Social Icons

Jumatano, 25 Septemba 2013

Wakaguzi wa UN wa silaha za kemikali warejea Syria

Raia wa Syria wakiwa katika maandamanao.
Raia wa Syria wakiwa katika maandamanao.
 
Wakaguzi wa silaha za kemikali wa Umoja wa Mataifa wamerejea Syria kufanya uchunguzi wa matumizi ya silaha hizo zilizopigwa marufuku nchini humo wakati wa miaka miwili na nusu ya vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Kundi linaloongozwa na Ake Sellstorm lilikwenda nchi jirani ya Lebanon jumatano na kusafiri kwa kutumia gari hadi Damascus.

Kwanza walikwenda Syria mwezi uliopita kufanya uchunguzi wa mashambulizi matatu ikiwemo lile la mwezi Machi nje ya mji wa Aleppo ambalo serikali ya Syria na wapiganaji waasi wanashutumiana.

Kundi hilo lilihamisha mwelekeo wake wa ujumbe wa wiki mbili na kuzingatia shambulizi jipya nje ya Damascus ambako waligundua kwamba silaha za kemikali zilitumika.

Wakati huohuo Jumatano kundi la waasi 13 lilitoa taarifa ya pamoja kupinga baraza la upinzani la taifa la Syria likisema kuwa haliwakilishi tena ushawishi wao.

Watu wengi waliokimbia nchi hiyo wamekwenda nchi jirani ikiwemo Jordan, Lebanon, Uturuki na Iraq.

Tetemeko la ardhi lawaua 270 Pakistan


Zaidi ya watu 300 wamejeruhiwa
Tetemeko kubwa la ardhi limewauwa watu 270 katika mkoa wa Kusini Magharibi wa Balochistan nchini Pakistan.
Tetemeko hilo la kipimo cha 7.7-lilipiga Jumaanne alasiri . Nyumba nyingi zilibomolewa na watu wengi walipaswa kulala nje.
Watu walikusanyika ufukweni kushuhudia kisiwa hicho kipya ambacho kinakadiriwa kua na urefu wa mita 200 na upana wa mita 100 na kiinuka mita 20 kutoka upeo wa bahari .
Balochistan ndio mkoa mkubwa wa Pakistan lakini ukiwa na watu wakaazi wachache kupita yote
Eneo hilo hukumbwa na mitetemeko ya mara kwa mara na mnamo mwezi wa Aprili watu 35 waliuwawa katika tetemeko ambalo kitovu chake kilikua Kusini Mashariki mwa Iran mnamo mwezi wa April.

Vibanda vya udongoTetemeko hilo lilikua la nguvu hata watu wa miji iliyo mbali ya Karachi, Hyderabad, na mji mkuu wa India, Delhi walihisi mtikisiko wake.Vijiji vizima inaarifiwa vilifyekwa katika wilaya ya wakaazi masikini ya AwaranMsemaji wa serikali ya Balochistan, Jan Buledi, 

Amesema waliopatwa na maafa zaidi ni katika mji wa Awaran na vijiji vinavyouzingira na ameonya idadi ya vifo huenda ikaongezeka. Takriban watu 340 wamejeruhiwa.Msemaji huyo amesema kuna ukosefu mkubwa wa huduma za matibabu na hospitali hazina nafasi za kutosha kuwatibu majeruhi .Alisema helikopta zinawasafirisha majeruhi mahututi hadi mjini Karachi na wengine wanahudumiwa katika wilaya jirani.

Jeshi la Pakistan lilikua miongoni mwa makundi ya kwanza kutoa msaada kwa kua tayari limekua huko miaka kadhaa sasa kwa sababu ya uasi wa watu wanaotaka kujitenga kwa mkoa huo wa Balochistan.Jeshi limesema limetuma zaidi ya wanajeshi 200 , wana matibabu na mahema kutoka mji mkuu wa mkoa huo Quetta, lakini shughuli za uokozi zinatatizwa kwa hali ya milima ya eneo hilo.

