AAR Healthcare inapenda kukujulisha kuwa kutakuwa na kampeni ya kitaifa ya chanjo ya surua na rubella kuanzia tarehe18 hadi 24 oktoba kituo cha City centre kuanzia saa moja na nusu asubuhi hadi saa kumi na mbili jioni. chanjo zitakazotolewa ni surua rubella kwa watoto wa umri wa miezi 9 hadi miaka 15, vitamin A watoto wa umri wa wa miezi 6 hadi miaka 4, dawa za minyoo kwa watoto wa umri wa mwaka 1 hadi miaka4 na dawa za matende na mabusha kwa watu wazima wenye umri wa zaidi ya miaka 5na kuendelea. Hakikisha familia yako inapata chanjo na dawa hizi muhimu kwa ajili ya kujilinda na magonjwa hatari na kuboresha afya yako.
NBAA YAENDELEA KUTOA ELIMU YA TAALUMA YA UHASIBU KWA WANAFUNZI WA CHUO
KIKUU CHA MZUMBE
-
Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) imeendelea
kutoa elimu na mafunzo kwa vyuo vikuu pamoja na shule za sekondari ikiwa na ...
Saa 7 zilizopita
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni