kamwe kuwatazama machoni
wale wanaowahofia au kuwaogopa.
f) Ukaribu au mgusano
Tabia
ya kujitenga na wengine huweza kumaanisha kujikweza au kukosa ujasiri.
Jaribu kuwa karibu na wengine zaidi kadri utamaduni wa jamii uliyopo
unavyokuruhusu. Kama kukumbatia kunaruhusiwa katika jamii yako fanya
hivo, kama kushika mkono ndio kunakoruhusiwa basi hakikisha unafanya hivyo,
mara kwa mara. Mgusano wa mwili unamaana kubwa sana katika kuongeza ukaribu
baina ya watu.
g) Ishara za mwili (gestures)
Tumia
ishara unapoongea. Mfano tumia mikono, tumia kichwa na macho kusisitiza
unachoongea. Kuongea tu kwa madomo pasipo kiungo chochote cha mwili,
hufanya mazungumzo yako huwa butu sana. Ishara za mwili tunazitumia
kusisitiza au kuthibitisha tunachokiongea. Ishara hizi za mwili zitumike
taratibu, zisizidishwe sana maana na zaweza kuwabughudhi wengine.
Chris
Mauki
Social,
Relationship and Counseling Psychologist
E-mail: chrismauki57@gmail.com
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni