Social Icons

Jumamosi, 28 Desemba 2013

ANGALIA PICHA YA MTOTO WA MCHEZAJI MPIRA MKUBWA DUNIANI AMBAYE NI ADIMU KUONEKANA KATIKA VYOMBO VYA HABARI.

ron2

article-0-1A1FF1B500000578-234_634x409
article-2526363-1A20036000000578-481_634x999

Huyo ndio mtoto wa Cristiano(Cristiano Jr)akiwa na familia yao katika uzinduzi wa jumba la makumbusho nchini kwao Ureno, sehemu iitwayo Madeira,nyumba hilo ni kwa jili kubwa ya Ronaldo na historia yake katika mpira.

Ni adimu sana mtoto huyo kuonekana katika Media na baba yake huwa hapendelei kabisa mwanae mwanae kuonekana katika vyombo hivyo.

Ijumaa, 27 Desemba 2013

SOMA HIII...MSICHANA ALIYEKAMATWA NA MADAWA YA KULEVYA NCHINI CHINA WAUMIZA VICHWA VYA WENGI NCHINI TANZANIA

 
 Msichana wa Tanzania aliyekamatwa na madawa ya kulevya akiwa amesimama karibu na meza yalipowekwa madawa yaliyotolewa kutoka kwenye mwili wake
 
Ni msichana gani wa Tanzania aliyekamatwa na madawa ya kulevya nchini China? Hilo ni swali gumu ambalo kila mmoja amekuwa akijiuliza bila kupata jibu la uhakika. Mtandao wa chinadaily.com.cn umeandika habari na kuweka picha za kukamatwa kwa msichana huyo mwenye umbo refu, mwenye nywele ndefu na mweupe. Mtandao huo umeandika: Msichana mwenye miaka 28 kutoka Tanzania alikamatwa kwa tuhuma za kumiliki madawa ya kulevya huko -Macao, Dec 19, 2013. Alikuwa ameficha kilo 1.1 za heroin zenye thamani ya $137,720 ( sawa na zaidi ya shilingi milioni 85) ndani ya mwili wake na kuchukua ndege kutoka Thailand hadi Macao. Alisema alikuwa akielekea Guangzhou, mji mkuu wa jimbo la Kusini mwa China Guangdong.

Madawa yaliyotolewa kwenye mwili wa msichana huyo mwenye miaka 28 yakioneshwa mbele ya waandishi wa habari
 
 
Msichana wa Tanzania aliyekamatwa na madawa ya kulevya na aliyefunikwa uso wake akiwa chini ya ulinzi
Tunafahamu kuna majina tayari yanayotajwa kuwa huenda wakawa ndio msichana huyo lakini hatuwezi kuyataja wala kuthibitisha kwa sasa ili kuepuka kuripoti habari zisizo na ukweli. www.onaviews.blogspot.com

SOMA HIII.......TAULO ZA IVO MAPUNDA MARUFUKU GOLINI


Tabia ya kipa wa Simba, Ivo Mapunda kutundika taulo katika nyavu za golini sasa inaelekea kufikia ukomo kwa kuwa licha ya waamuzi kadhaa kumkataza kufanya hivyo wakati wa mechi, mwamuzi mwingine wa kimataifa ameliambia gazeti hili kuwa ni marufuku kutundika taulo golini.


Ivo amekuwa na kawaida ya kutundika taulo kwenye nyavu kisha kuendelea na mchezo, lakini kwenye Michuano ya Kombe la Chalenji, mwamuzi mmoja aliitoa na kumtaka kuiweka chini na iwe nje ya goli, pia katika mechi ya Simba dhidi ya Yanga, mwamuzi wa kati, Ramadhani Ibada wa Zanzibar alimkataza kuining’iniza kwenye nyavu wakati mechi ikiendelea.

Mwamuzi Oden Mbaga amesema ni kosa kutundika taulo kwenye nyavu kwa kuwa inaweza kuwachanganya wachezaji wakati wa mchezo.

“Kimsingi hairuhusiwi kabisa kuingia na taulo labda aliweke kwa nje lakini siyo ndani ya lile goli tena siyo taulo tu bali na vitu vingine vyovyote,” alisema Mbaga.