MWANAMKE ALIYEFANANISHWA NA KINARA WA MAUAJI YA WESTGATE AJITOKEZA NA KUKANUSHA HABARI HIYO

Kufuatia mashambulizi ya kigaidi katika mall ya West Gate jijini Nairobi, kumekuwepo na uvumi kuhusu mwanamke wa Uingereza aitwaye Samantha Lewthwaite au ‘White Widow’ kuhusika na tukio hilo. Jana kulikuwa kumekuwa na picha zilizosambaa katika mitandao ya kijamii pamoja na kuripotiwa na baadhi ya vyombo mbalimbali vya habari ikiwemo mtandao wa Mail Online wa Uingereza, za mwanamke ambaye baadhi ya watu waliamini kuwa ni Samantha Lewthwaite au ‘White Widow’.

Habari iliyokuwa inasambaa ni kuwa mwanamke huyo aliyedhaniwa kuwa ‘white widow’ alitoroka kwa njia ya kujifanya kumsaidia mwanamke huyo (kwenye picha hapo juu).

NTV ya Kenya iliamua kusahihisha habari hiyo kwa kumtafuta mwanamke huyo (kushoto katika picha) na walifanikiwa kumpata na kuweka taarifa hiyo sawa kwa kukanusha kutokuwa mtu ambaye watu walimdhania.

Akiongea na NTV Mwanamke huyo alijitambulisha kwa jina la Henna, na wakati wa tukio alikuwa katika mall ya West gate na wanae wawili pamoja na dereva wakifanya manunuzi ndipo ghafla mashambulizi yakaanza. Wakati wa kujiokoa aliamua kuwa msamaria mwema kwa kumsaidia mwathirika mwenzie aliyejeruhiwa kama ilivyoonekana katika picha iliyozuwa uvumi wa kuwa ‘white widow’

Jumatatu, 23 Septemba 2013

BASI LA AL SAEDY LAPATA AJALI MBAYA LAGONGANA USO KWA USO NA LORI CHALINZE DODOMA

Lori la mizigo lililogongana uso kwa uso na basi la Al - Saedy lililokuwa likitoka Dar Es salaam kuelekea Mkoani Dodoma jana usiku linavyofanana baada ya kugongana na basi hilo uso kwa uso
Basi la Al Saedy linavyoonekana mara baada ya kugongana na lori la Mizigo Maeneo ya Chalinze Mkoani Dodoma Jana Usiku mpaka naondoka eneo la tukio idadi kamili ya waliopoteza maisha na kujeruhiwa bado haijafahamika
Basi la Al Saedy linavyoonekana mara baada ya kugongana na lori la Mizigo Uso Kwa Uso jana usiku eneo la Chalinze Mkoani Dodoma idadi ya Waliopoteza maisha wala Kujeruhiwa bado haijajulikana

Jana Majira ya Saa Nne usiku Basi la Al Saedy linalofanya safari zake kati ya Dar Es Salaam na Dodoma lilipata ajali mbaya kwa kugongana uso kwa uso na lori la mizigo maeneo ya Chalinze Mkoani Dodoma , Ajali hiyo ilihusisha Basi hilo la Al Saedy na lori la mizigo lililokuwa likitokTunaondoka eneo la tukio idadi kamili ya waliopoteza maisha wala kujeruhiwa bado haijafahamika.

AJALI MBAYA IRINGA LEO ABIRIA ZAIDI YA 50 WA SAI -BABA EXPRESS WANUSURIKA KIFO
Askari wa usalama barabarani Iringa wakilitazama basi la kampuni ya Sai - baba Express lenye namba za Usajili T 668 BCD ambalo liligongana uso kwa uso na lori la kampuni ya Ivori lenye namba T 280 ADK eneo la Kibwabwa katika barabara kuu ya Mbeya - Iringa mchana wa leo na watu zaidi ya watatu kujeruhiwa vibaya na wengine zaidi ya 50 ambao ni abiria wa basi hilo kunusurika kifo
Lori la kampuni ya Ivory lenye namba za usajili T 280 ADK lililogongana na basi hilo
Mmiliki wa Lori la Ivory akiwa kama amechanganyikiwa kwa kupiga picha kila kona la basi hilo huku abiria wakishangaa

WAKATI Taifa likiwa katika maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama barabarani ajali mbaya imetokea katika eneo la Kibwabwa barabara kuu ya Iringa - Mbeya baada ya basi la Sai- Baba Express kugongana uso kwa uso na lori la kampuni ya Ivori mchana wa leo.

