Social Icons

Jumatano, 24 Juni 2015

Hatutavumilia tishio la usalama

Francois Hollande
Serikali ya Ufaransa sasa imemtaka balozi wa Marekani nchini humo kufika mbele yake kufuatia madai kwamba Marekani iliwachunguza watangulizi wake wawili.
Mtandao wa Wikileaks unasema kuwa kitengo cha ujasusi nchini Marekani NSA kilimpeleleza rais Hollande,Nicholas Sarkozy na Jacques Chiraq kati ya mwaka 2006-12.
null
Marais wa Ufaransa
Bwana Hollande ameitisha kikao cha dharura na kusema Ufaransa haitavumilia vitendo ambavyo ni tishio kwa usalama wake.
Hatahivyo Marekani imesema kuwa haitatoa tamko kuhusu madai fulani ya kiintelijensia.
Ned Price ambaye ndio msemaji wa Baraza la kitaifa la usalama nchini Marekani ameongozea kwamba Marekani hailengi na wala haitalenga mawasiliano ya Hollande.
null
Wikilieaks
Shirika la NSA lilishtumiwa kwa kumpeleleza kansela wa Ujerumani Angela Merkel pamoja na viongozi wa Brazil na wale wa Mexico.

Jumanne, 23 Juni 2015

ASHLEY YOUNG AFUNGA NDOA NA MPENZI WAKE WA TANGU UTOTONI

youg2
Ashley Young amefunga ndoa na mpenzi wake ambae walikua pamoja tangu wapo watoto shuleni. Young aliwai kughailisha siku mbili kabla ya harusi yao mwaka 2011.Shemeji yetu anaitwa Nicky Pike unaambiwa wawili hawa hawajaanza kupenda wakati Ashley amekua superstar, mapenzi yao yapo tangu kitambo. Harusi yao imehudhuliwa na watu mbalimbali akiwe Fabrice Muamba.

young1
young3
young4

Mabondia wataka kukumbukwa Kenya

Bondia wa zamani nchini Kenya Abdullah Kent
Bondia wa zamani wa timu ya taifa ya Kenya Mohammed Abdullah Kent ametoa wito kwa Rais Uhuru Kenyatta kukutana na baadhi ya mabondia walioiwakilisha Kenya hapo awali.
Kent aliyewakilisha Kenya kuanzia mwaka 1973 hadi 1986 amesema kwamba kiongozi wa taifa alimuahidi kukutana nao lakini hajatizimiza ahadi hiyo kufikia sasa.
''Rais mwenyewe alisema anataka tukutane sana atusikize mambo yetu lakini najua ana shughuli zake nyingi za kitaifa. Naomba asisahau kupanga siku tukutane naye sisi mabondia wa zamani,'' alisema Kent
Amemtaka rais Kenyatta kuingilia kati na kuhakikisha kuwa anarudishiwa kipande chake cha ardhi alichopewa na rais mstaafu Daniel Arap Moi katika eneo la Mathare North 1983 ambacho alipokonywa na wanasiasa.
''Mabondia wameiletea Kenya sifa kubwa lakini tumesahauliwa. Katika michezo ya Olympiki ni mabondia na wanariadha tu ambao wameipatia Kenya medali'',aliongezea Kent.
Mbali na Kent na Muchoki, baadhi ya mabondia wengine ambao wako kwenye kundi hilo linalopanga kukutana na Rais Kenyatta ni George ''Mosquito'' Findo, Philip Waruinge na nduguye Sammy Mbogwa, Stephen Thega, Dick ''Tiger'' Murunga, Mike Irungu, Kamau Wanyoike, Isaiah Ikhoni, Aggrey Mwambi, Patrick ''Mont'' Waweru, David Makumba, Stephen ''Vedo'' Okumu, Ibrahim ''Surf'' Bilali, Omar Ahmed ''Kasongo'' na Suleiman Bilali.

