Social Icons

Jumatatu, 9 Septemba 2013

KIM POULSEN AKILI

BAADA YA KUFUNGWA NA GAMBIA - KIM POULSEN ASEMA TAIFA STARS ILISTAHILI KUFUNGWA



Taifa Stars imemaliza vibaya mechi za mchujo za Kombe la Dunia, Kanda ya Afrika baada ya kufungwa na Gambia huku Kocha Kim Poulsen akisema timu yake imefungwa mabao mepesi.


Wenyeji Gambia wameshinda mabao 2-0 katika mechi hiyo iliyochezwa leo (Septemba 7 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Independence ulioko hapa jijini Banjul ukiwa ni ushindi wake wa kwanza katika kundi hilo la C ambapo imemaliza ikiwa ya mwisho ikiwa na pointi nne.


Akizungumza baada ya mechi hiyo, Kocha Poulsen amesema Gambia ilistahili kushinda kwa vile ilitengeneza nafasi nyingi kuliko timu yake, na kuongeza kuwa mabao iliyopata Gambia yalikuwa mepesi.


“Hatukutengeneza nafasi nyingi za kufunga, lakini tukaruhusu mabao mapesi. Nawapongeza Gambia kwani walistahili ushindi. Unapofanya makosa unaadhibiwa. Gambia ilikuwa timu nzuri leo, kwani ilitengeneza nafasi nyingi za kufunga, sisi tukatoa mabao mepesi,” amesema Kim.


Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager imemaliza katika nafasi ya tatu katika kundi hilo lililokuwa na timu nne ikiwa na pointi sita ilizozipata nyumbani kwa kuzifunga Morocco na Gambia.


Hata hivyo, Kim amesema sababu nyingine ya kutofanya vizuri ni kuwakosa wachezaji wanaocheza nje ya nchi na wengine wa kikosi cha kwanza ambao ni majeruhi.


Mabao yote ya Gambia katika mechi hiyo iliyochezeshwa na Munyemana Hudu kutoka Rwanda yalifungwa na nahodha wa timu hiyo Mustapha Jarjue. Alifunga la kwanza dakika ya 44 na kupachika lingine dakika ya 51, mabao yaliyotokana na wachezaji wa Stars kutokuwa makini.

 
Katika mechi hiyo Stars iliwakilishwa na Juma Kaseja, Vincent Barnabas, Erasto Nyoni/David Luhende, Nadir Haroub, Henry Joseph, Frank Domayo, Haruni Chanongo, Amri Kiemba, Mrisho Ngasa, Simon Msuva na Khamis Mcha/Juma Liuzio.

UCHAMBUZI

   TASWIRA YA MATAIFA KWA RAIS PAUL KAGAME

 

TASWIRA ya kimataifa ya Rais wa Rwanda, Paul Kagame, ambaye katika siku za hivi karibuni aliibua mzozo wa kidiplomasia na Rais Jakaya Kikwete, inaonekana kuchukua mwelekeo wa kuchuja badala ya kustawi kwa namna ilivyokuwa miaka michache tu iliyopita, MTANZANIA Jumapili limebaini.

Baada ya kuvuma kwa zaidi ya muongo mmoja sasa, Kagame, aliyekuwa akibeba taswira ya mtu shupavu na shujaa, amegeuka na kuanza kuonekana kiongozi mpenda vita, makuu na rais anayeweza kusababisha kuibuka na kukua kwa ufa mkubwa wa kimahusiano kati yake binafsi na viongozi wenzake wa ukanda huu wa Afrika.


Nje ya bara hili, kuzorota kwa taswira ya kiongozi huyo kunaonekana kuanza kugusa hisia za wachambuzi wa masuala ya kisiasa, wanadiplomasia wanaoheshimika na viongozi wakuu wa mataifa ya Ulaya, Marekani na ndani ya Umoja wa Mataifa.

Siku chache baada ya Rais wa Marekani, Barack Obama, kukaririwa na vyombo vya habari mbalimbali duniani akimtaka Rais Kagame kuacha kukisaidia kijeshi kikundi cha waasi wa M23, kidole hicho cha lawama kinaonekana kuungwa mkono kwa kasi na makundi mengine ya kimataifa.

Kagame, ambaye kwa miaka mingi amekuwa kiongozi kipenzi cha mataifa ya Ulaya na hasa Marekani tangu alipofanikiwa kumaliza mapigano yaliyosababisha mauaji ya halaiki nchini kwake mwaka 1994, katika siku za hivi karibuni taswira yake inaonekana kubadilika na kuchukua mwelekeo wa lawama zaidi kuliko sifa.

