Social Icons

Jumapili, 24 Agosti 2014

Jackie Chan awajibika kama mzazi baada ya mwanae kukamatwa na dawa za kulevya

Muigizaji maarufu wa filamu za mapigano, Jackie Chan ameeleza jinsi alivyosikitishwa na tukio la mwanae wa kiume kukamatwa na dawa za kulevya.Jackie Chan ametoa tamko lenye maneno mazito ya busara na kueleza kuwa mwanae huyo amemuaibisha sana lakini pia amemuumiza zaidi mama yake mzazi.Akiwa kama mzazi, Jackie Chan ameeleza kuwa yeye pia anapaswa kuwajibika kwa kushindwa kumpa malezi bora mwanae hivyo akachukua nafasi hiyo kwa niaba yake kuomba radhi kwa kilichotokea huku akimtaka mwanae Jaycee kufahamu kuwa amefanya kosa na anapaswa kuwajibika.

Hiki ndicho alichokieleza:
“Niliposikia habari, nilikasirishwa sana. Kama mtu mashuhuri katika jamii, najisikia aibu; kama baba yake, nimesikitishwa sana na ameniangusha. Lakini mtu aliyevunjwa moyo zaidi ni mama yake. Ninatumaini kizazi kinachofuata kitajifunza kutoka kwa kosa la Jaycee. Umefanya kitu ambacho ni kosa na unapaswa kuwajibika na madhara yake. Mimi ni baba yako na siku zote nitakuwa na wewe. Tutaface yaliyombele yetu pamoja.Napaswa pia kuchukua sehemu ya wajibu kama baba, sikukufumfundisha vyema.”
“Kwa hiyo, kwa niaba ya Jaycee na mimi, ninamuomba radhi kila mmoja kwa madhara hasi yote yaliyosababishwa. Asanteni.”
Jaycee, ni muigizaji pia na ameshafanya filamu kadhaa. Baba yake aliwahi kusikika akimwambia kuwa anapaswa kutengeneza pesa yake mwenyewe kupitia filamu zake na sio kumtegemea.

Mchezaji afariki baada ya kupigwa



Mchezaji mmoja wa soka raia wa Cameroon amefariki baada ya kupigwa na kitu katika kichwa chake kilichorushwa kutoka kwa mashabiki mwishoni mwa mechi katika ligi ya Algeria.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 24 Albert Ebosse aliyekuwa akiichezea kilabu kubwa ya JS Kabylie alikuwa ameifungia timu yake bao la pekee katika mechi ambayo timu hiyo ilishindwa kwa mabao mawili kwa moja na kilabu ya USM Alger.
Kitu kilichomgonga kichwani kilirushwa baada ya mechi kukamilika,wakati ambapo wachezaji walikuwa wanarudi katika chumba cha kujianda.
Waziri wa maswala ya ndani nchini Algeria ameagiza kuanzishwa uchunguzi kuhusu mauaji hayo.

MH;WAZIRI AAMUA KUVUA SUTI NA KUSAIDIA MAJERUHI,ATOA HUDUMA YA KWANZA

Mh.Mwigulu Nchemba akizungumza na Kondakta wa Gali lililopata ajali mara baada ya Kumnasua kwenye roli hilo.Kijana anaonekana kuuguria maumivu makali kwenye Mkono.Mh.Mwigulu Nchemba akiangalia sehemu aliyokuwa amebanwa Kondakta wakati Roli hilo likianguka na baadae kuinuka kutokana na kugonga Ukuta pembezoni mwa Barabara ya Iringa-Morogoro.Mh:Mwigulu Nchemba akitoka huduma ya Kwanza kwa Majeruhi wa ajali hiyo.Huyu ni Dreva akijaribu kuwasha Gari hilo.Mh:Mwigulu Nchemba akiendelea kutoa huduma ya kwanza kwa Majeruhi kabla  ya kumkimbiza kwenda hospitali ya WIlaya ya Mikumi.