Basi hilo la kampuni ya Sai - baba Express lenye namba za Usajili T 668 BCD ambalo liligongana uso kwa uso na lori la kampuni ya Ivori lenye namba T 280 ADK ndilo ambalo linatajwa kuwa chanzo cha ajali hiyo.

Mashuhuda wa ajali hiyo wameueleza mtandao huu wa www.matukiodaima.com kuwa ajali hiyo imetokea majira ya saa 8 mchana wakati basi hilo likitokea mkoani Mbeya na Lori hilo likitokea mjini Iringa na hivyo kugongana uso kwa uso .

Mmoja kati ya abiria wa basi hilo Yusuph Juma alisema kuwa dereva wa basi hilo alikuwa katika mwendo kasi mbali ya eneo hilo la mji kuwepo alama zinazokataza spindi zaidi ya 50 ila bado basi hilo lilikuwa katika mwendo zaidi .

Alisema kuwa mbali ya magari hayo kugongana uso kwa uso ila bado basi hilo liliweza kushindwa kusimama na kulazimika kusimama zaidi ya mita 200 kutoka eneo la ajali .

Hata hivyo alisema ni jambo la kushuruku Mungu katika ajali hiyo mbali ya dereva wa lori kujeruhiwa vibaya wengine waliojeruhiwa ni pamoja na utingo wa basi na abiria mmoja huku abiria wengine zaidi ya 50 wakinusurika katika ajali hiyo.

Viongozi mbali mbali wa jeshi la polisi ,Sumatra na mwenyekiti wa kamati ya usalama barabarani mkoa wa Iringa Bw Salim Asas ni miongoni mwa mashuhuda waliofika kushuhudia tukio hilo ambalo limetokea huku taifa likiwa katika wiki ya nenda kwa usalama taifa yatakayodfanyika kitaifa jijini Mwanza kuanza wiki ijayo chini ya udhamini wa kampuni ya simu ya Airtel Tanzania .

ALSHABAAB WAONGEA : SOMA WALICHOKISEMA HAPA NA SABABU ZA KUISHAMBULIA KENYA.


Mwandishi Jamal Osman amefanya mahojiano exclusive na msemaji wa kundi la kigaidi la Al-Shabaab kuhusiana na sababu za kuishambulia mall ya Westgate.


Hii ni tafsiri ya Kiswahili ya mahojiano hayo yaliyofanywa kwa Kiingereza kwenye mtandao wa Channel4

Jamal Osman: Kwanini mmefanya shambulio?


Msemaji wa Al-Shabaab: Sababu ya kufanya shambulio ni kuwalinda watu wetu na nchi yetu sababu Kenya ilitushambulia, bado wanaendelea kushikilia sehemu ya ardhi yetu. Tumekuwa majirani wenye amani, lakini wao ndio walitushambulia na tunajilinda.

Haijalishi kama wewe ni Muislamu ama Mkristo, sheria inasema unatakiwa kujilinda mwenyewe dhidi ya yule aliyekushambulia.


JO: Mmeua watu wa mataifa mengi wakiwemo Waingereza, hamuogopi mataifa makubwa yatawatafuta?


Msemaji wa Al-Shabaab: Tumewaambia Wakenya na wale wanaoenda Kenya kwamba hatuwezi kuvumilia kile Kenya inatufanyia. Tuliwaambia tutajilinda wenyewe na tuliwaonya kuhusu kwenda Kenya.