Matamko na maandishi yenye mwelekeo wa lawama ambayo yalitolewa dhidi yake katika siku za hivi karibuni yameanza kuchukua mwelekeo unaoonyesha kwamba Kagame wa sasa si yule tena aliyekuwa akitajwa kuwa mfano wa kuigwa wa viongozi wapenda maendeleo na wazalendo wa kweli katika Afrika.

Tukio la hivi karibuni kabisa, ni makala ya uchambuzi iliyochapishwa katika gazeti la Uingereza la The Telegraph, ambayo ilieleza namna majeshi ya Rwanda yalivyokuwa yakijipenyeza ndani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na kutoa misaada ya silaha na vyakula kwa kundi la waasi wa M23, ambalo limekuwa likipigana Mashariki mwa nchi hiyo tangu mwaka 2010.

The Telegraph katika makala yake hiyo lilidurusu ripoti ya Shirika la Kimataifa la kutetea haki za binadamu la Human Right Watch, iliyotolewa mwezi mmoja uliopita, ambayo pamoja na mambo mengine, iliainisha ushahidi wa namna vikosi vya Jeshi la Rwanda vilivyokuwa vikishiriki katika vitendo vya kiharamia ndani ya DRC.

Katika uchambuzi wa ripoti hiyo, The Telegraph limeainisha kwamba ndani ya Rwanda, wanaume na vijana wadogo wenye umri wa miaka 15 wamekuwa wakilazimishwa kupewa mafunzo ya kupigana kijeshi kwa lengo la kulinda maeneo yenye utajiri wa madini katika mpaka wa nchi hizo mbili.

The Telegraph limeandika kuwa licha ya utetezi wa awali wa Uingereza juu ya misaada inayopelekwa Rwanda kuwa haimaanishi nchi hiyo inakwenda vitani Kongo, lakini sasa uhalisia wa tuhuma dhidi Rwanda umejiweka hadharani.

Andrew Mitchell, Katibu wa zamani wa Wizara ya Maendeleo ya Kimataifa nchini Uingereza, alikuwa mstari wa mbele wa kumtetea Rais Kagame dhidi ya shutuma za kuchochea mapigano Kongo, pamoja na kupingwa vikali na mbunge wa nchi hiyo, lakini Julai mwaka jana alifanikiwa kuidhinisha msaada wa pauni milioni 16 kwa ajili ya serikali ya Rwanda.

Awali Mitchell alipata kumshawishi Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameron, kwamba madai yaliyokuwa yakiihusisha serikali ya Kagame na tuhuma za kuwaunga mkono waasi wa M23 hayakuwa na ukweli.

Ushawishi huo ambao ulipingwa vikali na wabunge wa nchi hiyo katika mjadala wa bajeti ya misaada, hatimaye ilisababisha Mitchell alazimike kung’atuka katika nafasi hiyo ya uongozi kwa sababu za kisera.

Kitendo cha wabunge kupinga mtazamo huo wa Mitchell kutokana na kuwa na imani yao kwamba Rwanda imekuwa ikisaidia kundi la waasi wa M23, mrithi wa kiti chake, Justice Greening, alilazimika kufuta misaada ya kifedha kwa taifa hilo yenye thamani ya jumla ya pauni milioni 21 mwishoni mwa Novemba, mwaka jana.

Mwanzoni mwa mwaka huu, Kagame alipata kukaririwa akieleza namna alivyokuwa akikerwa na maamuzi ya Jumuiya ya Kimataifa kuikatia misaada Rwanda, hatua alizozielezea kwamba zitalifanya taifa hilo liendelee kustawi.

Mwishoni mwa wiki iliyopita, ndani ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, ziliibuka tuhuma zilizoelekezwa kwa Kagame na Majeshi ya Rwanda kwa namna walivyokuwa wakishiriki katika mapigano ndani ya DRC.

Alikuwa ni Balozi wa Kudumu wa Ufaransa ndani ya baraza hilo, Alexis Lameck, ambaye alikariri taarifa za kutoka kwa Msemaji wa UN aliyeko Kinshasa nchini Kongo, Edmond Mulet, ambazo zilikuwa zikiinyooshea Rwanda kidole cha namna ilivyokuwa ikishirikiana na M23.

Shutuma mpya dhidi ya Kagame zinakuja ikiwa ni takribani mwezi mmoja sasa, tangu gazeti hili la MTANZANIA Jumapili lilipoandika kwa mara ya kwanza namna taswira ya sasa ya kiongozi huyo inavyoweza kuwa mwanzo wa hatma mbaya kwake.

