Social Icons

Jumapili, 5 Oktoba 2014

MAGAZETI YA LEO

 


.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

RAIS DK. SHEIN APOKELEWA PEMBA

IMG_8570
Rais wa Zanzibar na  Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed  Shein na Mkewe Mama Mwanawema Shein  wakisalimina na Viongozi mbali mbali  alipowasili katika uwanja wa Ndege  wa Karume Pemba leo
IMG_8577
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein na Mkewe Mama Mwana Mwema Shein wakisalimiana na Viongozi mbali mbali wa Vikosi vya Ulinzi Pemba mara baada ya kuteremka Ndege katika uwanja wa Ndege wa Karume Pemba leo 
IMG_8595
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein na Mkewe Mama Mwana Mwema Shein wakisalimiana na Viongozi mbali mbali wa Vikosi vya Ulinzi Pemba mara baada ya kuteremka Ndege katika uwanja wa Ndege wa Karume Pemba leo 

Alhamisi, 2 Oktoba 2014

MAGAZETI YA LE0
























Ebola:Maambukizi yaongezeka S Leone

Ebola
Shirika moja la hisani limeonya kuwa kiwango cha visa vitano vya maambukizi ya ugonjwa wa Ebola kila saa nchini Sierra Leone inamaanisha kuwa kuna uhaba mkubwa wa vituo vya afya nchini humo.
Save the Children limesema kuwa kuna visa 765 vipya vya Ebola ambavyo vimeripotiwa katika taifa hilo la Afrika Magharibi huku kukiwa kuna vitanda 327 pekee nchini humo.
Wataalam na wanasiasa wanatarajiwa kukutana mjini London ili kujadili mbinu mpya za kutatua tatizo hilo.
Ni mlipuko hatari wa ugonjwa huo kuwahi kutokea baada ya kuwaua watu 3338 kufikia sasa.
Kuna visa 7,178 ambavyo vimethibitishwa huku mataifa ya Sierra Leone ,Liberia na Guinea yakiathirika vibaya.
Shirika hilo linasema kuwa ugonjwa huo unasambaa nchini Sierra Leone kwa kasi mno huku visa vipya vinavyoripotiwa vikiongezeka mara mbili kila wiki.
Limesema kuwa hata baada ya maafisa wa afya kukabiliana na mlipuko huo katika eneo moja ,ugonjwa umekuwa ukisambaa katika maeneo mengine.
Vilevile viwango vya ugonjwa huo havijaripotiwa kama inavyotakikana kwa kuwa watoto wengi wanaendelea kufariki majumbani mwao ama hata barabarani bila kujulikana.
Mapema mwezi huu ,Uingereza ilisema kuwa itajenga vituo vya afya vyenye vitanda 700 nchini Sierra leone ,lakini vitanda hivyo havitakuwa tayari baada ya wiki moja na kwamba vyengine vitachukuwa miezi kadhaa kukamilika.
Save the Children limesema kuwa iwapo jamii ya kimtaifa haitachukua hatua ,raia wengi wataendelea kufariki majumbani mwao mbali na kutishia kuwaambukiza watu wengi wa familia na jamii nzima kwa jumla

BAKWATA YATANGAZA SIKUKUU YA IDD EL HAJI

Baraza Kuu la Waislam Tanzania, BAKWATA limetangaza kuwa sikukuu ya Idd el Haji itafanyika siku ya Jumapili ya tarehe 5 Oktoba 2014.
Akizungumza na TBC, Kaimu Mufti wa Tanzania ambaye pia ni Shehe Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Ismail Habib Mwakusanya amsesema swala ya sikukuu hiyo itaswaliwa Kitaifa katika msikiti wa Al Farouq uliopo Kinondoni jijini Dar es Salaam na kufuatiwa na Baraza la Idd.
Mufti huyo amewataka Mashehe wa Wilaya na Mikoa kuwatangazia taarifa hii waumini katika misikiti yao.

RASIMU IMEPITA DODOMA,THERUTHI MBILI/3 IMEPATIKANA PANDE ZOTE MATOKEO HAYA HAPA

MWENYEKITI WA BUNGE MAALUM LA KATIBA, SAMUEL SITTA HIVI PUNDE AMETANGAZA RASMI KUPITISHA RASIMU YA KATIBA INAYOPENDEKEZWA BAADA YA MATOKEO KUTANGAZWA.‎HABARI‬ RASIMU YA TATU YA BUNGE MAALUM LA KATIBA NCHINI TANZANIA IMEPITA KWA THELUTHI MBILI ZA WAJUMBE KUTOKA TANZANIA BARA NA ZANZIBAR.