Wakenya wana damu yetu mikononi mwao. Mtu yeyote aliyejiandaa kwenda Kenya lazima ajiandae na kukabiliana na ukweli huo, na hatuwaogopi watu wa Ulaya ama Wamarekani sababu sisi si wadhaifu.
Na tunasema hili kwa watu wa Ulaya na Wamarekani ambao wamekuwa wakiwasaidia wale wanaotushambulia, muwaambie Wakenya waache uonevu wao kama mnataka kuwa salama.


JO: Kwanini mliilenga mall ya Westgate?


Msemaji wa Al-Shabaab: Sababu ya kwanini tuliilenga mall ya Westgate, ni kwakuwa Wakenya na serikali yao wametumia majeshi dhidi yetu, ni maadui wetu. Wamewatuma watu wao Somalia, wameiunga mkono serikali yao kuishambulia nchi yetu. Kwetu, popote pale Kenya ni sawa, tutawapiga popote tuwezapo.
Sababu tulilenga Westgate ni kwamba tunajua ni sehemu ambayo wanajisikia maumivu zaidi. Ni kwasababu inaingiza hela nyingi na ipo katikati ya jiji.

Ni sehemu wanasikia maumivu na kwasababu tulitaka kutuma ujumbe na hatukutaka kuupoteza ujumbe wetu. Tulitaka ujumbe wetu umfikia kile Mkenya.


JO: Wapiganaji wenu ndani ya mall bado wanapigana?

Msemaji:
Ni zaidi ya saa 27 sasa, wapo ndani na bado wameshika hatamu.


JO: Nasikia kuna mpiganaji mwanamke ndani pia?


Msemaji: Hatupeleki wanawake wetu kwenye uwanja wa vita.


JO: Kitu gani mnategemea kitatokea sasa? Nini litakuwa tokeo la hili?


Msemaji: Kama Mungu akipenda, tunategemea Wakenya watapata ujumbe kwamba kama ukimwaga damu, damu yako itamwagika pia. Kwao kujua kuwa hawawezi kushikilia Kismayu, Dhobley na Afmadow na wategemee waishi kwa amani Nairobi. Huo ni ujumbe tunataka kuutuma kwao.


JO. Kwenye jumbe zenu kupitia Twitter mnasema huu ni mwanzo tu na mtaendelea, ama mmeshafikia malengo yenu?


Msemaji: Tunasema kwa Kenya, iacheni nchi yetu. Huo ni ujumbe wa kwanza. Na kama wakikataa kuiacha nchi yetu basi tutaanzisha vita yenyewe.


JO: Hivyo matakwa yenu kwa Wakenya, ni kuiacha nchi yenu kama wanataka amani?

Msemaji:
Kama Wakenya wanataka amani, wanatakiwa kuiacha nchi yetu.


JO: Kwanini mnawalenga watu wasio na hatia?


Msemaji: Raia wa kigeni, wanatakiwa kuondoka kwenye nchi hiyo (Kenya) kwasababu Wakenya na Al-Shabaab wapo kwenye mgogoro na tunamwambia kila mtu – Kenya ni eneo la vita.


JO: Kwakuwa unasema raia wa kigeni na Waingereza wana maslahi makubwa nchini Kenya, mna ujumbe gani kwao?

Msemaji: Tunasema kwa Waingereza, kwakuwa tunaamini wanawasaidia Wakenyan na Wakenya ni watumwa wao, wao (Waingereza) wanatakiwa kuwaambia Wakenya, walitoe jeshi lao Somalia.