Katika gazeti hilo, ilielezwa namna Kagame anavyokabiliwa na hatari ya kufikishwa mbele ya Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai (ICC), kama ilivyopata kuwa kwa aliyekuwa Rais wa Liberia, Charles Taylor.

Kama ilivyo kwa Kagame anavyohusishwa na vita ya Kongo, Taylor alituhumiwa kwa miaka mingi kama mbabe wa vita vya Sierra Leone, ambayo iligharimu maisha ya takribani zaidi ya watu 50,000.

Kwa sasa Taylor anatumikia kifungo cha miaka 50 jela, baada ya kupatikana na makosa ya uhalifu wa kivita nchini Sierra Leone.

YOOO! UNAPENDA NISEME......

FAHAMU KWA UFUPI KUHUSUASKOFU MOSES KULOLA

Askofu Kulola alizaliwa Juni 2, 1928 katika Kijiji cha Nyahonge wilayani Kwimba mkoani Mwanza. Ameacha mjane, watoto 10, wajukuu 44 na vitukuu 16. Alifungua makanisa zaidi ya 4,600 ya EAGT ndani na nje ya Tanzania, ikiwemo Zambia, Malawi, Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia Kongo (DRC). Lakini ana nyumba moja tu aliyojengewa na waumini
Ni vigumu kuzungumzia historia ya vuguvugu la uanzishaji makanisa nchini, pasipo kumtaja Askofu Moses Kulola.
Askofu Kulola anajulikana na wengi kama mtu aliye na nia ya dhati kutangaza neno la Mungu, kutokana na kile kinachoonekana wazi kwamba hakujilimbikizia mali kama ambavyo tunaona baadhi ya watumishi wa Mungu siku hizi wanavyomiliki majumba, benki na hata magari ya milioni ya shilingi.
Hali halisi
Kwa namna inavyoonekana nchini, ni kama kuna kundi kubwa la watumishi wanaohubiri kwa lengo la kushibisha matumbo yao zaidi; Hawana mpango thabiti wa kusaidia yatima wala maskini, badala yake waumini ndio wanaonyonywa kwa kutoa zaka na sadaka ambazo baadhi yake hata matumizi yake yamekuwa yakizua maswali.
   
