Serikali ya Iraq imeupinga mpango uliotangazwa na Marekani wa kutuma vikosi maalum kupambana na wanamgambo wa itikadi kali wa dola la kiislam-IS nchini humo.Kabla ya hapo wanamgambo wa kishiya wenye ushawishi mkubwa nchini humo walisema watapambana na vikosi hivyo vya Marekani vikiletwa Iraq.Waziri wa ulinzi wa Marekani Ashton Carter,alisema katika kikao cha masuali na majibu cha baraza la wawakilishi jana,vikosi maalum vya Marekani vitapelekwa Iraq.Lengo ni kuwasaidia wanajeshi wa Iraq na makundi ya wapiganaji wa kikurdi-Peshmerga katika juhudi zao za kupambana na wanamgambo wa itikadi kali wa dola la kiislam-IS.Kwa mujibu wa waziri wa ulinzi wa Marekani,wanajeshi hao maalum wa Marekani watakaowekwa Iraq wanaweza pia kusaidia nchini Syria.Wakati huo huo serikali ya Marekani inafikiria uwezekano wa kutuma vikosi maalum vyengine katika nchi jirani ya Syria.
KAYA 7,816 TANGA ZANUFAIKA NA MPANGO WA BIMA YA AFYA KWA WOTE
-
Na Oscar Assenga,TANGA.
'
Zaidi ya wananchi 20,000 kutoka kaya masikini mkoani Tanga wameanza
kunufaika na mpango wa Bima ya Afya kwa Wote, unaolenga kub...
Saa 12 zilizopita
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni