Social Icons

Jumamosi, 22 Novemba 2014

Zaidi 28 wauwawa na wanamgambo Kenya

Wanamgambo wa al-shabaab wanaaminika kutekeleza mauaji hayo.
Polisi nchini Kenya wanasema kuwa wanamgambo wanaoshukiwa kuwa wa kundi la Al Shabaab wamewauwa kwa kuwapiga risasi zaidi ya watu 28 waliokuwa wakisafiri kwenye basi moja karibu na mpaka wa Somalia.
Maafisa wa ngazi ya juu wamesema kuwa basi hilo lilitekwanyara katika Jimbo la Mandera wakati likiwa njiani kuelekea katika mji mkuu Nairobi.
Watu wasiokuwa waislamu wanasemakana kutengwa na abiria wengine na kisha kupigwa risasi.
Kundi la al-Shabab nchini Somalia limetekeleza mashambulizi kadhaa nchini Kenya tangu mwaka 2011.
Huo ndio mwaka ambapo Kenya iliwatuma wanajeshi wake nchini Somalia kupigana na kundi hilo la waislamu wenye itikadi kali.
Mji wa Mandera katika eneo la Kaskazini mashariki ndio ulioathirika pakubwa. Baada ya shambulio hilo la mapema jumamosi maafisa katika eneo hilo wamenukuliwa na vyombo vya habari nchini kenya wakisema kuwa serikali ilikataa kuitikia ombi lao la kutaka usalama kudumishwa zaidi.
Afisa mmoja ameliambia gazeti la Daily Nation kwamba wavamizi hao waliwataka abiria kusoma aya katika Koran kabla ya kuwaangamiza walioshindwa kufanya hivyo.

JAMAA ALIYEMTWANGA MKEWE TALAKA SIKU YA HARUSI




Jamaa mmoja kutoka nchini Saudi Arabia amempa talaka mkewe siku ya harusi baada ya kumuona uso wake kwa mara ya kwanza. Maharusi hao kutoka mji wa Saudia,Medinah walikubaliana kuoana pamoja na kujua kabisa hawajawahi kuonana sura zao,swala ambalo ni utamaduni mkubwa wa mataifa ya kiarabu.
Lakini wakati mwanamke huyo alipofungua kitambaa cheupe kilichopo katika shela alichokuwa amejifunika uso na kutabasamu katika kamera,mumewe alishtuka na kuondoka wa ghafla.
Mwanamume huyo alianguka na kuzirai huku wageni waalikwa wakijaribu kuingilia kati ili kutatua kilichokuwa kikiendelea. Hata hivyo Bwana harusi alisema kuwa hakuweza kumwona bi harusi kabla ya harusi yao.
'' Si wewe msichana niliyetaka kuoa,si wewe kamwe niliyedhani '' kwa hivyo nakupa talaka''alisema bwana harusi.
Na alipompa talaka bi harusi naye alianguka na kuzirai na kuifanya harusi hiyo kuwa usiku wa majonzi.

Ujue Mmea wa Mlonge na faida zake kwa binadamu(Moringa Tree)



1. Karibu kila sehemu ya mti wa Moringa inatumika au inalika kama chakula. Majani ndio sehemu kuu ya mti wa Moringa, unaweza kuyala yakiwa mabichi au yakiwa yamepikwa kama mboga yoyote ya majani, na pia unaweza ukayakausha na kuyahifadhi kama unga-unga kwa miezi mingi huku ukitumia kama kiungo kwenye mboga na mchuzi. 

Pia majani yanaweza kutumika kama lishe bora ya mifugo.

Utafiti wa kisayansi umeonyesha kuwa majani ya Moringa ni chanzo kikubwa cha virutubishi vingi sana. Virutubishi hivi ni pamoja na;

Vitamini C - Kirutubishi hiki ni muhimu katika kutengeneza kinga ya mwili dhidi ya magonjwa mbalimbali. Kiwango chake katikamajani ya Moringa ni zaidi ya mara saba ya ile inayopatikana kutoka kwenye machungwa.

Calcium (madini chuma) - Kirutubishi hiki ni muhimu katika kuimarisha pamoja na kujenga mifupa na meno mwilini. Kiwango chake katika majani ya Moringa nimara nne zaidi ya yale yanayopatikana kutoka kwenye maziwa.

Protini - Kirutubishi hiki ni muhimu katika kujenga mwili na kuimarisha ngozi. Kiwango chake katika majani ya Moringa ni mara mbili zaidi ya ile inayopatikana kutoka kwenye maziwa.

Vitamini A - Kirutubishi hiki ni muhimu katika kuimarisha macho na kuongeza uwezo wa kuona. Kiwango chake katika majani ya Moringa ni mara nne zaidi ya ile inayopatikana kutoka kwenye Karoti.