Wakati Ivo akiambiwa hivyo, makipa kadhaa wa Ulaya wamekuwa na kawaida ya kutundika taulo kwenye nyavu na hawazuiliwi na waamuzi.

Wakati huohuo, Ivo amesema ana mpango wa kuchapisha taulo zitakazo kuwa na nembo yake ili aweze kujiongezea kipato. "Fursa hiyo nimeona siku nyingi. Nitakutana na kampuni mbalimbali kuona uwezekano huo," anasema Mapunda.

 Alisema hivi sasa taulo anazotumia kujifuta jasho pindi anapokuwa uwanjani zina nembo mbalimbali lakini atakoma kuzitumia pindi zenye nembo yake zitakapoanza kutoka.

RAGE ANENA.............Yanga haitufungi hadi tuhujumiane.


Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage

Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage ametoa kali baada ya kuifananisha timu ya Yanga na kikosi cha vijana wa Simba wenye umri chini ya miaka 20 (Simba B).

Akizungumza katika kipindi cha 'Hot Mix' kilichorushwa na EATV juzi jioni, Rage alisema kikosi cha Yanga kwa sasa ni sawa na Simba B, hivyo hakina uwezo wa kuifunga Simba.

"Yanga ni Simba B, itawachukua muda mregu sana kuja kutufunga. Wamejaza wachezaji wengi waliotoka kwetu (Simba) ambao lazima walipe fadhila kutokana na mazuri ambayo Simba iliwafanyia," alisema Rage.

"Kwa sasa Simba inaweza kufungwa na Yanga pale tu mmoja ama baadhi wa viongozi wetu wataamua kuihujumu timu yetu. Hawana uwezo wa kutufunga pasipo sisi (Simba) wenyewe kuhujumiana," alisema zaidi Rage.

Aidha, Rage alitumia muda huo kujibu hoja 'maiti' za 'waasi' wa Simba waliokuwa wakidai kwamba hajahusika hata kidogo katika kufanikisha ushindi wa timu yao dhidi ya Yanga Jumamosi.

"Kuna vitu visivyo na maana vinazungumzwa juu yangu. Naambiwa sijashiriki katika kufanikisha ushindi dhidi ya Yanga. Mchezaji aliyefunga bao la tatu (kiungo Awadh Juma) nilimsajili nyumbani kwangu na ndiye aliyechangia pia bao la kwanza," alisema.

Mbunge huyo wa Tabora Mjini (CCM) alibainisha kuwa watu wanaompinga wanasumbuliwa na ukata wa fedha, hivyo wanatafuta namna ya kumng'oa madarakani ili wahujumu mali za klabu hiyo.

"Wanasumbuliwa na njaa, ni njaa tu inawasumbua hao. Zipo njia sahihi za kikatiba za kuutoa madarakani uongozi. Wasubiri uchaguzi mkuu wa Simba," alisema kiongozi huyo anayesifika kwa lugha ya vijembe.