Utumishi wa Mungu na mali
“Hakuna shaka kwamba kama kila nyumba ya ibada Tanzania ingekuwa na mpango thabiti wa kusaidia watu maskini, yatima na watu wengine wenye hali ngumu, hali ya maisha ingekuwa nzuri zaidi kwa wengi. Lakini wapi, baadhi ya watumishi wako ‘bize’ kujaza matumbo, wanaendesha magari ya kifahari yenye thamani ya mamilioni ya shilingi badala ya kutumia fedha hizo kutangaza neno la Mungu au kusaidia wasiojiweza,” anasema Charles Mtanga, mkazi wa Mbezi, Dar es Salaam.
Mtanga anawashauri viongozi wa nyumba za ibada kuwa na mkakati wa kusaidia yatima na watu wengine wasio na uwezo, huku wakiendelea kutangaza neno la Mungu, ili wote waweze kuufurahia ulimwengu.
Utanuzi wa huduma
Kwa  mujibu  wa  Askofu wa EAGT Sengerema, Joshua Wawa, Askofu Kulola alizaliwa Juni 2, 1928 katika Kijiji cha Nyahonge wilayani Kwimba mkoani Mwanza. Ameacha mjane, watoto 10, wajukuu 44 na vitukuu 16.
Katika uhai wake, Askofu Kulola alifungua makanisa 4,600 ya EAGT ndani na nje ya  Tanzania, ikiwemo Zambia, Malawi, Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia Kongo (DRC) na ameacha wosia kwamba makanisa yafunguliwe kadiri inavyowezekana.
Hata hivyo, licha ya kuwa na wingi wote huo wa makanisa, Askofu Kulola anamiliki nyumba moja iliyoko mkoani Mwanza aliyojengewa na waumini.
Askofu Moses Kulola
“Yoooh! Unapenda niseme?” hicho ndicho kilikuwa ‘kibwagizo’ cha  Askofu Moses Kulola wakati wa uhai wake hasa alipokuwa akihubiri mikutano ya injili.
Askofu Kulola alifariki Agosti, 29 mwaka huu  katika Hospitali ya AMI (African Medical Investments) iliyopo Slipway jijini Dar es Salaam.
Mikakati mingine
Askofu huyo mkuu wa EAGT, ameelezewa kuwa  amewahi kwenda Ikulu mara kadhaa kuombea nchi kupitia kwa Rais Jakaya Kikwete.
Rais Jakaya Kikwete alishuhudia hayo wakati wa maziko yake yaliyofanyika Bugando, jijini Mwanza kwamba kwa namna inavyoonekana Askofu Kulola alikuwa ana maanisha kuifanya kazi ya Mungu.
Kufungwa na kunusurika kuuawa
Askofu Kulola amewahi kufungwa gerezani kwa ajili ya kuhubiri injili, pia amewahi kunusurika kifo katika ajali. Rais Kikwete anamzungumzia kama mchungaji aliyekuwa mkweli na aliyeutumia muda wake kusaidia wote bila kujali imani zao za dini.
Maisha yake
Katika maisha yake, Kulola alisoma Shule ya Msingi ya Ligsha Sukuma, mwaka 1939 baadaye akajiunga na taasisi ya usanifu mwaka 1949. Alibatizwa mwaka 1950 katika Kanisa la AIC Makongoro. Alimwoa Elizabeth.
Mwaka 1959 alianza kufanya kazi serikalini, wakati huo huo akihubiri injili katika miji na vijiji. Utumishi wake serikalini ulifika mwisho mwaka 1962, aliamua kujitolea moja kwa moja katika kazi ya kutangaza neno la Mungu.
Mwaka 1964 alijiunga na chuo cha theolojia na kuhitimu 1966. Aliendelea na masomo ya theolojia ndani na nje ya nchi.
Alihudumu kama mchungaji katika Kanisa la AIC kabla ya kuhamia madhehebu ya Pentekoste mwaka 1961-1962 na alifanya kazi katika Kanisa la TAG 1966 mpaka 1991 alipoamua kuanzisha Kanisa la Evangelistic Assemblies God (EAGT) baada ya kutokea mgogoro wa kiuongozi.
Kisa cha Askofu Kulola kuanzisha kanisa lake
Katika kitabu cha Historia ya Kanisa la Tanzania Assemblies of God, mwandishi Dk Jotham Mwakimage anasimulia kiini cha mtafuruku uliolikumba kanisa hilo miaka ya 1980 kiasi cha kusababisha mgawanyiko mkubwa. Anasema kulikuwa na mikutano mikuu ya kanisa hilo kati ya mwaka 1980 na 1982.
“Mkutano mkuu wa mwaka 1980 ulikuwa wa kipekee kwa wale waliohudhuria, kwani ulitawaliwa na ujumbe wa kinabii zaidi, ulifanyika kwenye jengo la udongo lililoko Chuo cha Biblia Dodoma,” kinasema kitabu hicho na kuongeza:
“Kwa mtazamo wangu, mkutano huu haukuonekana kama mkutano wa shughuli za kikanisa, bali kama kusanyiko la uamsho wa kiroho katika kuwatia nguvu wachungaji wa TAG kwa ajili ya huduma za kichungaji.”
Dk Mwakimage anaendelea kusema kuwa kulikuwa pia na mkutano wa aina hiyo pia mwaka 1982. Lengo la mkutano huo uliofanyika pia Dodoma lilikuwa ni kuchagua viongozi wakuu wa kanisa hilo na hapo ndipo kanisa lilipopasuka.
“Sababu ya mgawanyiko ilitokana na ule mtafaruku uliokuwa kati ya wainjilisti wawili mashuhuri waliokuwa na mvuto ambao ni Emmanuel Lazaro aliyekuwa Askofu Mkuu wa TAG na Moses Kulola. Ushawishi wa viongozi hao kiroho ulikuwa mkubwa na uligusa watu wengi,” anasimulia.
Anasema ushawishi huo uliwagusa siyo waumini tu wa kanisa hilo, bali hata wamisionari waliolisaidia kanisa hilo.
“Viongozi hawa hawakukubaliana katika mambo ya msingi na mgongano wao ukawagusa watu wengi na matokeo yake hayakuweza kuepukika.”
“Kabla ya mwaka 1982, sheria ndogo ya uhamisho iliongezwa katika Katiba
“Uhamisho huo haukueleweka vizuri… hasa uhamisho wa Mchungaji Calist Masalu wa Kanisa la Temeke ambalo lilikuwa ndiyo kituo kikuu cha Dar es Salaam kwa ajili ya shughuli za Moses Kulola.”
“Wachungaji, washirika na hata wamisionari hawakuelewa sababu za kuwahamisha wachungaji hao, hivyo wakatafsiri kwamba kumhamisha Mchungaji Masalu kulilenga kuharibu huduma ya uinjilisti za Kulola. Kwa sababu hiyo Mchungaji Masalu akagoma kuhama, akisubiri uamuzi wa mkutano mkuu”. Dk Mwakimage aliyekuwa mjumbe katika mkutano huo uliotawaliwa na minong’ono ya uhamisho wa wachungaji anasema uchaguzi ulifanyika na Lazaro kuchaguliwa kuwa askofu mkuu na Kulola kuwa msaidizi wake. Hata hivyo mambo yakazuka tena.
“Siku iliyofuata wakati wa kipindi cha shughuli, suala la uhamisho wa Mchungaji Masalu likajitokeza tena na hoja kama sharti la Kulola kuikubali nafasi yake hiyo ikaibuka. Kulola alinukuliwa akisema, “Kama uhamisho wa Mchungaji Calist Masalu kwenda Bugando Mwanza hautatangazwa, kuondolewa au kufutwa, basi siko tayari kupokea wadhifa mlionichagua.”
“Huo ndiyo ulikuwa msimamo wa Kulola,” anasema Dk Mwakimage na kuongeza:
“Baada ya hapo Askofu Mkuu Lazaro akasimama kujibu hoja akimpinga Kulola akisema; “Uhamisho wa Mchungaji Masalu utabakia na kamwe hautafutwa wala kubadilishwa”.
Ni kutokana na kauli hizi mbili zilizosigana ikawa ndiyo sababu ya mgawanyiko kutokea. Mgawanyiko huo kwanza ulizaa chuki na kashfa endelevu kati ya makundi hayo mawili hadi leo. Lakini kwa upande mwingine umeyaimarisha makundi hayo, kwani hadi sasa ni madhehebu yaliyokua.
TAG bado yaidai EAGT
Akizungumzia uhusiano kati ya TAG na EAGT hivi karibuni Askofu Mkuu wa TAG, Dk Barnabas Mtokambali, licha ya kusema kuwa makanisa hayo yana uhusiano mzuri, anaongeza kuwa bado kanisa lake linaidai mali zake EAGT. Anaongeza kuwa mwaka 1991 kabla Askofu Kulola hajasajili kanisa lake, Serikali ilimpa sharti la kurejesha mali za TAG ili apate usajili, ndipo alipoweka ahadi ya kurudisha jambo ambalo hakulifanya hadi anafariki.
EAGT haidaiwi
Hata hivyo madai hayo yamekanushwa na Katibu Mkuu wa EAGT, Brown Mwakipesile akisema mgogoro uliopo ni wa kikatiba:
“Hakuna mali yoyote tunayodaiwa na TAG, tatizo letu lilikuwa ni la kikatiba tu,” anasema Mwakipesile. Kanisa la EAGT chini ya Askofu Kulola limeendelea kukua kwa kasi. Tofauti ya uongozi kati ya makanisa hayo mawili ni kwamba, EAGT imekuwa chini ya Askofu Kulola hadi mauti yanamkuta huku TAG ikibadilisha uongozi, kutoka Askofu Lazaro kuja kwa Ranwel Mwenisongole hadi askofu wa sasa Dk Barnabas Mtokambali.