PHIL JONES AONGEZEWA MKATABA MAN UTD

Kama kawaida hii ndio mida ya kurekebisha, kuongeza na kupata mikataba mipya kwa wachezaji mbalimbali. Wengine wanakua over priced na wengine under priced ili mradi biashara ifanyike na kila mtu apate chake.Manchester united inategemea kumpa mkataba mpya beki wao Phil Jones wiki hii baada ya mkataba wake wa sasa kuwa unaisha mwishoni mwa msimu ujao. Jones ana miaka 23 hivi sasa na anategea kulipwa £80,000 kwa wiki kwenye mkataba mpya.
Jones alijiunga na Man united akitoka Blackburn kwa ada ya pound milioni 16 mwaka 2011

Rwanda yashtumu kukamatwa kwa afisa wake

Karenzi karake
Rwanda imeshutumu uamuzi wa mamlaka za Uingereza kumkamata kiongozi wake wa ujasusi wa Rwanda, Karenzi Karake, ambaye anatakiwa Uhispania kwa madai ya uhalifu wa kivita.
Waziri wa maswala ya kigeni Louis Mushikwabo ameelezea hatua hiyo kama wazimu na lengo lake ni kukandamiza waafrika akiongezea kwamba inatokana na madai ya watu wanaotaka kuwanyima haki waathiriwa wa mauaji ya kimbari nchini humo mwaka 1994.
Mamlaka ya Uhispania inataka kumhoji bwana Karake kuhusu kuhusika kwake katika mauaji ya raia wakiwemo wafanyikazi wa msaada kutoka Uhispania baada ya mauaji hayo.
Kesi ya Uhispania ilianzishwa mwaka 2008,lakini waandishi wanasema kuna wasiwasi kuhusu ushahidi wa mashtaka.
Makumi ya maelfu ya raia wa Rwanda wanadaiwa kufariki baada ya mauaji hayo ya kimbari aidha kupitia mauaji ya kulipiza kisasi nchini Rwanda ama katika kile waandishi wanataja kama wimbi la mauaji ya kikabila katika taifa jirani la jamhuri ya kidemokrasia ya Congo baada ya wapiganaji wanaoungwa mkono na serikali ya Rwanda kuwalazimisha raia wa kabila la Hutu kutoka katika kambi za wakimbizi karibu na mpaka.
Takriban watu laki nane hususan wale wa kabila la Tutsi waliuawa na wenzao wa kabila la Hutu katika mauaji ya kimbari yaliochukua miezi mitatu.

HARUSI YA KIPRE TCHETCHE

Nimezipata hizi picha kutoka kwenye harusi ya mchezaji Kipre Tchetche ambae ameuaga ukapela na kujiunga na club ya wanandoa. Hongera kwake na shemeji yetu.


Ugumu Wa Maisha Isiwe Sababu Ya Kukufanya Wewe Ukashindwa Kufanikiwa.

Mara nyingi katika maisha yetu tuliwahi kukutana au kukumbana na masaibu, vimbwanga, vioja na mambo mengine mengi ya kukatisha tamaa ya kusonga mbele. Nina uhakika kama kuna baadhi yetu tungepewa fursa ya kuandika mahali kuhusu masaibu yaliyotukuta, basi tungejaza maelfu ya kurasa, kwa sababu ni dhahiri kuna mambo mengi tuliyopitia.


Huenda pengine vingekuwa ni vitabu vingi sana ambavyo vingeweza kuuzika sana. Baadhi wange vitumia kwa ajili ya kujifunza mambo mengi na kuwasahihisha wengine ambao walikatishwa tamaa au wamekatishwa tamaa au na mambo kama hayo.

Lakini kwa bahati mbaya au nzuri kuna wengine hawajapata nafasi hiyo au na wengine imewadondokea na wameipata kwa kutumia vyema nafasi hiyo. Kwa wale waliopata nafasi ya kuandika vitabu ambavyo vimesomwa sana duniani na kuhamasisha watu wengine  na hata kubadili maisha yao, wamekuwa na mchango mkubwa sana na wanakumbukwa daima.