Siwataji walioficha mabilioni Uswisi ng’o, Zitto


Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe amevunja ukimya na kusema hayuko tayari kwa sasa kuwataja Watanzania wenye mabilioni huko Uswisi na kuitaka Serikali ifanye uchunguzi.
Zitto ndiye aliyeibua hoja bungeni kuwa kuna Watanzania walioficha Sh315 bilioni katika taasisi za fedha nchini Uswisi.
Katika taarifa yake aliyoitoa jana, Zitto alisema anasita kutaja majina hayo sasa ili kuepusha kile alichosema majina hayo kutumiwa vibaya bila kujali kama Watanzania walizipata fedha hizo kihalali au la na kuzihifadhi nje ya nchi.
Alisema ameshauri mchunguzi wa kimataifa anafaa kufanya kazi hiyo.
Mbunge huyo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), amesema wastani wa Sh729.3 bilioni hutoroshwa kila mwaka kwenda nje ya nchi.
Alisema kauli ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Fredrick Werema kwamba yeye (Zitto) hakutoa ushirikiano wa kamati inayochunguza sakata hilo si ya kweli.
“Nataka niwahakikishie, nimekutana mara nne na kamati hii. Nimewapa mpaka jina la mchunguzi wa kimataifa atakayeweza kuwasaidia katika uchunguzi huu, leo naambiwa sitoi ushirikiano,” alisema Zitto.
Alisema mchunguzi huyo wa kimataifa ana uzoefu katika uchunguzi wa suala kama hilo na angeweza kuwatambua kwa majina na kiasi cha fedha na pia uhalali na uharamu wa fedha hizo.
Alisema ameshangazwa na hatua ya Serikali kumbeza pale alipopendekeza suala la kutafutwa mchunguzi wa kimataifa lakini siku chache baadaye ikatangaza magazetini nafasi ya kazi hiyo.
Tangazo hilo lilichapwa Desemba 17, mwaka huu siku ambayo Zitto alisema kwamba angesoma maelezo binafsi kujibu kauli ya Jaji Werema. Hata hivyo, alisema alikosa nafasi. Zitto amesema hashurutishwi na azimio la Bunge kutaja majina hayo kwa sababu yeye siyo chombo cha uchunguzi ambacho kinapaswa kuwa na mkono mrefu.
Alisema wakati akikabidhi majina ya Watanzania hao, angependa ushahidi huo uwe umefanyiwa uhakiki na vyanzo vyake vya kimataifa na vyombo vya usalama vya Serikali nchini.
“Siko tayari kutaja kwa sasa. Narudia tena kwa sasa hayo majina maana naweza kusababisha wahukumiwe na umma bila kupitia utaratibu uliowekwa na sheria zetu hapa nchini,” alisema Zitto.
Alisema inawezekana pengine shinikizo hili linatoka kwa watuhumiwa wenyewe baada ya kuona watu wengine waliokumbwa na kashfa nyingine walitajwa majina na hakuna hatua zilizochukuliwa.
“Mimi kama kiongozi makini na kama wasiwasi huu nilionao utakuwa wa kweli basi siko tayari kurudia makosa yaleyale ya kutaja majina halafu ikaishia hapo bila wahusika kushughulikiwa,” alisema.
Alisema suala la utoroshaji wa fedha nje ya nchi ni kubwa kuliko Watanzania wa kawaida wanavyolifahamu na kusema hilo ni janga la kitaifa na kimataifa na si la Zitto pekee.
Akitoa mfano, Zitto alisema uchunguzi unaonyesha mwaka 2010 pekee, kiasi cha Sh2.1 trilioni kilitoroshwa hapahapa nchini na mwaka 2011 kiasi cha Sh1.3 trilioni kilitoroshwa kwenda nje.
Alisema taarifa za mashirika ya kimataifa zinaonyesha kuwa katika kipindi cha miaka 10 iliyopita, kiasi cha fedha kilichotoroshwa hapa nchini na kupelekwa nje ya nchi ni Sh7.3 trilioni.
Zitto alisema hali hiyo si nzuri hata kidogo kwani inatokea wakati kuna Watanzania wanaoishi katika lindi kubwa la umaskini na kutahadharisha kuwa ipo siku kundi hilo linaweza kuchukua hatua.
“Nawaomba wenzangu waifanye vita hii kama ya Watanzania wote, wafahamu wale wenye masilahi na fedha hizi hawataacha kufanya kila njia kubeza vita hiyo. Mimi ni mpuliza filimbi tu katika vita hii na Watanzania wajue sina uwezo wa kuishinda vita hii peke yangu bila kuungwa mkono na wabunge, wananchi na hata Serikali.”

Watatu mbaroni kwa tuhuma za kumteka, kumtesa Absalom Kibanda


Absalom Kibanda, Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF)

Watu watatu wametiwa mbaroni kwa tuhuma za kumteka, kumtesa na kumjeruhi Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Absalom Kibanda.
Katika tukio hilo, Kibanda aling'olewa meno pamoja na kutobolewa jicho na watu wasiojulikana.

Akizungumza na NIPASHE kwa njia ya simu jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini (DCI), Kamishna wa Polisi, Isaya Mngulu, alisema kuwa watu watatu wanashikiliwa mpaka sasa na wanahusishwa na tukio hilo.