Alhamisi, 5 Septemba 2013


Rais Jakaya Kikwete leo amefanya mazungumzo na Rais Paul Kagame wa Rwanda katika mkutano wa saba wa kimataifa wa nchi za maziwa makuu, unaofanyika Kampala, Uganda.
Haijafahamika mara moja walichozungumza, hizi ni picha za mkutano wao. 

 Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na Rais Paul Kagame wa Rwanda wakati walipokutaba na kufanya mazungumzo ya faragha, katika Hoteli ya Munyonyo Commonwealth Resort, jijini Kampala, Uganda.Picha na Freddy Maro

KILICHO TOKEA BUNGENI LEOIMG_0032 Naibu Spika wa Bunge Job Ndugai akimwamuru Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe kukaa chini, Bungeni Mjini Dodoma Septemba 5, 2013. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)IMG_0069Wabunge wa Chadema wakiwa wamesimama kukaidi amri ya Naibu spika, Job Ndugai ya kuwataka wakae chini , Bungeni Septemba 5, 2013. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)IMG_0073IMG_0104 IMG_0119 IMG_0124Wabunge wa CHADEMA wakipambana na Polisi, Bungeni Mjini Dodoma Septemba 5,2013. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)Askari wa bunge la jamhuri wa Muungano wa Tanzania wakimdhibiti Mhe mbunge wa Chadema jimbo la Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi a.k.a Suga ndani ya bunge wakati akitolewa ndani ya ukumbi wa bunge hilo mjini Dodoma leo.