1. ZANZIBAR.
* Sura ya Kwanza Ibara ya 1 hadi 11 imepata theluthi Mbili
* Sura ya Pili Ibara ya Ibara ya 12 hadi 21 imepata theluthi mbili
* Sura ya Tatu Ibara ya 22 hadi 22 hadi

26 imepata theluthi mbili
* Sura ya Nne Ibara ya 27 hadi 30 imepata theluthi mbili
* Sura ya Tano Ibara ya 31 hadi 64 imepata theluthi mbil
*Sura ya Sita Ibara ya 65 hadi 69 imepata theluthi mbili
*Sura ya Saba Ibara ya 70 hadi 75 imepata theluthi mbili
*Sura ya nane Ibara ya 76 hadi 121 imepata theluthi mbili
*Sura ya Tisa Ibara ya 122 hadi 123 imepata theluthi mbili
*Sura ya Kumi Inara ya 124 hadi 157 imepata theluthi mbili
*Sura ya Kumi na Moja Ibara ya 158 hadi 161 imepata theluthi mbili
*Sura ya Kumi na Mbili Ibara ya 162 hadi 202 imepata theluthi mbili
*Sura ya Kumi na Tatu Ibara ya 203 hadi 208 A imepata theluthi mbili
*Sura ya Kumi na Nne Ibara ya 209 hadi 221 imepata theluthi mbili


*Sura ya Kumi na Tano Ibara ya 222 hadi 242 A. imepata theluthi mbili
*Sura ya Kumi na Sita Ibara ya 243 hadi 257. imepata theluthi mbili
*Sura ya Kumi na Saba Ibara ya 258 hadi 269. imepata theluthi mbili
*Sura ya Kumi na Nane Ibara ya 270 hadi 274. imepata theluthi mbili
*Sura ya Kumi na Tisa Ibara ya 275 hadi 289. imepata theluthi mbili

Jumatano, 1 Oktoba 2014

KESI YA MSOFE NA MWENZAKE YAAHIRISHWA


Papa Msofe (katikati) akishuka ngazi za Mahakama ya Kisutu baada ya kesi kuahirishwa.KESI ya mauaji inayomkabili mfanyabiashara Marijan Abubakar ‘Papa Msofe’ na mwenzake, Makongoro Joseph, imetajwa leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam na kuahirishwa hadi Oktoba 13 mwaka huu kutokana na uchunguzi kutokamilika.



Msofe na Makongoro wanakabiliwa na kesi ya mauaji ya Onesphory Kitoli. Kesi hiyo imetajwa chini ya Hakimu Mkazi Hellen Riwa 
Makongoro Joseph (kulia) akisalimiana na mmoja wa wapambe wake.
Watuhumiwa pamoja na wapambe wao wakitoka mahakamani.

WAMAREKANI WAKARIBISHWA KUWEKEZA NCHINI KATIKA MAENEO MBALIMBALI


 Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Balozi Rajabu Gamaha.
  Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Balozi Rajabu Gamaha akisalimiana na Balozi wa Heshima kutoka Michigan Marekani ambaye pia ni Rais wa Taasisi ya  Sumake Global Partiner, Robert Shumake  ambaye aliongozana na ujumbe wa Marekani wa watu 10 na kufanya nao mazungumzo Dar es Salaam leo asubuhi. Ujumbe huo unajumuisha mabalozi wa heshima wa Tanzania nchini Marekani na wafanyabiashara waliopo nchini kwa ajili ya kuangalia fursa za uwekezaji na vivutio vya utalii.
  Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Balozi Rajabu Gamaha (katikati), akizungumza na ujumbe huo.
 Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Balozi Rajabu Gamaha akisalimiana na Balozi wa Heshima kutoka Marekani ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Kufua Umeme ya Tanas Energy Group, William Crawford. Kushoto ni Balozi wa Heshima kutoka California Marekani. Habari zaidi bofya hapa 
 Ujumbe huo ukimsikiliza Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Balozi Rajabu Gamaha. Wa kwanza kushoto na wa pili ni maofisa wa wizara hiyo.
 Ujumbe huo ukimsikiliza Kaimu Katibu Mkuu wa wizara hiyo. Wa pili kushoto ni ofisa wa wizara. 
 Ujumbe huo ukiwa katika mkutano huo na Kaimu Katibu Mkuu.
 Ujumbe huo ukiwa katika mkutano huo na Kaimu Katibu Mkuu.
 Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Balozi Rajabu Gamaha (Wa pili kulia mbele) akiwa katika picha ya pamoja na Ujumbe huo uliofika nchini kuangalia fursa za uwekezaji.
 
 
Blogger Templates