MAGWIJI WA REAL MADRID WAZINDUA DUKA JIPYA LA VIFAA VYA UMEME LA TROPICAL LILILOPO VICTORIA KINONDONI DAR

1 (13)
Muonekano wa Jengo la Makao Makuu ya Kampuni ya Tropical.
2 (12)
Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuf Mwenda (kulia), akisalimiana na mwanasoka bora  mstaafu wa timu ya Real Madrid, Fernando Sons (kushoto), baada ya kufika na wenzake kuzindua duka jipya la vifaa vya umeme la Tropical lililopo maeneo ya Victoria Kinondoni Dar es Salaam jana. Katikati ni Christian Karembeu.
3 (11)
Wakurugenzi wa Kampuni ya Tropical wakiwa na wacheza hao wakati wa sherehe hizo. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji, Aloyce Ngowi na Kulia ni Meneja Mkuu, Charles Mlawa.
4 (9)
Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuf Mwenda (kushoto), akiwa na wageni waalikwa. Wa pili kushoto ni Balozi wa Zambia nchini.
5 (6)
Warembo watoa huduma katika duka hilo wakiwa katika picha ya pamoja.
6 (1)
Wapiga picha kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakipiga picha na wachezaji hao.
7

Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuf Mwenda (kulia), akigongesha glasi na wachezaji wastaafu wa timu ya Real Madrid, wakati wa hafla ya uzinduzi wa duka  jipya la vifaa vya umeme la Tropical lililopo maeneo ya Victoria Kinondoni Dar es Salaam.

Jumatatu, 18 Agosti 2014

TRAFIKI AGONGWA NA GARI ENEO LA BAMAGA!!


Askari mmoja wa kikosi cha usalama barabara ambaye jina lake halikuweza kufahamika mara moja, amenusurika kufa baada ya kupata ajali akiwa
anaendesha pikipiki ya polisi,ambayo ilikosa mwelekeo na kugongana uso kwa uso na gari dogo lenye namba za usajili T 681 CUX eneo la Bamaga Mikocheni jijini Dar es salaam.

JAJI LEWSI MAKAME WA TUME YA UCHAGUZI AMEFARIKI DUNIA


Jaji Lewis Makame amefariki muda mchache uliopita katika Hospitali ya Trauma Centre Masaki, aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi,

MeTL GROUP YAPATA MKOPO WA BILIONI 300/- KUTOKA RMB

speech
Afisa Mtendaji Mkuu wa MeTL GROUP, Mohammed Dewji (MB) akisoma risala yake kwenye hafla ya utiliaji saini wa mkopo wa Bilioni 300 za kitanzania kutoka Benki ya Rand Merchant ya Afrika Kusini (RMB) iliyofanyika kwenye hoteli yaSaxon jijini Johannesburg Afrika Kusini.