Rais Kikwete na Paul Kagame wakutanishwa na Rais wa Uganda


Rais wa Uganda, Yoweri Museveni ameitisha mkutano wa dharura wa marais wa nchi za Maziwa Makuu (ICGLR), kujadili hali ya usalama Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Rais Jakaya Kikwete ni miongoni mwa waalikwa kwenye mkutano huo ambao pia unatarajiwa kuhudhuriwa na Rais wa Rwanda, Paul Kagame.


Wakati hali ya usalama Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ikidhoofika, katika siku za karibuni, uhusiano wa Tanzania na Rwanda umekuwa wa shaka hasa baada ya Rais Kikwete kuishauri Serikali ya Rwanda kukaa na wapinzani ili kumaliza mzozo uliolikumba eneo la Maziwa Makuu.

Rais Kikwete alitoa ushauri huo wakati akiwa katika sherehe za maadhimisho ya miaka 50 ya Umoja wa Afrika (AU), zilizofanyika mjini Addis Ababa, Ethiopia. Mkutano wa leo utafanyika kwenye Ukumbi wa Commonwealth Resort, Munyonyo katikati ya Jiji la Kampala.

Kwa mujibu wa taarifa Rais Museveni ameitisha mkutano huo hasa kuzungumzia hatua ya Umoja wa Mataifa kupambana na Kundi la Waasi wa M23.

Mbali na viongozi hao wa Tanzania na Rwanda, viongozi wengine wanaotarajiwa kuhudhuria mkutano huo wanatoka Angola, Burundi, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Jamhuri ya Kongo, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Kenya, Sudan, na Zambia.

Ndugu wa bilionea aliyeuawa Arusha wazimia mahakamani 

Ndugu wa mfanyabiashara Erasto Msuya (43)aliyeuawa kwa kupigwa risasi Agosti 7, mwaka huu, wameangua kilio na kuzimia  katika Mahakama ya Hakimu Mkazi mjini Moshi, Kilimanjaro baada ya mahakama kuhairisha usikilizaji wa kesi hiyo.

Ndugu hao  ni dada wa marehemu, Antuja Msuya na Bahati Msuya ambao katika tukio hilo, wote  walipoteza fahamu.


Hali hiyo ilijitokeza baada ya mahakama kuahirisha kesi hiyo kufuatia maelezo ya upande wa mashtaka kuwa upelelezi haujakamilika na hivyo kuzua simazi na majonzi miongoni mwa watu waliohudhuria usikilizaji wa kesi.


Wakili wa Serikali Stella

Majaliwa, aliomba mahakama kuridhia hoja ya kuahirisha shauri hilo ili kutoa nafasi ya kukamilisha shughuli za upelelezi.
Watuhumiwa walifikishwa mahakamani saa 5: 10, wakiwa ndani ya karandika la polisi.

Washtakiwa hao ni Sharifu Mohammed (31), mkazi wa Kimandolu mkoani Arusha, na Musa Mangu (38), mkazi wa Shangarai kwa Mrefu jijini Arusha.

Wanatuhumiwa kumuua Msuya kwa kukusudia, kinyume cha kifungu cha sheria namba 196 cha kanuni ya sura 16 ya mwaka 2012. Hakimu mkazi wa mahakama hiyo, Theotimus Swai, aliahirisha kesi hiyo hadi Septemba 18 mwaka huu.


Mshtakiwa wa pili katika kesi hiyo Shaiba Mpunga, hakuwepo mahakamani kwa kile kilichoelezwa kuwa ana matatizo ya kiafya.