Potassium - Kirutubishi hiki ni muhimu katika kujenga na kuupatia mwili nguvu. Kiwango chake katika majani ya Moringa ni mara tatu zaidi ya ile ipatikanayo kutoka kwenye ndizi. Maua ya Moringa yamejaliwa madini chuma (calcium) na Potassium kwa wingi na yanaweza kuchemshwa au kupikwa na kuliwa kama mboga. 

2. Mboga
Majani ya Moringa huliwa kama mboga nyingine za majani kwa mfano mchicha. Majani yanaweza kuvunwa wakati wa kiangazi ambapo mboga nyingine hazipatikani. Pia matunda mateke ya Moringa huweza kutumika kama mboga, hutayariswa kama maharage mabichi (machanga). Matunda yalikomaa hutoa mbegu ambazo zinaweza kutumika kama njegere au kukaangwa kama karanga.

3. Mafuta
Mafuta kutoka kwenye mbegu za mti wa Moringa huweza kutumika katika kupikia na kuwasha katika nyumba. Pia hutumika sana kwenye viwanda katika utengenazaji wa sabuni na bidhaa za urembo. Mafuta hukamuliwa kutoka kwenye mbegu kama ambavyo alizeti hukamuliwa.

4. Lishe ya Mifugo
Majani ya Moringa huliwa na ng’ombe, mbuzi, kondoo, sungura na kuku. Mbegu huliwa na kuku pamoja na wanyama wengine kwenye jamii ya ndege.

5. Pambo la nyumba
Mti wa Moringa hupandwa kwa wingi kwenye bustani kama ua au mti wa kivuli na hutumika katika upambaji. Pia miti ya moringa ikipandwa karibu karibu inaweza kutumika kama fensi.

6. Chanzo cha kipato
Mti wa Moringa ukitumiwa vizuri ni chanzo kizuri cha kipato. Mfano ni uuzaji wa miche ya mti wa moringa na utengenezaji wa bidhaa zitokanazo na moringa.

7. Tiba mbadala 
Moringa ni mti muhimu sana katika utabibu kama tiba mbadala, majani, maua, mbegu na mizizi yake hutumika sana katika kutibu magonjwa mbalimbali.


Majani



  • Majani mabichi ya Moringa ni mazuri kwa kina mama wajawazito na wenye kunyonyesha, huongeza wingi wa maziwa na hushauriwa kwa kutibu Anaemia.
  • Juisi ya majani ya Moringa hutumika kusafisha tumbo na hutibu magonjwa ya zinaa. Juisi ikichanganywa na asali inatibu kuharisha.
  • Pia juisi ina uwezo wa kusawazisha presha (BP) na kudhibiti viwango vya sukari kwa wagonjwa wenye
  • kisukari.
  • Majani pia huweza kupakwa mwilini katika kutibu majipu na maambukizi ya ngozi.



Mbegu


  • Mbegu za mti wa Moringa ni kinga dhidi ya vijidudu (bacteria) wasababishao magonjwa na kuathiri ngozi.
  • Pia mbegu hutuminka katika kusafisha au kuchuja maji ambapo zikipondwa na kuwekwa kwenye maji yenye tope au machafu husababisha uchafu kujikusanya na kuzama chini kisha kuacha maji yakiwa safi na salama kwa kupikia au kunywa baada ya kuchemsha.



Magome


  • Magome ya mti wa Moringa hupondwa na kuwa rojorojo kisha hutumika kutibu majipu pia hupakwa ili kupunguza maumivu yatokanayo na kung’atwa na wadudu kama nyoka na nge.



Matumizi mengineyo
Miti ya Moringa ikipandwa shambani huweza kuwa msaada kwa mimea ipandayo kama vile maharage. Pia Moringa ikipandwa bustanini husaidia kupunguza joto la moja kwa moja kufikia mimea kama vile mboga mboga na kupunguza uwezekano wa mboga kusinyaa au kukauka. Mti wa Moringa unaota katika mazingira yote, kwenye ukame na meneo yenye maji. Angalizo huchukuliwa kuhakikisha kuwa maji hayatuami kwenye mti kwasababu maji huweza kusababisha ugonjwa na kufanya mizizi ioze. Karibu aina zote za udongo zinafaa kwa mti wa Moringa. Mbegu, kipande cha tawi na hata mzizi vinaweza kutumika kuotesha mti wa moringa.


Namna ya kupanda mti wa Moringa

I. Mbegu
Mbegu iliyokomaa ya mti wa Moringa hulowekwa siku moja kabla ya kuoteshwa, kama maji sio tatizo mbegu inaweza kupandwa moja kwa moja kwenye udongo baada ya kuchimba shimo, weka maji na kisha changanya udongo na samadi angalau kilo tano kabla ya kupanda mbegu halafu endelea kumwagilia katika miezi ya mwanzo. Baada ya angalau siku kumi na tano mbegu inatakiwa iwe imeshachipua. Pia unaweza kuotesha mbegu za Moringa katika vifuko kwenye kitalu kisha kuhamishia shambani baada ya kuota.