Na Mwandishi wetu.
Kampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL) imetiliana saini mkataba na benki ya Rand Merchant (RMB) ya Afrika Kusini utakaoiwezesha kupata mkopo wa zaidi ya sh bilioni 300.
Mkataba huo umetiwa saini nchini Afrika Kusini na Ofisa Mtendaji Mkuu MeTL GROUP, Mohammed Dewji.
Akizungumza kabla ya kutiwa saini kwa mkataba huo,Dewji alisema kwamba mkataba huo wa kihistoria unatokana na RMB kuiamini kampuni yake ya MeTL tangu walipoanza mahusiano ya kibiashara mwaka 2007.
“MeTL na RMB tulianza mahusiano yetu mwaka 2007, wakati RMB ilipotukopesha dola za Marekani milioni 7.5million. Wakati huo MeTLilikuwa na bidhaa mbili tu,ngano na sukari! Toka wakati huo, MeTL imekuwa ikikua na kuongeza bidhaa zaidi.” Alisema Dewji na kuongeza kuwa mwaka jana 2013, uwezo wa MeTL wa kukopa sasa umefikia dola milioni 100.
signing deal
Ofisa Mtendaji Mkuu wa MeTL GROUP, Mohammed Dewji (Mb) (wa pili kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa Rand Merchant Bank (RMB), Bw. Bruce Macfarlane (wa pili kulia) wakitiliana saini ya mkopo huo wa bilioni 300 za kitanzania. Kushoto ni Makamu wa Rais wa MeTL GROUP, Vipul Kakad na kulia ni Gregory Havermahl wa RMB wakishuhudia tukio hilo la utiliaji saini wa mkopo baina ya RMB na MeTL Group.
Dewji ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Singida Mjini amesema kampuni yake imekuwa na mafanikio makubwa kibiashara mpaka kuaminiwa na benki mbalimbali za ndani na nje ya nchi.
Pamoja na mkopo huo kwa MeTL hivi karibuni kupitia kampuni yake dada ya kuingiza, kuhifadhi na kusambaza mafuta nchini ya Star Oils Ltd, ilipata mkopo wa sh. bilioni 100 kutoka kwa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC).
“Mwaka 1999 wakati najiunga katika kampuni hii ya kifamilia biashara yetu ilikuwa ni ya dola za marekani milioni 26 na sasa tumejiongeza mara zaidi ya 60 kwani sasa pato letu litafikia dola za Marekani bilioni 1.5 ifikapo mwishoni mwa mwaka”, alisema Dewji.
Alisema mafanikio yalkiyopatikana ya kulipa mikopo husika yamewezesha yeye kusaini mkataba wa mkopo wa dola za Marekani milioni 200 ikiwa ni mwaka mmoja tu tangu wafikie uwezo wa kukopa dola milioni 100 za Marekani.
“Ninataka kusema kwamba maendeleo makubwa ya MeTL yasingelifikia hapa bila RMB kutuamini katika hatua za awali” alisema ofisa mtendaji huyo ambaye pia alielezea kazi mbalimbali zinazofanywa na MeTL.
Alisema kampuni yake inafanya shughuli anuai kwenye sekta mbalimbali, ikiwemo kilimo na viwanda, lojistiki, huduma za fedha,majumba ya biashara, petroli,vinu vya kusindika nafaka,vifaa vya plastiki, usambazaji na masuala ya simu.
Toast
Afisa Mtendaji Mkuu wa MeTL GROUP, Mohammed Dewji (Mb) na Mkurugenzi Mtendaji wa Rand Merchant Bank (RMB), Bw. Bruce Macfarlane wakinywa shampeni baada ya kufanya "Toast" kama ishara ya kutakiana kheri na mafanikio kwenye biashara zao.
Akisaini mkopo huo, Dewji aliwashukuru wote waliohudhuria hafla hiyo ya kusaini kati ya kampuni yake MeTL na RMB huku ikijivunia kufanya biashara katika nchi za Ethiopia, Malawi, Msumbiji, Zambia, Dubai, Uganda, Rwanda, Burundi, Congo, Sudan Kusini na Kenya.
Alisema kwamba kampuni hiyo inataka kujiimarisha zaidi katika sekta mbalimbali.MeTL kwa sasa ina viwanda zaidi ya 31 nchini Tanzania pekee; huku ikiwa imetawanyika katika nchi 11 zilizopo Kusini mwa jangwa la Sahara.
"Tumejitanua katika nchi mbalimbali barani Afrika, nashukuru kwa ushirikiano mzuri ambao umechangia mafanikio makubwa ya kampuni yetu", alisema Dewji.
Dewji maarufu kwa jina "MO" anasema elimu aliyoipata katika Chuo Kikuu cha Georgetown nchini Marekani ndio iliyomfumbua macho na kuona umuhimu wa kutumia fursa za ushindani wa kibiashara duniani.
“Nia yetu ni kuwa na nguvu kubwa ya kibiashara Afrika Mashariki na Kati tukipania MeTL kuwa na pato la zaidi ya dola za Marekani bilioni 5 kwa mwaka ifikapo mwaka 2018 na kutengeneza ajira za watu 100,000.” Alisema Dewji
Alisema katika hotuba yake hiyo kuwa siri ya mafanikio ya kampuni ya MeTL ya kukua kwa zaidi ya mara 60 katika kipindi cha miaka 15 tangu alipojiunga nayo kuwa ni kutumia vyema fursa zilizopo na pia hamu yangu ya kuwatumikia na kuboresha maisha ya watanzania.
“Falsafa yangu kama mfanyabiashara sio kuridhika na mafanikio niliyonayo bali kuendelea kufanyakazi kwa bidii na kufanikiwa zaidi.” Alisema.
Chat
Afisa Mtendaji Mkuu wa MeTL GROUP, Mohammed Dewji (Mb) (katikati) akibadilishana mawazo na Mkurugenzi Mtendaji wa Rand Merchant Bank (RMB), Bw. Bruce Macfarlane (kulia). mara baada ya kutiliana saini mkopo wa Bilioni 300 za Kitanzania.