Mshtakiwa wa kwanza na wa tatu katika kesi hiyo wanatetewa na Wakili Hudson Ndusyepo.
 Watuhumiwa wa kesi ya mauaji ya bilionea wa madini Erasto Msuya,Sharifu Mohamed na Musa Mangu wakiwa mahakamani.
 Ndugu wa marehemu Erasto Msuya wakiwa mahakamani.
 Ndugu wa marehemu Erasto Msuya wakiwa mahakamani.
 Wakazi wa mikoa ya Kilimanjaro na Arusha walifurika mahakamani kusikiliza kesi hiyo.
 Mtuhumiwa Sharifu Mohamed akiteta jambo na wakili wake Mhe. Hudson Ndusyepo mara baada ya kuhairishwa kwa kesi hiyo .
 Dada wa marehemu Msuya aliyefahamika kwa jina la Antuja Msuya baada ya  kupoteza fahamu mara baada ya kuahirishwa kwa kesi.
 Dada wa marehemu Msuya aliyefahamika kwa jina la Antuja Msuya baada ya kupoteza fahamu mara baada ya kuahirishwa kwa kesi.
 Dada wa marehemu Msuya aliyefahamika kwa jina la Antuja Msuya akiangua kilio na baadae kupoteza fahamu mara baada ya kuahirishwa kwa kesi.
 Mdogo wa marehemu Msuya aliyefahamika kwa jina la Bahati Msuya akiwa anasaidiwa kupelekwa kwenye gari mara baada ya kuahirishwa kwa kesi
hiyo.
 Mdogo wa marehemu Msuya aliyefahamika kwa jina la Bahati Msuya akiwa anasaidiwa kupelekwa kwenye gari mara baada ya kuahirishwa kwa kesi
hiyo.
 Mama mzazi wa marehemu Erasto akisindikizwa na wanandugu kwenda kwenye gari la familia.
Umati mkubwa wa wananchi ulifurika mahakamani hapo
CHOMBO ICHO..............

SAMAHANI KWA PICHA MBAYA ZA JERAHA LA WYNE ROONEY LAKINI HILI NDIO JERAHA LA MSHAMBULIAJI HUYO BAADA YA KUGONGANA PHIL JONES MAZOEZINI


Deep cut: Wayne Rooney posted this picture on his Facebook page
Wayne Rooney ametupia picha hii kwenye ukurasa wake wa Facebook
Ouch: The gash on Rooney's head is reminiscent of the leg injury he sustained against Fulham last year
Ouch: The gash on Rooney's head is reminiscent of the leg injury he sustained against Fulham last year

Zoom in: Wayne Rooney's head injury that keeps him out of the World Cup qualifiers has been uncovered
'Horror movie': Rooney sustained the cut in Manchester United training following a challenge from Phil Jones


Other half: Rooney was with his family at the park including wife Coleen (right)
Rooney alikuwa na familia yake akiwemo mkewe Coleen (kulia)

Heads up: Wayne Rooney has been ruled out of England's World Cup qualifiers against Moldova and Ukraine
TATHMINI YA MAJINA KUTOKANA NA HERUFI ZA MWANZO ZA MAJINA HAYO

HERUFI A
Mwenye jina linaloanziana na herufi A ni mtu anayependa mambo makubwa, anajiamini na mwenye uwezo wa kutimiza malengo yake. Ni mtu mwenye tahadhari, mchangamfu na mpenda matukio. Anapenda Kuheshimiwa, anapenda Mamlaka, na ana kiburi, na hasira.

HERUFI B
wenye jina linaloanziana na herufi B ni mtu, mkarimu, muaminifu, na hupenda kazi. Ni Jasiri, shujaa na mkatili katika vita au pale anap
otaka kulinda vilivyo katika himaya yake.

HERUFI C
Mwenye jina linaloanziana na herufi C ni mtu wa kukubadilika badilika, mshindani na hupenda kupigania malengo yao wanayopenda. Ni watu wa wabunifu na wanaopenda mawasiliano.

HERUFI D
Mwenye jina linaloanziana na herufi D ni mtu anayependa usawa, Biashara. Ni watu wanaopenda kuamrisha na mwenye kupenda usafi. Ni jeuri na wenye msimamo.

HERUFI E
Mwenye jina linaloanzia na herufi E ni mtu mwenye roho nzuri ,yenye mapenzi na huruma. mwenye kupenda uhuru katika mapenzi na mchangamfu. Kinyume na hivyo atakuwa ni mtu asiotegemewa na kigeugeu.

HERUFI F
Mwenye jina linaloanzia na herufi F ni mtu mwenye mapenzi,huruma , roho nzuri na ana uwezo wa kuwafariji watu. Ni mtetezi wa watu na mwenye huzuni lakini ni mzito wa kufanya maamuzi.

HERUFI G
Mwenye jina linaloanzia na herufi G ni mtu mwenye mwenye imani ya kidini na nguvu za kiroho. Ana kipaji cha kubuni na uwezo wa kutatua matatizo ya watu. ni mtu mwenye hisia kali,msomi, mpweke na mkaidi wa kukubali ushauri wa kutoka kwa watu.