Mngulu alisema kinachoendelea kwa sasa ni kwa Jeshi hilo kujiridhisha ikiwa ni pamoja na kukusanya ushahidi wa kutosha kuhusu watuhumiwa hao kuhusika kwenye tukio hilo ili wafikishwe mahakamani.


“Jeshi limefanikiwa kuwakamata watu watatu kwa tuhuma za kuhusika na tukio hilo, lakini kwa sasa upelelezi unaendelea kwani bado tunakusanya ushahidi wa kutosha ili tujiridhishe kwa watuhumiwa hao kuhusika na tukio hilo kabla hatujawafikisha mahakamani,” alisema Mngulu.

Kauli ya DCI inakuja baada ya kuwapo kwa kauli tofauti na tata zilizowahi kutolewa na jeshi hilo na serikali tangu kutokea kwa tukio hilo juu ya matukio ya Kibanda na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania, Dk. Steven Ulimboka.

Moja ya kauli iliyowahi kutolewa na Jeshi la Polisi ni ile ya kivihusisha vyombo vya habari kuwa vilichangia upelelezi wa matukio hayo kuzorota kutokana na kuandika sana ikiwamo wanaohusika na upelelezi (vyombo vya usalama) kushutumiwa.

Novemba, mwaka huu, aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, ambaye uteuzi wake ulitenguliwa na Rais hivi karibuni, Dk. Emmanuel Nchimbi na Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Suleiman Kova, walilazimika kulizungumzia suala hilo baada ya waandishi wa habari kutaka ufafanuzi kutoka kwao.

Waandishi walihoji iweje upelelezi wa tukio la kuvamiwa, kujeruhiwa na kuporwa kwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, marehemu Dk. Sengondo Mvungi, ukamilike na watuhumiwa kukamatwa haraka huku matukio hayo mawili yakiwa kimya.

Wakati Dk. Nchimbi na Kova wakisema hayo, Oktoba 14, mwaka huu, Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai, (DCI) mstaafu Robert Manumba, aliliambia NIPASHE kuwa uchunguzi wa uhalifu nchini wa kuteka, kutesa na kujeruhi raia pamoja na matukio mengine ya kumwagiwa tindikali upo njia panda kutokana na kukosekana kwa vifaa vya kisasa kuwabaini wahusika.

Manumba alisema katika kupeleleza matukio hayo, polisi wanakabiliana na changamoto za kubaini wahusika kutokana na kutumia teknolojia duni pamoja na kukosa wataalam.

Alishauri kila taasisi ikiwamo misikiti, makanisa na sehemu nyingine zenye mikusanyiko ya watu wengi, kufunga kamera (CCTV) ili kusaidia kubaini namna uhalifu unavyotokea. Hata hivyo, ushauri wa Manumba wa kufunga kamera kwenye nyumba za ibada, hauwezi kubaini uhalifu ambao umeshatendwa siku zilizopita.

KAULI YA KOVA
Akijibu hoja hiyo, Kamanda Kova alisema kila tukio lina mazingira yake na hakuna linalofanana na lingine kwa asilimia 100, hivyo matukio hayo (ya Kibanda na Dk. Ulimboka) na la Dk. Mvungi, hayafanani kimazingira na kinyakati.

“Safari hii (katika tukio la marehemu Dk. Mvungi), media (vyombo vya habari) vimekuwa kimya hata tulivyowaomba wasiandike walikubaliana nasi, ndiyo maana upelelezi ukawa rahisi…matukio ya Kibanda na Ulimboka, yaliandikwa sana na wanaopeleleza walituhumiwa,” alisema.

Aidha, aliviomba vyombo vya habari kunyamaza kunapokuwa na tukio linalohitaji upelelezi ili kutoa nafasi kwa Idara ya Upelelezi kufanya kazi vizuri.

“Tukio la Dk. Mvungi liwe fundisho jema kwa vyombo vya habari kuwa kunapotokea tukio watuachie Polisi na vyombo vingine vya usalama tupeleleze ndipo tuwape taarifa,” alisisitiza Kova.