Jumamosi, 16 Agosti 2014

JAJI WEREMA APINGANA NA IKULU ,ASEMA BILA UKAWA HAKUNA KATIBA


IMG_0173Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jaji Frederick Werema akitoa ufafanuzi wa masuala Kisheria kwa waandishi wa habari kuhusu mchakato wa upatikanaji wa katiba mpya wakati wa mkutano uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
IMG_0197Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jaji Frederick Werema akiwaonesha waandishi wa habari Rasimu ya katiba wakati akitoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali ya kisheria katika mchakato wa Katiba wakati wa mkutano uliofanyika leo jijini Dar es Salaam 
IMG_0199
IMG_0206
Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jaji Frederick Werema wakati wa mkutano uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.

Viongozi wa vyama vya siasa waliopo nje ya Bunge Maalumu la Katiba wameaswa kurejea bungeni ili kufanya maridhiano ndani ya bunge hilo.
Kauli hiyo imetolewa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema alipokuwa akiongea na waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam.
Jaji Werema amesema kuwa wajumbe walio nje ya Bunge Maalum hawana budi kurejea bungeni na kuacha kumshinikiza Rais kulivunja bunge hilo kwani hana mamlaka ya kulivunja kulingana na sheria inayoliongoza bunge hilo.
“Sheria inasema kuwa baada ya bunge hilo linaweza kuvujwa baada ya katiba kupatikana, kinyume na hapo bunge husitishwa kufikia maridhiano na kufikia mwafaka kwa kufuata misingi ya demokrasia.” alisema Jaji Werema.
Pia Jaji Werema alisema kuwa wajumbe walio nje ya bunge hilo hawana budi kurudi ili kuendelea kujadili vipengele vingine vya rasimu ili kuweza kupata katiba iliyo bora kwa nchi na watu wake.
Aidha, Jaji Werema aliviasa vyombo habari kutumia nafasi yao ya kuwa mhimili muhimu katika uongozaji wa nchi kutokuwa na upendeleo katika utoaji wa taarifa na kuacha kuongozwa na mawazo ya wachache ili kuweza kusaidia nchi kupata Katiba Mpya kwa manufaa na maendeleo ya nchi.

Moto wateketeza kituo cha kupozea umeme cha mjini Moshi Leo asubuhi

Askari wa kikosi cha Zimamoto wakifika eneo la tukio asubuhi hii

Wananchi wakishuhudia juhudi za kuzima moto huo



Moto ukiendelea 
Juhudi zikiendelea. Picha na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini. 
Transforma zinazosambaza umeme katika maeneo mbalimbali ya mji wa Moshi Mkoani Kilimanjaro zilizoko eneo la Bomambuzi zimewaka moto asubuhi hii muda mfupi baada ya kutokea shoti ambayo haijafahamika chanzo chake ni nini. 
 Moto huo umetokea majira ya saa 1:10 na kusababisha maeneo kadhaa ya mji wa Moshi kukosa umeme hadi sasa. 
 Globu ya jamii imeshuhudia kikosi cha zimamoto kutoka manispaa ya moshi kikijaribu kuzima moto huo ambao hata hivyo ulikwisha teketeza sehemu kubwa ya  kituo hicho cha kupozea umeme
 
 
Blogger Templates