Social Icons

Jumatano, 11 Novemba 2015

Rais wa Myanmar ampongeza Suu Kyi

Image copyrightAFP
Image captionBi Aung San Suu Kyi
Rais wa Myanmar Thein Sein amekipongeza chama cha upinzani cha Aung San Suu Kyi kwa kushinda uchaguzi mkuu, msemaji wake ameiambia BBC.
Huku ikiwa asilimia 47 ya viti vimetangazwa, Chama cha Nationa League for Demokrasi kimechukua asilimia 90 ya kura.
Bi Suu Kyi ameuandiakia uongozi akitaka mazungumzo ya uwiano wa kitaifa.
Lakini msemaji U Ye Htut amesema mkutano kama huo unaweza kufanyika tu baada ya matokeo rasmi kutangazwa.
Amesisitiza kuwa hakuna jaribio lolote la kucheleweshwa kutangazwa kwa matokeo hayo ya uchaguzi wa siku ya jumapili.
Image captionRais wa Myanmar Thein Sein
Waandishi wanasema bi Suu Kyi anafuatilia mambo kwa tahadhari licha ya ushindi wake mkubwa.
Chama cha NLD kilishinda uchaguzi wa mwaka 1990,kabla ya matokeo hayo kufutiliwa mbali huku bi Suu Kyi akiwekwa katika kifungo cha nyumbani cha mda mrefu.
Chama tawala cha kijeshi Union Solidarity Development Party {USDP} kilichoshinda uchaguzi uliopita ambao ulikosolewa miaka mitano iliopita kufikia sasa kina asilimia 5 ya viti vionavyogombewa nchini humo .
Robo ya viti vya ubunge huwekewa wanajeshi.

Marekani yakerwa na ziara ya Assad Moscow


Assad na Putin


Marekani imeshutumu Urusi kwa kumpa mapokezi ya taadhima Rais wa Syria Bashar al-Assad mjini Moscow.

"Tunatazama mapokezi ya zulia jekundu aliyopewa Assad, aliyetumia silaha za kemikali dhidi ya watu wake, kuwa kinyume na lengo lililoelezwa wazi na Urusi la kutaka kuwepo na shughuli wa mpito kisiasa Syria,” msemaji wa ikulu ya White House Eric Schultz amewaambia wanahabari.

Afisa wa wizara ya masuala ya ndani ya Marekani alisema taifa hilo halijashangazwa na ziara hiyo, lakini wasiwasi mkubwa kwa Marekani ni Urusi kuendelea kumsaidia kivita Assad.

Alisema hilo litaipa nguvu zaidi serikali ya Assad na hivyo kuendeleza mapigano ya wenyewe kwa wenyewe nchini humo.

Ziara hiyo ya kiongozi huyo wa Syria Jumanne ilifanyika wiki tatu baada ya Urusi kuanza kushambulia kwa ndege ngome za wapiganaji wa Islamic State na makundi mengine yanayopinga utawala wa Assad.

Ilikuwa ziara ya kwanza kabisa kwa Assad nje ya nchi baada ya mapigano kuzuka Syria 2011. Mapigano hayo ya wenyewe kwa wenyewe yameua watu 250,000.

Akiwa jijini Moscow, Assad alitoa shukrani zake kwa Urusi kuingilia kati kijeshi nchini mwake.

Alisema operesheni hiyo ya Urusi ilikuwa imezuia ugadi kueneza zaidi na kuwa madhara makubwa Syria.

Kwa upande wake, Bw Putin alisema matumaini ya Moscow ni kwamba suluhu ya muda mrefu itapatikana kupitia mchakato wa kisiasa na kwa kushirikisha makundi yote ya kisiasa, kikabila na kidini.

Mwandishi wa BBC aliyeko Moscow Steve Rosenberg anasema kuwa kwa kumkaribisha kiongozi huyo wa Syria mjini Moscow, Putin alikuwa akituma ujumbe mkali kwa mataifa ya Magharibi kwamba Moscow ni mhusika mkuu katika mzozo huo Mashariki ya Kati na kwamba suluhu haiwezi kupatikana bila kuhusisha Urusi.

Marekani yaadhimisha siku ya mashujaa.


Rais Barack Obama akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku ya mashujaa, Nov. 11, 2015,huko Arlington,Virginia.