HERUFI H
Mwenye jina linaloanzia na herufi H ni mtu mwenye ubunifu na nguvu katika biashara, hupata faida kubwa kutokana na jitihada na bidii zake. ni mwenye mawazo mengi, mchoyo na mbinafsi.

HERUFI I
Mwenye jina linaloanzia na herufi I ni mtu mwenye kupenda sheria, ana huruma na utu. Wakati mwingi hajiamini na ni mwenye hasira za haraka.

HERUFI J
Mwenye jina linaloanzia na herufi J ni mtu mwenye matamanio,mkweli, mkarimu na muerevu. asiyekubali kushindwa na hupata mafanikio makubwa. Wakati mwingine anakuwa ni mtu mvivu na aliyekosa mwelekeo.

HERUFI K
Mwenye jina linaloanzia na herufi K ni mtu mwenye jeuri. mwenye msimamo thabiti,mashuhuri na mwenye uwezo wa kushawishi na kuamsha hisia za watu wana uwezo wa utambuzi ambao watu wengi hawana. ni mtu asioridhika na hali ya kimaisha.

HERUFI L
Mwenye jina linaloanzia na herufi L ni mtu wa vitendo, mwenye hisani na aliyejipanga vizuri kimaisha. Huwa wanapata ajali mara kwa mara.

HERUFI M
Mwenye jina linaloanzia na herufi M ni mtu mwenye kujiamini sana, mchapakazi na hupata mafanikio. ni mtu mropokaji,mwenye haraka na mwepesi kukasirika.

HERUFI N
Mwenye jina linaloanzia na herufi N ni mtu mwenye ubunifu, hisia kali na hupenda kuwasiliana lakini ana wivu sana.

HERUFI O
Mwenye jina linaloanzia na herufi O ni mtu mwenye subra, mvumilivu na mwenye bidii ya kusoma. Ni mtu mwenye kupenda kutumikia jamii na mwenye uwezo mkubwa wa kudhibiti hisia.

HERUFI P
Mwenye jina linaloanzia na herufi P ni mtu mwenye uwezo wa kuamrisha na hekima kubwa. Ana nguvu za kiroho lakini anapenda sana kujitumbukiza kwenye mambo ya watu.

HERUFI Q
Mwenye jina linaloanzia na herufi Q ni mtu mwenye kupenda mambo ya asili. Ni watu wasiyoelezeka nawana uwezo wa kuonyesha vitu visivyojulikana hata hivyo ni mtu aliyepooza sana.

HERUFI R
Mwenye jina linaloanzia na herufi R ni mtu mwenye uvumilivu, wenye huruma lakini ana hasira za haraka. Muda wote anakuwa mpenda amani.

HERUFI S
Mwenye jina linaloanzia na herufi S ni mtu mwenye mvuto mkali wa kuleta utajiri. Ni watu wenye maamuzi ya ghafla na hupenda mageuzi makubwa.

HERUFI T
Mwenye jina linaloanzia na herufi T ni mtu mwenye kupenda ushauri wa kiroho, anatumia nguvu za ziada kusaidia watu na hupata mafanikio baada ya muda mrefu. Ni watu wenye hisia kali sana na ni wepesi kushawishika.

HERUFI U
Mwenye jina linaloanzia na herufi U ni mtu mwenye bahati kubwa kwa ujumla. Anapenda uhuru katika mapenzi. Lakini ni mtu mbinafsi, mwenye tamaa na aliyekosa maamuzi.

HERUFI V
Mwenye jina linaloanzia na herufi V ni mtu Mchapakazi, wenye bidii na asie choka. Hata hivyo ni watu wasiotabirika.

HERUFI W
Mwenye jina linaloanzia na herufi W ni mtu muwazi, wachangamfuu kupita kiasi na mwenye uwezo wa kutambua mtu mwema na mbaya. Ni watu wenye tamaa na hufanya mambo ya hatari.

HERUFI X
Mwenye jina linaloanzia na herufi X ni mtu asiyependa kuwekewa vizuizi katika kwenye anasa na ni rahisi kujiingiza kwenye uzinzi na kujitoa uaminifu.

HERUFI Y
Mwenye jina linaloanzia na herufi Y ni mtu mwenye kupenda Uhuru na hawapendi kupingwa jambo lao lolote. Ni watu wanaokosa uamuzi na husababishia kupoteza bahati katika maisha.

HERUFI Z
Mwenye jina linaloanzia na herufi Z ni mtu mwenye kupenda matumaini na amani. Ni wenye msimamo mkali ila wanashauriwa kufikiria kabla ya kuamua jambo.
 
 
Blogger Templates