Mfano ni daktari na mtaalamu wa nyurolojia wa Marekani, Ben Carson, ambaye alipitia maisha magumu sana kabla ya kufikia mafanikio hayo. Kutokana na yale aliyokuwa amepitia hadi kufikia kuwa mtu mwenye jina kubwa duniani, aliamua kuandika kitabu ili awahamasishe watu wengine ambao wamepitia masaibu kama aliyoweza kupitia yeye.



Moja ya vitabu vyake vinavyopendwa na vilivyopata kuuzwa sana hapa duniani kile cha “ Gifted Hands” (Mikono iliyobarikiwa). Kitabu kilichoelezea maisha yake kwa ujumla mpaka alipofika kwenye ngazi ya mafanikio aliyopo sasa. Mwanzoni  Ben Carson alikuwa na maisha magumu shuleni. Hali iliyosababisha kuwa wa mwisho darasani mara kadhaa.


Alikuwa akiitwa majina mbalimbali kutokana na hali hiyo, hivyo ikasababisha kuwa mtu wa hasira sana karibu na kila mtu. Akiwa amedhamiria kubadili maisha ya mtoto wake, mama yake alimnyima kuangalia televisheni wala kutoka nje na kucheza na wenzake hadi pale atakapokuwa amemaliza kazi zake za shule kila siku.

Muda huo aliweza kuutumia kusoma vitabu viwili na kuandika taarifa juu ya kile lichokisoma. Baada ya muda fulani wa kuishi maisha hayo tofauti alianza kuona mabadiliko hata shuleni walimu na wanafunzi wenzake walianza kumshangaa.

Aliwahi kusema : “Ni wakati ule ndipo nilipogundua kuwa sikuwa mpumbavu”. Huo ni ulikuwa mwanzo wa kihistoria uliobadilsha maisha yake ambayo yalikuwa magumu kupita kiasi.


Huo ni mfano mmoja tu lakini nafahamu kuwa wapo baadhi ya watu walioandika vitabu kama hivyo kwa ajili ya kuhamasisha watu wengine kuwa imara katika mafanikio na kile wanachokifanya katika maisha yao, ili baadae mbele kuwe kweupe.

Japokuwa siyo rahisi kwa sababu wakati mwingine utafanya hivi, halafu utaambiwa siyo vile. Basi tu watu wengine hulka yaoni kuona unapiga hatua moja mbele halafu unarudi hatua mbili nyuma. Jambo la muhimu ni kutokukata tamaa na kuongeza juhududi zaidi na zaidi kwa kile tunachokifanya. Kumbuka hakuna marefu yasiyo na ncha, hivyo huwezi kubaki kwenye umaskini milele ikiwa utaamua, ni lazima UFANIKIWE hakuna wa kukuzuia.

Jumatatu, 22 Juni 2015

SIMBA SPORT CLUB WAZINDUA TOVUTI YAKE

Afisa Mtendaji Mkuuwa EAG Group Imani Kajula Akimwelezea Jambo Rais wa Simba Sport Club Evans Aveva (Aliyekaa) Wakati wa Uzinduzi wa Tovuti ya Club Hiyo Anayeshuhudia ni Makamu wa Rais wa Club ya Simba Geofrey Nyange ‘Kaburu
Simba Sports Club leo hiiimezindua tovuti yake Ili kukuza  mawasiliano  na  wadau wake mbalimbali  hususani; wanachama, wapenzi, vyombo  vya  habari na wadau wengine muhimu. 
Akizungumza  wakati  wauzinduzi  huo  Rais  wa  Simba Evans Aveva  alisema ‘’Katika dunia na zama  za  utandawazi  tovuti  ndio  na  mitandao   ya   jamii   ndio  njia  kuu ya mawasiliano. Sisi  tuliliona  hili  na  leo  hii  nafurahi  kuwa  Simba Sports Club itazindua  rasmi  tovuti  yake  ambayo  itakuwa  jukwaa  kuu la mawasiliano  na utoaji wa taarifa zake za  club ya   Simba. Natarajia wengi wenu mtaitumia kikamilifu na muhimu zaidi mtatupa mrejesho chanya kuhusu  tovuti yetu’’. 
AfisaMtendajiMkuuwa EAG Group Imani Kajula ambao ni washauri watekeleza ji wa Masokona Biashara wa Simba alisema ‘’Tovuti hii sio tuitaiwezesha Simba kuwapa wadau wake taarifa mbalimbalibali pia  itatumika  kwa  ajili  ya uuzaji  wa  vifaa  vya  Simba, Bidhaa  mbalimbali  mpya  na  muhimu  zaidi  kuwaunganisha   wanachama, mashabiki  na wapenzi wa  Simba  kutumia   mitandao  ya  jamii  iliyo   rasmi  ya  Simba Sports Club’’. 