Migahawa na biashara nyingine hapa Marekani Jumatano zinatoa punguzo la bei kwa bidhaa na huduma ikiwa ni siku ya mashujaa .
Hali hiyo ya shukran maalum inaendelea wakati wa maadhimisho ya kila wakati na kukiwa na yale ya huzuni  ikiwa ni pamoja na kuwekwa kwa shada la maua katika kaburi la wale wanajeshi ambao hawakuweza kutambulika na Rais Barack Obama alifanya hivyo katika eneo la  makaburi ya mashujaa huko Arlington Virginia, karibu kabisa na makao makuu ya nchi ya Marekani.
Siku hii ambayo ni maalum kabisa kutoa heshima kwa wale wote waliotumikia taifa katika jeshi la Marekani ilianza tangu 1919 wakati rais Woodrow Wilson alipotangaza Novemba 11 kama siku ya kusitisha mapigano kwa muda  kusheherekea  kumalizika mapigano ikiwa ni mwaka mmoja katika vita vya kwanza vya dunia “vita kumaliza vita vyote” kati ya Ujerumani na mataifa yalioungana ya Uingereza , Ufaransa na Marekani.
 Sitisho la mapigano  lilikamilika rasmi mwishoni mwa siku ya 11 katika mwezi wa kumi na moja.

EU kutoa mabilioni kwa Afrika kupunguza wahamiaji

Wahamiaji

Image copyrightReuters
Image captionWahamiaji wengi wamekuwa wakifa maji wakijaribu kufika Ulaya
Viongozi wa Muungano wa Ulaya wanatarajiwa kutoa mabilioni ya euro kwa mataifa ya Afrika kuyawezesha kusaidia kupunguza mzozo wa wahamiaji Ulaya.
Tume ya Muungano wa Ulaya imesema itatoa €1.8bn (£1.3bn) na inatarajia mataifa zaidi ya EU yaahidi pesa zaidi.
Lengo la ufadhili huo ni kusaidia kusuluhisha matatizo ya kiuchumi na kiusalama ambayo huwafanya watu kutoroka mataifa ya Afrika. Aidha, zitatumiwa kuyashawishi mataifa ya Afrika kuwapokea watu ambao wamenyimwa hifadhi Ulaya.
Ahadi hiyo inatarajiwa kutolewa kwenye mkutano mkuu kuhusu wahamiaji unaofanyika Malta, na ambao ulipangwa baada ya meli iliyobeba wahamiaji kuzama Libya mwezi Aprili. Watu 800 walifariki
Watu 150,000 wamevuka bahari ya Mediterranean kutoka Afrika mwaka huu, wengi wakitua Italia na Malta.
Hata hivyo, mtazamo wa EU umebadilika tangu Aprili na kuangazia zaidi wakimbizi wanaotoka mashariki na hasa Syria, ambao wanawasili kwanza Ugiriki na kuvuka hadi Uturuki kisha kuelekea kaskazini kupitia bataifa ya Balkan.
Zaidi ya viongozi 60 kutoka Afrika na Ulaya, akiwemo Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron, wanakutana Valletta, Malta kwa mkutano huo mkuu wa siku mbili kujadili uhamiaji.
Tume ya Muungano wa Ulaya itaweka pesa hizo €1.8bn kwenye "hazina maalum" kwa ajili ya Afrika na imehimiza mataifa wanachama kufikisha kiasi hicho cha pesa.
Hata hivyo, kuna shaka kuhusu iwapo mataifa hayo yatakubali wito huo.

Jumatatu, 9 Novemba 2015

MOURINHO ALIKUWEPO UWANJANI KWA SAUTI,FA UENDA IKA MFUNGIA.

soka nchini England FA, huenda kikamfungulia mashtaka ya kinidhamu meneja wa klabu ya Chelsea, Jose Mourinho baada ya kubainika kulikua na mawasialiano kati yake na meneja msaidizi, Steve Holland sambamba na Rui Faria.
Mourinho alifanya hivyo, kutokana na adhabu ya kufungiwa kuingia uwanjani katika mchezo dhidi ya Stoke City, kufuatia utovu wa nidhamu ambao aliuonyesha mara baada ya mchezo wa ligi dhidi ya Southampton kwa kumsemea mbovu muamuzi mbele ya waandishi wa habari.
Uchunguzi wa awali umebaini kuwepo kwa kifaa cha mawasilino kwenye benchi la ufundi la Chelsea na mara kadhaa meneja msaidizi Steve Holland alionekana akizungumza na kwa kijificha.

Hata hivyo uchunguzi bado unaendelea kufanya na ikibainika kuliwepo na mchezo huo ambao haukutakiwa kuwepo, Mourinho ataadhibiwa zaidi kutokana na kanuni za kinidhamu ambazo zipo chini ya chama cha soka nchini England FA.
Jambo lingine ambalo huenda likaiingiaa klabu ya Chelsea kwenye hatari ya kuadhibiwa na FA, ni hatua ya mameja wasaidizi kushindwa kufika kwenye mkutano wa waandishi wa habari.
Katika mchezo huo Chelsea walikubali kufungwa bao moja kwa sifuri.

