Social Icons

Alhamisi, 20 Agosti 2015

kaseja atua Mbeya city....jana.

Baada ya kuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu golikipa mkongwe na mahiri Juma Kasejakuwa bila timu na kuhusishwa kujiunga na vilabu mbalimbali hatimaye uvumi huo umemalizika August 19 baada ya kusaini mkataba wa miezi sita wa kuitumikia klabu yaMbeya City kutoka Jijini Mbeya.
IMG-20150819-WA0008 (1)
Mkataba wa Juma Kaseja wa kujiunga na klabu ya Mbeya City umesainiwa August 19 mbele ya meneja wake mpya Athumani Tippo hivyo huo ni mwisho wa uvumi wa habari za Juma Kaseja atacheza wapi msimu ujao, taarifa hizo zinakuwa pigo kwa kocha waMwadui FC ya Shinyanga Jamhuri Kiwelu ambaye alikiri katika vyombo vya habari kuwa ana hitaji huduma ya Kaseja kikosini mwake.
Kabla ya kusaini mkataba na Mbeya City Juma Kaseja alikuwa nje ya uwanja kwa kipindi cha zaidi ya miezi nane baada ya kuingia katika mgogoro wa kimkataba na iliyokuwa klabu yake ya zamani ya Yanga nakufanya kesi hiyo kutinga mahakamani.

Rais Nkurunziza aapishwa kwa muhula wa 3

Rais Nkurunziza aapishwa
Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza anaapishwa kwa muhula wa tatu uliozua utata.
Mwandishi wa BBC Prime Ndikumagenge nchini Burundi anasema kuwa sherehe hiyo imefanyika kwa mshangao mkubwa kwa kuwa rais Nkurunziza alitarajiwa kuapishwa wiki ijayo.
Rais Nkurunziza
Takriban watu 10 wameuawa tangu Nkurunziza atangaze mnamo mwezi Aprili kwamba atawania muhula wa tatu wa urais.
Serikali inaushtumu upinzani ambao unasema kuwa muhula huo ni kinyume na sheria kwa kuzua ghasia.
Nkurunziza
Umoja wa Afrika,muungano wa Ulaya na wizara ya maswala ya kigeni ya Marekani wote wameonyesha wasiwasi wao kwamba uchaguzi huo wa mwezi Julai haukuwa huru na wa haki.

IS lakiri kutekeleza shambulizi Misri

Cairo
Bomu kubwa limelipuka karibu na makao makuu ya usalama kaskazini viungani mwa mji mkuu wa Misri, Cairo.
Watu 29 walijeruhiwa katika mlipuko huo ikiwemo maafisa sita wa polisi.
Bomu hilo lilisikika katika maeneo mengi ya mji huo na mwandishi wa BBC anasema kuwa hayakuwepo majeraha mengi kwa kuwa mlipuko huo ulitokea usiku.
Mlipuko Cairo
Eneo hilo kwa sasa limefungwa na kuna maafisa wengi wa polisi katika barabara za mji huo.
Kundi la wapiganaji wa Islamic State limekiri kutekeleza shambulizi hilo.

Pedro:Kwanini ni chaguo la Chelsea?

Pedro Rodriguez
Chelsea wanaonekana kuishinda kasi Manchester United katika kumsajili Pedro baada ya timu hiyo ya London kukubali kutoa kitita cha paund milioni 21 kwa mchezaji huyo mwenye miaka 28.
Pedro kwa sasa yupo katika hatua za mwisho kukamilisha usajili wake huku mashabiki wa Chelsea wakiwa na msisimko mkubwa kumtizama mchezaji huyo akiwaruudhisha katika mbio za ubingwa wa mataji mbalimbali.
Pedro
Pedro anatazamiwa kujijengea umaarufu kwa mashabiki wa Chelsea kutokana na kuwa msikivu na mnyenyekevu huku pia akiwa na shauku ya kucheza ambapo mashabiki wa Uingereza hupenda watu kama hao.
Atapata ukaribisho mzuri pia katika vyumba vya kubadilishia nguo vya Chelsea kutoka kwa wachezaji wenzake kwa sababu sio mbinafsi,ni mpambanaji na mkarimu ambaye anaweka mahitaji ya timu mbele kuliko ya kwake binafsi.
Pedro wakati akiwa Barcelona, alikua akitumika zaidi kama mchezaji wa akiba licha ya kuifanyia makubwa timu hiyo.

MAGAZETI YA LEO





PICHA YA SIKU

KINGWENDU ACHUKUA FOMU YA UBUNGE

KIPINDUPINDU KIPO JIJINI DAR ES SALAAM TUWE MAKINI.


 Muuguzi Mkuu wa Manispaa ya Kinondoni, Nusura Kessy (kushoto), akiwaelekeza wauguzi wa saidizi wake namna ya kuchanganya dawa maalumu ya kuondoa vijiji vinavyoweza kuwa vya ugonjwa wa kipindupindu katika kambi ya wagonjwa walioathiriwa na ugonjwa huo iliyopo Zahanati ya Mburahati Dar es Salaam leo asubuhi. Katika kambi hiyo kuna wagonjwa 21 kati yao watoto ni 7.
 Vyombo vikiwekwa kwenye dawa.
 Muuguzi Msaidi wa Zahanati ya Mburahati, Maimuna Pazi (kushoto) na Mlinzi wa Zahanati hiyo, Abdallah Mbagala wakisaidiana kuweka dawa maalumu ya kuzuia kuenea kwa vijidudu vya maambukizi ya ugonjwa wa kipindupindu katika vyombo walivyoletewa chakula na ndugu zao katika kambi ya matibabu kwa wagonjwa walioathiriwa na ugonjwa huo iliyopo katika Zahanati ya Mburahati Dar es Salaam leo asubuhi.
Dawa hiyo maalumu ikiwekwa katika vyombo vya kutumia.