Mkutano   huo  wa  wandishi  wa  habari   ulitumika  kutaarifu   Wanachama, Wapenzina  Vyombo   vya   habari   juu   ya  kocha   mpya   wa   Simba. Alizungumza  wakati  wakumtambulisha   kocha   mpya   wa   Simba, Rais   Aveva   alisema ‘’Baada ya kupitia  vyeti  na  maombi   ya  makocha   mbalimbali, Napenda  kuwa taarifu kuwa Klabu ya Simba imeingia  kwenye  mkataba  wa   kuifundisha   na   kocha Dylan Kerr raia   wa   Uingereza. Ni kocha   mwenye    uzoefu   wa   zaidi   ya   miaka 30, akiwa  amefanya  kazi  Nchi  mbalimbali  zikiwemo    Uingereza, Scotland, Vietnam   na    AfrikayaKusini’’. 

Aliendelea  kusema ‘’Tunaamini   ujuzi   na   uzoefu wake wa  ukocha na pia kama mchezaji wa kiwango cha juu  utakuwa   chachu   ya   kuifanya   Simba    ifanye    vizuri’’

MAGAZETI YA LEO












 



 






Jumamosi, 20 Juni 2015

Mambo Unayoyapoteza Katika Maisha Yako Kwa Sababu Ya Kuwa Na Hofu.


Kuwa na hofu ni kitu ambacho kila binadamu anacho, lakini kwa bahati mbaya hofu hizi zimekuwa zikiwatesa na kuwaumiza wengi zaidi. Hili limekuwa likitokea hivyo, kutokana na wengi wetu kuwa na hofu zilizopitiliza zaidi.

Je unajua ni madhara kiasi gani ambayo unaweza ukayapata katika maisha yako kutokana na wewe kuwa na hofu nyingi? Kwa haraka haraka naomba nikutajie mambo unayoweza kuyapoteza katika maisha yako ikiwa tu wewe utakuwa mtu wa hofu sana.  

1. Hofu inakupotezea mipango na malengo yako.
Hofu unazokuwa nazo katika maisha yako, mara nyingi huwa ni rahisi kuweza kukupotezea mipango na malengo yako uliyojiwekea. Hii huwa inatokea  kwa sababu unapokuwa una hofu zaidi unakuwa unajikuta unashindwa kufuata malengo yako uliyojiwekea kwa usahihi. Na hilo huwa linatokea pengine kwa sababu ya kuogopa ukubwa wa malengo uliyojiwekea.

Watu wengi kutokana kutawaliwa na hofu nyingi katika maisha yao, wamejikuta wakiwa ni watu wa kushindwa kutimiza karibu malengo yao muhimu ambayo wanajiwekea. Kiukweli ukiwa na hofu nyingi, tambua kabisa kuwa utaharibu mambo yako mengi katika maisha yako. Hivyo basi ni muhimu kuweza kumudu hofu ulizonazo ili kufanikiwa.


 2. Hofu inakupotezea ujasiri.
Unaweza ukawa jasiri na kuweza kusimamia maisha yako kweli, lakini unapokuwa una hofu kwa bahati mbaya huo ujasiri huwa huwa unatoweka. Hiki ndicho kitu kimojawapo ambacho hofu huweza kutupotezea katika maisha yetu. Tambua kuwa kwa kadri unavyozidi kuwa na hofu ule ujasiri na ushujaa wote hutoweka. Huwezi kuwa shujaa wa kweli kama ndani yako umejawa na hofu nyingi.