Na Waingereza wanajua Wasomali hawataka tamaa. Tuliwakatalia Waingereza mwanzoni, ambao wana nguvu kuliko Wakenya

JOHNSON JABIR MWANDISHI HABARI AVAMIA, APIGWA NA MAPANGA, AJERUHIWA



Majeraha aliyoyapata kichwani
Johnson Jabir
ARUSHA: (JAIZMELALEO) - Maisha ni safari ndefu wadau wa JAIZMELALEO.
Siku zote mshukuru Mungu kwa kila jambo linapotokea katika maisha yako wala usiwe na hofu kabisa hata kama linauma kama nini LEAVE TO GOD.
Usiku wa kuamkia Septemba 22, 2013 katika mtaa wa Elkurei katika Kata ya Kiranyi, Arumeru mkoani Arusha wezi walinivamia na kunijeruhi haswa.
Walibeba vifaa vya kazi lakini kubwa zaidi ilikuwa ni kunitoa roho lakini Mwenyezi Mungu alininusuru kwa kunitia nguvu kupambana nao walikunja na marungu, visu na mapanga.
JINA LA BWANA LIBARIKIWE KWA YOTE.
Source:JAIZMELALEO)

Jumapili, 22 Septemba 2013

PLEASE PRAY FOR KENYA

PLEASE PRAY FOR KENYA,
WATU 43 WAMEPOTEZA MAISHA NA ZAIDI YA WATU 143 WAMEJERUHIWA VIBAYA,MPAKA SASA WAVAMIZI BADO HAWAJA KAMATWA ILA JUHUDI ZA DHATI ZINAENDELEA NA TAYARI JESHI LA KENYA LIME FANIKIWA KUFIKA OROFA YA PILI.
BUsY0QGCEAAY4Ci1 389x258 Latest on Westgate shoot out
A plain clothes police officer escorts rescued captives away from the Westgate mall
BUtYvx8CQAAe7yD 389x259 Latest on Westgate shoot out
A mother and her children hide from gunmen at Westgate Shopping Centre in Nairobi.

Jumamosi, 21 Septemba 2013

PATA PICHA NA HABARI ZA TUKIO LA UVAMIZI WA JENGO LA KIBIASHARA WESTGATE MALL NAIROBI,KENYA.MPAKA SASA NATOA HABARI HII BADO WAVAMIAJI HAO HAWAJATOKA KATIKA JENGO HILO NA WALA HAWAJAKAMATWA.
Hali ni tete katika jiji la Nairobi ambapo washambuliaji wenye silaha wamevamia eneo la kifahari la Westgate Mall nje kidogo ya jiji la Nairobi.
Vyombo vya habari vya Kenya vinaripoti kuwa washambuliaji hao waliokuwa wamegubika nyuso zao walivamia maduka hayo mwendo wa saa sita mchana kwa saa za Kenya na kuwateka nyara watu kadha.
Wafanyakazi wengi wamenaswa katika mtafaruku huo huku ikiripotiwa kuwa zaidi ya watu 30 wameuawa na zaidi ya watu 60 wamejeruhiwa vibaya.Polisi wa Kenya wamewaambia wananchi wasiende eneo hilo ambapo kikosi maalum cha jeshi la G.S.U.maarufu kama 'fanya fujo uone' kimepelekewa eneo hilo kuwasaka na kukabiliana na washambuliaji hao.
Hili ndilo jengo lililovamiwa.

An injured man is treated outside an upmarket shopping mall, seen background, in Nairobi, Kenya, 21 September 2013.Emergency medical staff treated some of the wounded near the building's entranceA soldier moves to take up a position outside an upscale shopping mall, seen background, in Nairobi, Kenya Saturday 21 September 2013.Security forces have surrounded the shopping centreShoppers are helped to evacuate the area of an upmarket shopping mall, seen background, in Nairobi, Kenya Saturday 21 September 2013.Dozens of shoppers were given assistance in evacuating the areaTwo women hug outside an upscale shopping mall, seen background left , in Nairobi, Kenya Saturday 21 September 2013.Children and families were taken to safety after the shootings began

YOUNG SCIENTISTS AWARD TANZANIA 2013
Heriel akihakikisha kila kitu kianenda sawa kwa upande wa live ya sauti/audio ambayo ilikuwa ina rushwa  TBC 1 TV,sound/music ndani ya ukumbi iposawa na watu wa vision wikipata sauti sahii ya kuweza kurusha na kuweka katika youtube(young scientists award 2013)fungua usikie

 
 
Blogger Templates