HALI ya ugonjwa wa kipindupindu ulioikumba maeneo kadhaa ya jiji bado inaonesha ni tete kufuatia idadi ya wagonjwa huo kuongezeka kutoka watu 34 na kufikia 43.

Hayo yamebainishwa na Muuguzi Mkuu wa Manispaa ya Kinondoni ambayo imeathiriwa na ugonjwa huo, Nusura Kessy wakati akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi.

Kessy ambaye anasimamia kutoa huduma katika kambi ya wagonjwa iliyopo Zahanati ya Mburahati alisema mpaka jana asubuhi kulikuwa na wagonjwa 21 kati yao watoto ni saba na wagonjwa 10 wameruhusiwa kurudi majumbani mwao baada ya hali zao kuimarika.

"Hali bado sio nzuri kwani tunaendelea kupokea wagonjwa kutoka Hospitali ya Mwananyamala hata hivyo uwezo wa vyumba vya kulaza wagonjwa ni watu 16 tu" alisema Kessy.

Alisema kutokana na changamoto hiyo wameomba mahema ambayo yatafungwa nje ya zahanati hiyo kwa ajili ya kusaidia ongezeko hilo la wagonjwa.

Kessy alitunmia fursa hiyo kuwaomba wananchi kuzingatia usafi hasa baada ya kutoka kujisaidia kunawa kwa kutumia maji ya moto na kuto kula vyakula holela pamoja na kuchemsha maji ya kunywa.

Muuguzi huo pia alitoa mwito kwa wananchi pale wanapo muona mtu anatapika na kuharakisha kutoa taarifa mapema na kumpeleka mgonjwa hospitali kwa matibabu.

Alisema kuwa kati ya watu waliopoteza maisha kwa ugonjwa huo kati yao ni walifariki wakiwa majumbani na njiani wakati wakipelekwa hospitali wakiwa katika hali mbaya baada ya kucheleweshwa

Jumatano, 19 Agosti 2015

ZARI ASEMA WATAIONESHA SURA YA TIFFAH BAADA YA SIKU…


Shauku kubwa ambayo mashabiki wa Diamond Platnumz na Zari the Boss Lady wako nayo kwa sasa ni kuiona sura ya mtoto wao wa kike Latiffah Naseeb a.k.a Princess Tiffah.

Hii ni kutokana na maneno mengi ambayo yanaendelea hivi sasa kwenye mitandao ya kijamii, wengi wanahamu ya kujua mtoto anafanana na nani kati ya baba na mama yake.

Picha zote za Tiffah zilizowekwa kwenye mitandao ya kijamii zinamuonesha mikono, miguu, mdomo lakini amekuwa haoneshwi sura yake.

Shabiki mmoja alimuuliza swali Zari kupitia ukurasa wake, ni lini wana mpango wa kuionesha sura ya Tiffah, na jibu la Zari lilikuwa “Baada ya siku 40”.

Hadi sasa ukurasa wa Instagram wa Princess Tiffah una followers 87,650.

704 wahamia chadema,jimbo analo gombe mgombea wa CCM Nape.




Aliyekuwa mgombea wa kura za maoni kupitia chama cha mapinduzi jimbo la mtama SELEMANI METHEW amekihama chama hicho na kuondoka na wana CCM wapatao 704 na kuhamia chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA kwa kile anachodai hakutendewa haki katika mchakato mzima wa kura za maoni.

METHEW amesema kuondoka ndani ya CCM kumetokana na maamuzi ya wananchi ambao wameona haiwezekani na haitawezekana kiongozi wanayemuitaji kufanyiwa hila na mizengwe,kudhulumiwa haki yake ya msingi ya kuwaongoza wananchi wa jimbo la mtama.

Amesema jimbo la mtama halihitaji usanii bali linaitaji mgombea shupavu atakayeweza kupambana na mgombea wa CCM Nape Nnauye huku akisisitiza uwezo huo anao.

Mkutano huo umeudhuriwa na wanawake wengi ambao kwa sehemu kubwa ndiyo waliorudisha kadi za CCM.

Mkutano huo ulipambwa na vimbwanga mbalimbali likiwemo tambiko rasmi lililotumika kumzindika mgombea huyo ikiwa ni pamoja na kumpa nguvu na kumkinga na majanga ili aweze kufanikisha kampeni na kuibuka na ushindi.

UKAWA WAKINGAZA MAJIMBO WALIYOGAWANA KATIKA UCHAGUZI MKUU


 Kaimu Katibu Mkuu wa Chama cha NCCR-Mageuzi,  Nderakindo Kessy (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Makao Makuu ya chama hicho, Ilala Dar es Salaam jana, wakati akitangaza majimbo yaliyochini ya vyama vinavyounda Ukawa ambayo vyama hivyo vitasimamisha wagombea wao katika uchaguzi mkuu. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha NLD, Masudi Makunjunga.
 Kaimu Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Shaweji Mketo (wa pili kulia), akizungumza katika mkutano huo na waandishi wa habari. Kutoka kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha NLD, Masudi Makunjunga, Kaimu Katibu Mkuu wa Chama cha NCCR-Mageuzi,  Nderakindo Kessy na Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), John Mnyika.
 Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), John Mnyika, akizungumza katika mkutano huo.
 
 
Blogger Templates