II. Kipande cha tawi
Vipande vya tawi lililo komaa huweza kutumika katika kupanda mti wa Moringa, hivi hupandwa eidha moja kwa moja shambani au kwenye vifuko katika kitalu. Kama ukipandwa moja kwa moja angalau robo moja ya tawi inatakiwa ipandwe kwenye udongo, usimwagilie maji mengi sana kwani inaweza kusababisha kuoza.

PHILI KUMKUMBUKA KIEMBA

Kocha wa Simba Mzambia, Patrick Phiri, ameibuka na kudai kuwa atamkumbuka kiungo wake Amri Kiemba iwapo atakamilisha dili lake la kutimkia Azam FC ambayo inamuwinda kwa mkopo.


Kiemba anadaiwa kutakiwa na Azam FC kwa mkopo, baada ya kutoelewana na uongozi wa Simba ambao ulikuwa ukimtuhumu mara kwa mara kucheza chini ya kiwango wakati akiitumikia klabu hiyo tofauti na anapokuwa na timu ya taifa, Taifa Stars.

Kutokana na hali hiyo uongozi wa Simba ulimsimamisha pamoja na wachezaji wenzake wawili ambao ni Shabani Kisiga na Haruna Chanongo.

Phiri alizungumza  akiwa uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, tayari kwenda Zambia na kusema iwapo ataondoka, atamkumbuka sana kiungo huyo ambaye alifanya naye kazi akiwa Simba.

Alisema anatamani kuona anaendelea kuwa naye kwenye kikosi chake lakini wenye maamuzi ya mwisho ni viongozi wa timu hiyo.

“Kiemba ni mchezaji mzuri ambaye katika kipindi chote alichokuwa na mimi sikuwahi kugombana naye, hivyo nitammisi sana katika kikosi changu iwapo ataondoka lakini naamini kwa uwezo wake anaweza kufanya vizuri popote atakapokwenda.

“Kuhusiana na kuziba pengo lake nimeshaongea na viongozi, pia katika ripoti yangu hilo nimelizungumzia, ni matumaini yangu kuwa litafanyiwa kazi na tutampata mbadala wake,” alisema Phiri ambaye anatarajia kurejea nchini Novemba 26 mwaka huu kuendelea na majukumu yake ya kukinoa kikosi hicho chenye maskani yake mtaa wa Msimbazi.

MECHI ZA LEO LIGI YA UINGEREZA




Chelsea vs West Bromwich Albion  18:00 jioni

Everton vs West Ham Utd  18:00 jioni

Leicester City vs Sunderland 18:00 jioni

Manchester City vs Swansea City 18:00 jioni

Newcastle United vs Queens Park Ranger 18:00 jioni

Stoke City vs Burnley 18:00 jioni

Arsenal vs Manchester United  20:00 usiku

KUYT AONYESHA UJUZI WAKE KWENYE 'MA KUNG-FU'


Kiungo Dirk Kuyt, ametupia picha kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter akionyesha ujuzi wake wa mchezo wa Kung Fu.

Kuyt raia wa Uholanzi anayekipiga Besiktas ya Uturuki ameonyesha namna alivyo na uwezo wakati akiwa gym.

Tayari kumekuwa na taarifa kiungo huyo wa zamani wa Liverpool ana mpango wa kurejea kwenye Ligi Kuu England.

Inaelezwa, Kuyt mwenye mapafu ya ‘mbwa’ huenda akajiunga na Southampton.

Ijumaa, 21 Novemba 2014

Adebayor adai mamaake ni mchawi

Mchezaji huyu wa kilabu ya Totenham amedai kuwa mamaake amekuwa akitumia uchawi kujaribu kumuharibia kazi yake.
Mshambuliaji wa kilabu ya Totenham nchini Uingereza Emmanuel Adebayor amekosana na mamaake kwa madai kwamba anatumia uchawi kumharibia kazi yake.
Duru zimearifu kuwa mama huyo tayari ameondoka katika nyumba ya familia huku dadaake Adebayor akiambia radio moja ya mjini Accra kwamba Adebayor ndiye aliyemfukuza.
Lakini mchezaji huyo wa zamani wa kilabu ya Arsenal anadai kwamba mamaake aliondoka mwenyewe na kwamba hawana mawasiliano yoyote kati yao kwa kuwa amekuwa akitumia uchawi kutaka kumuharibia kazi yake.
Adebayo aliwahi kuchezea Arsenal
'' Ninawezaje kuzungumza na mama ambaye yeye na dadaangu wamekuwa wakijaribu kuniroga''aliwauliza maripota.
Mchezo wa Adebayor katika kilabu ya Tottenham umeathirika katika kipindi cha miezi kadhaa iliopita huku Tottenham ikidaiwa kujaribu kumuuza kwa mkopo mchezaji huyo katika dirisha la uhamisho mnamo mwezi January kufuatia kushuka kwa mchezo wake.