Kama haunielewi kwa hili sana, tuchukulie kwa mfano umeajiriwa iwe na serikali au kampuni fulani. Wakati huohuo kuna madai au haki fulani unazozidai kwenye eneo hilo unalolifanyia kazi. Ikiwa ndani yako utakuwa na hofu za kufikiri kuwa kwa kudai kwako haki zako unaweza kufukuzwa kazi uwe na uhakika, huwezi kufanya mabadiliko. Kwanini? Ni kwa sababu hofu inakuwa imekupotezea ule ujasiri bila ya wewe kujijua.


3. Hofu inakupotezea uwezo wa kufanya maamuzi sahihi.
Elewa kuwa, hakuna maamuzi yoyote ya maana ambayo unaweza ukayafanya ikiwa ndani mwako una hofu nyingi. Maamuzi yote mara nyingi utakayoyafanya wakati una hofu yatakuwa yana nia ya kukufanya uikimbie hofu hiyo inayokukabili. Hivyo kwa maana hiyo hayawezi kuwa maamuzi sahihi kwako zaidi ya kujilazimisha ili kwako upate unafuu fulani wa kutoka kwenye hofu.

Jaribu kufikiri kidogo katika maisha yako juu ya maamuzi ambayo umewahi kuyachukua ambayo yalikuwa ni ya hofu zaidi. Utakuja kugundua kuwa maamuzi uliyoyafanya hayakuwa yako na si hivyo tu pia hayakuwa sahihi kwako kwa asilimia zote. Bali ni maamuzi ambayo uliyafanya kutokana na hofu zako. Kutokana na hofu hizo ulipoteza uwezo wa kufanya maamuzi sahihi.


4. Hofu inakupotezea fursa nyingi.
Ni rahisi sana kumkuta mtu akifanya kazi ileile hata kwa miaka ishirini bila kuiboresha na kwa bahati mbaya kazi hiyo inaweza kuwa haimsaidii sana hata yeye katika maisha yake. Hiki ni kitu ambacho nimekiona sana kwa maisha ya wengi wakiwa palepale bila kusogea kutokana na kuwa ving’ang’azi wa kazi ambazo hazina tija kwao eti kwa sabau ya mazoea, hivyo ni ngumu sana kwao kuweza kuzibadilisha.

Unapokuja kuchunguza kwa nini inakuwa hivyo kwao, jibu ni rahisi tu hofu walizonazo. Kutokana na hofu zao wanaogopa ikiwa wataacha kazi au watabadilsha biashara maisha yao yatakuwaje? Ni watu ambao hawana uhakika wa njia mpya, hivyo ni bora wabaki hapo walipo. Katika maisha yako hakuna kitu kibaya kama kupoteza fursa kubwa kwa sababuya hofu ulizonazo. Jifunze kuzikabili na zidi kusonga mbele.



5. Hofu inakupotezea furaha na amani ya kweli.
Hakuna utakachoweza kukifurahia katika maisha yako  ikiwa wewe umetawaliwa na hofu nyingi. Kikubwa utakachokuwa ukiwaza tu hizo hofu zako na mwisho wa siku utajikuta ile amani ya kweli ndani yako imetoweka kabisa. Unaweza ukawa shahidi kwa hili kwa kukumbuka zaidi kupitia maisha yako binafsi kuwa kipindi ambacho upo ama ulikuwa na hofu nyingi ni lazima ulikuwa ukikosa ile furaha ya kweli.

Si wewe tu jaribu angalia watu wote iwe jirani zako ama marafiki zako ambao hawana furaha sana. Ukija kuwaangalia sana watu hao kinachowafanya wawe hivyo  mara nyingi ndani mwao wanakuwa wana hofu nyingi zaidi. Hofu hizo huweza kuwapelekea washindwe kujiamini, kujiaona kama vile hawafai na zaidi ya yote furaha wanayokuwa nayo pia huweza kutoweka kabisa katika maisha yao. Hiyo yote inakuja kwa sababu ya hofu.




 
 
Blogger Templates