Hata hivyo, alipobanwa aeleze upelelezi umefikia wapi na iwapo kuna wanaoshikiliwa, Kova alisema: “Tusiyazungumzie ya Kibanda na Ulimboka jibu tulilotoa awali linatosha.”

KAULI YA NCHIMBI
Dk. Nchimbi aliwahi kusema kuwa upelelezi wa matukio hayo (la Kibanda na la Dk. Ulimboka), unaendelea na hata kama utachukua muda mrefu kiasi gani ni lazima waliohusika wakamatwe.

“Ninaandaa semina kwa waandishi wa habari niwaonyeshe mikanda ya matukio ya uhalifu nchi mbalimbali duniani na jinsi upelelezi ulivyofanyika …tunaweza kutumia miaka mitatu hadi minne na tukawakamata watuhumiwa,” alisema.

Dk. Nchimbi alisema kabla ya Desemba 31, mwaka huu, itaundwa Kurugenzi ya Intelijensia na itakuwa na Kamishna ikiwa ni pamoja na kuwa na mafunzo ili kuharakisha upelelezi.

Mara kadhaa, Jeshi la Polisi limekwepa kuzungumzia tukio la kutekwa, kupigwa na kuteswa kwa Kibanda huku kukiwa na kurushiana ‘mpira’ kati ya Kova, Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini, Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), na Mkuu wa Jeshi hilo, Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Said Mwema.

Kibanda ambaye pia ni Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya New Habari (2006) Limited ambayo ni wachapishaji wa magazeti ya Rai, Dimba, Mtanzania, Bingwa na The African, alivamiwa na watu hao, wakati akirejea nyumbani kwake, Mbezi Juu, jijini Dar es Salaam Machi 5, mwaka huu.

Katika tukio hilo, watu hao walimng’oa meno, kumkata kidole, kumjeruhi kwa kitu kizito kichwani na kumharibu jicho la kushoto.

Mara baada ya tukio hilo, Msemaji wa Jeshi la Polisi, Advera Senso, alimkariri IGP Mwema, akisema kuwa ameunda timu ya wapelelezi wazoefu kufanya uchunguzi ili kuwabaini waliohusika katika uhalifu huo na kuwatia mbaroni. Timu hiyo ya makachero wanne kutoka makao makuu ya polisi iliunganisha nguvu na makachero wa Jeshi hilo Kanda Maalum ya Dar es Salaam, ambayo hadi sasa haijatoa matokea ya uchunguzi huo, licha ya kuwapo kwa ahadi za kufanya hivyo mara kadhaa.
Jukwaa la Wahariri Tanzania kwa kushirikiana na Baraza la Habari Tanzania (MCT), waliunda timu kuchunguza tukio hilo na kutoa taarifa iliyohusisha tukio hilo na sababu mbalimbali ikiwamo kazi yake ya uandishi wa habari.

Dk. Ulimboka alikutwa na tukio hilo Juni 27, mwaka 2012 na baada ya muda mfupi polisi walimkamata raia wa Kenya, Joshua Gitu Mulundi (31), kwa madai ya kuhusika na tukio hilo na kufikishwa mahakamani.

Baada ya kitambo, Mwendesha Mashitaka wa Serikali aliamua kufuta kesi dhidi yake na aliachiwa huru kabla ya kukamatwa tena na polisi na kushtakiwa kwa kosa la kuwadanganya Polisi na kuhukumiwa kulipa faini ya Sh. 1,000 au kifungo cha miezi sita. Alilipa faini hiyo.

Aidha, Jeshi la Polisi mpaka sasa bado halijafanikiwa kuwatia mbaroni watuhumiwa wa matukio mawili ya mabomu yaliyotokea jijini Arusha na kusababisha vifo vya watu kadhaa.

Matukio hayo ni yale ya bomu lililotokea kwenye mkutano wa kufunga kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani wa kata tano wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Juni 14, mwaka huu na kuua watu wawili. Lingine ni lililotokea katika Kanisa Katoliki Parokia ya Olasiti Mei 5, mwaka huu na kusababisha vifo vya watu wanne pamoja na kujeruhi watu kadhaa.