Wenger:Tulijaribu kumsajili Messi

Arsene Wenger asema alijaribu kumsajili nyota wa Barcelona Lionel Messi
Mkufunzi wa kilabu ya Arsenal Arsene Wenger amethibitisha kuwa kilabu hiyo ilijaribu kumsajili nyota wa kilabu ya barcelona Lionel Messi kama mpango wa kutaka kuwanyakua wachezaji watatu wachanga wa kilabu hiyo.
Messi alikuwa na miaka 15 wakati huo na mwenzake Gerrad Pique pamoja na aliyekuwa kiungo wa kati wa Arsenal Cess fabregas.
Wenger:''Tulitaka kumchukua Fabregas,Messi na Pique,lakini tukafanikiwa kumpata Fabregas pekee''.
Fabregas aliichezea kilabu ya Arsenal kwa miaka minane kabla ya kurudi Barcelona ,huku Pique akijiunga na Manchester United mwaka 2004.
Wachezaji Cess fabregas na Lionel Mesi wakiwa katika kilabu ya Barcelona.
Messi mwenye umri wa miaka 27,ameichezea timu ya Barcelona kwa muda wote na kuisadia kushinda mataji sita ya La liga pamoja na kombe la vilabu bingwa mara tatu baada ya mpango wa kujiunga na Arsenal kugonga mwamba.
Hatahivyo ,Wenger amepinga madai kwamba mpango huo ulifeli kutokana na makaazi ya Messi na familia yake.
Mchezaji huyo wa timu ya Argentina pia angelazimika kuwa na kibali cha kufanya kazi nchini Uingereza.
Wenger aliongezea:''Nadhani Messi mwenyewe hakutaka kujiunga nasi''.

Zambia:Kaimu rais atimuliwa chamani

Scott alichukua usukani baada ya aliyekuwa Rais Michael Sata kufariki
Chama tawala nchini Zambia (PF) kimemtimua kaimu rais wa nchi hiyo Guys Scott kutoka chamani na kuvunja utaratibu wa katiba.
Taarifa hii ni kwa mujibu wa msemaji wa chama hicho.
''Amekuwa akiwaajiri na kuwafuta watu kazi ovyo na pia bila ya kushauriana na kamati kuu ya chama,'' amesema Malozo Sichone.
Bwana Scott, ambaye licha ya hatua hiyo ataendelea kuwa mwanachama wa chama hicho, ataendelea kuhudumu kama kaimu rais hadi uchaguzi utakapofanyika tarehe 20 Januari.
Scott aliteuliwa kuwa kaimu rais kufuatia kifo cha hayati Rais Michael Sata aliyefariki mwezi jana.

WABUNGE WARUKA UKUTA KUINGIA BUNGENI


PIC.24.-FRACAS-AT-THE-NATIONAL-ASSEMBLY-IN-ABUJA11-600x324 
Ukweli ni kwamba kuna story ambayo unaweza ukasimuliwa na rafiki yako ama mtu yoyote halafu ukaona kama ni uzushi na hakuna ukweli wowote.
Pata picha pale ambapo Spika wa Bunge pamoja na Wabunge wanafungiwa geti la kuingia ndani ya Ukumbi Bunge ….!!
Nakupa story kutoka Nigeria, Spika wa Bunge la Nchi hiyo Aminu Tambuwal amelazimika kuingia ndani ya Bunge kupitia mlango mdogo wa dharura baada ya Polisi kufunga milango ya Bunge hilo kwa sababu za kiusalama.
PIC.25.-FRACAS-AT-THE-NATIONAL-ASSEMBLY-IN-ABUJA1-600x390
Spika huyo alijitambulisha kwa Maafisa Usalama hao ili wamruhusu aingie lakini hakuna aliyeonekana kujali ombi lake wala kumjibu, japo baadaye walimruhusu aingie kupitia mlango mdogo wa dharura huku wabunge wengine wakizuiwa kuingia kitendo kilichowafanya waamue maamuzi magumu ya kuingia ndani ya Bunge kwa kuruka ukuta.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nigeria, Suleiman Abba amesema walilazimika kuzuia mtu yeyote kuingia ndani ya jengo hilo na kuweka ulinzi wa hali ya juu baada ya kupata taarifa kwamba kuna majambazi walipanga kuvamia Bunge hilo.
Polisi waliwashambulia kwa gesi ya machozi Wabunge waliokaidi amri ya kutokuingia Bungeni, Wabunge wawili walipoteza fahamu katika vurugu hizo
 
 
Blogger Templates