Matukio ambayo hata hivyo, Mngulu aliiambia NIPASHE wiki iliyopita kuwa Jeshi lake bado linaendelea na upelelezi na kwamba mpaka sasa limefanikiwa kumtia nguvuni mtu mmoja kwa tuhuma za kuhusika kwenye tukio la Olasiti na kesi yake iko mahakamani.

Alhamisi, 26 Desemba 2013

MKOANI MOROGORO GARI LILILOKUWA LIMEBEBA MAITI LAKAMATWA LIKIWA NA DAWA ZA KULEVYA

 

Kamanda wa Polisi Mkoani Morogoro,Faustine Shilogile akizungumza na wanahabari (hawapo pichani).
Hizi ndio baadhi ya Pipi zilitolewa tumboni mwa Marehemu Khalid Kitala.
Baadhi ya Makachero wa Polisi wakijadiliana jambo baada ya kuona Mwili huo.
Jeshi la Polisi mkoani Morogoro limefanikiwa kukamata gari dogo aina ya Toyota Spacio likiwa limebeba mwili wa mtu aliefari ambaye alitambulikwa kwa Jila la Khalid Kitala (47) na kukutwa na kete kadhaa za Madawa ya Kulevywa tumboni.

Kamanda wa polisi mkoani Morogoro, Faustine Shilogile amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa walipata taarifa za kuwepo kwa gari  hilo toka kwa wasamalia wema ambao waliliona njiani, ambapo inasemekana lilikuwa linatokea Mkoani Mbeya kuelekea Dar.

Polisi wa mkoa wa Morogoro waliweka mtego wao kwenye kituo cha Mikumi na hatimaye kufanikiwa kukamata gari hilo likiwa na watu watatu ndani (majina yao yamehifadhiwa),pipi saba za vitu vinavyosadikiwa kuwa ni dawa za kulevya.

Mwili huo ulipelekwa hospitali na kufanyiwa uchunguzi na kukutwa na pipi nyingine kumi na saba tumboni mwa Marehmu huyo na inasemekana mtu huyo alifariki akiwa Mbeya.

Watu wote watatu ambapo wawili wanahusika na gari hilo na mmoja ni mfanyabiashara wa Kariakoo wanashikiliwa na polisi huko Morogoro.

WEMA,DIAMOND SIELEWI????? KATIKA SHOW YA ...........25 PATA HABARI NA PICHA.

sdd    

Hii ilikuwa jana pale Leaders club kwenye show ya Diamond ambapo Wema Sepetu alipanda kwenye stage na kuongea na mashabiki waliofika kwenye show hiyo.
Kwenye hiyo show Diamond aliuliza,”Mnataka kumjua mchumba wangu”?
 
Show ilivyoendelea Diamond alitaka kuimba wimbo wa ukimwona akasema, “Naskia ninayetaka kumuimbia wimbo huu yupo humuhumu ndani”.
Wema Sepetu akapanda kwenye stage wakaimba na kucheza wote.

379719_654725334570888_100223854_n
 

MCHEZAJI WA CHELSEA SAMUEL ETOO NA MKEWE WAKIFANYA YAO X-MASS...!


 

Jumatano, 25 Desemba 2013

BAADA YA RUBEN,FALCAO NAYE ATETA YAKE: RONALDO NI MCHEZAJI BORA ZAIDI YA LIONEL MESSI

Mshambuliaji wa Monaco  Radamel Falcao anaamini kwamba mshambuliaji wa Real Madrid  Cristiano Ronaldo ni mchezaji mzuri kuliko staa wa klabu ya Barcelona Lionel Messi.

Mchezaji huyo wa Colombia anawakubali wachezaji wote wawili, ingawa Falcao anaamini Cristiano ni bora zaidi ya Messi.

"Messi na Cristiano ni wachezaji muhimu na wakubwa duniani leo hii lakini, kwangu mimi naamini Ronaldo ni bora zaidi," alisema mchezaji huyo mwenye miaka 27 alipoongea na El Tiempo.

Falcao pia amesema ni Cristiano Ronaldo anayestahili kuwa mchezaji bora wa dunia katika tuzo za Ballon D'or zitakazotolewa mwezi ujao ambapo Ronaldo anapambana na Ribery pamoja na Messi.
 
 
Blogger Templates