Kagame awashutumu viongozi wa Burundi


Kagame

Image copyrightReuters
Image caption


Kagame amesema mauaji yanayoendelea Burundi yanaweza kumfanya mtu yeyote mpenda haki kuingilia kati
Rais wa Rwanda Paul Kagame ameshutumu vikali viongozi wa Burundi kutokana na mauaji yanayoendelea nchini humo nakuonya kuwa huenda kukatokea mauaji ya halaiki
Bw Kagame ameshangaa ni vipi viongozi wa taifa hilo jirani "wanaweza kuruhusu wananchi wao kuuwawa kiholela".
Rais Kagame alisema hayo Ijumaa, lakini matamshi yake hayakutangazwa hadi mwishoni mwa wiki, akionekana sana kumlenga Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza.
Akizungumza kwa Kinyarwanda Rais Kagame alisema: ''Tazama nchi jirani kama Burundi, maisha yao yamesimama kabisa. Lakini sababu ni ipi? Wana historia inayofanana na yetu.
Ila viongozi wao wapo kwa ajili ya kuua wananchi kuanzia asubuhi hadi jioni."
Nkurunziza
Image copyright
Image caption
Rais Nkurunziza amekuwa haonekani sana hadharani
''Rais akajifungia sehemu isiyojulikana, hakuna anayejua sehemu alikojificha, hakuna anayezungumza naye, huyo anaongoza watu vipi?" alisema Bw Kagame, akihutubu katika hafla ya kuwatunuku Wanyarwanda waliosaidia kuwaficha na kuwaokoa Watutsi wakati wa mauaji ya kimbari 1994 pamoja na wanaharakati wanaotetea umoja na maridhiano miongoni mwa Wanyarwanda.
''Watu wanakufa kila siku, maiti zinabururwa barabarani. La kusikitisha ni kuwa bara la Afrika lina ugonjwa wake lenyewe kiasi kwamba hata nitalaumiwa eti nimekosea kuitaja nchi nyingine, eti ningecheza diplomasia au siasa. Siyo haki mimi nitasema wazi. Viongozi wanashinda wakiua watu, maiti zinatapakaa sehemu zote; wakimbizi wanarandaranda sehemu zote watoto, wanawake ....kisha unasema ni siasa. Hiyo ni siasa gani?"
Uhusiano kati ya Rwanda na Burundi umedorora sana tangu Bw Nkurunziza atangaze kuwa atawania urais kwa muhula wa tatu, hatua iliyopingwa na wapinzani.
Mwezi uliopita, Burundi ilimfurusha mwanabalozi mmoja kutoka Rwandaikimtuhumu kwa kuhujumu usalama wa nchi hiyo.
"Utasema kuwa ni nani aliyesababisha matatizo ya Burundi? hata kukiwa na mtu anayekutakia mabaya atavutiwa na ubaya wako unaotenda...Hata kama ni mtu kutoka Rwanda anayesababisha machafuko nchini Burundi, bila shaka atavutiwa na maovu ya viongozi wa Burundi wanayotendea wananchi wao. Shida ni ya Warundi wenyewe," alisema Bw Kagame.
Image copyright

Maelfu ya raia wamekuwa wakitoroka mitaa ya Bujumbura
"Tatizo ni kwamba hawakupata somo kutoka kwetu (Rwanda), kutokana na yaliyosibu taifa letu wangepata somo hasa kutokana na baadhi ya Warundi wenyewe kuhusika katika yale yaliyolisibu taifa letu.
Afrika sijui tunaugua ugonjwa upi?"
Hayo yamejiri siku moja baaya watu 9 kuawa usiku na watu wenye silaha, ndani ya baa moja katika mji mkuu wa Bujumbura.
Askari wa usalama wanafanya msako katika kila nyumba, kwenye mitaa inayoonekana kuwa ni ngome za upinzani, baada ya muda uliowekwa na serikali kwa watu kusalimisha silaha zao kumalizika.
Watu takriban 20 wameuwawa nchini Burundi katika juma lilopita, huku maelfu ya watu wakitoroka makwao.

UWANJA WA ARSENAL WAHARIBIWA NA MASHABIKI WA SPURS










no comments
Mashabiki wa klabu ya Tottenham Hotspurs, wameonyesha kulipiza kisasi kwa kuvunja vyoo vya uwanja wa Emirates unaomilikiwa na mahasimu wao wakubwa wa jijini London Arsenal.
Hatua hiyo inadhamiwa kufanywa na mashabiki wa Spurs, kufutia kuchukizwa na kitendo kilichoonyeshwa na mashabiki wa Arsenal, wakati wa mchezo wa kombe la ligi (Capital One Cup) mwezi Septemba cha kung’oa baadhi ya mabango yayokua yametundikwa kwenye uwanja wa White Hart Lane.
Mashabiki wa Arsenal walifikia hatua ya kufanya hivyo kwa kudhaniwa huenda furaha ilikua imewajaa, kutokana na kikosi chao kuibuka na ushindi wa mabao matano katika mchezo huo wa mwezi Septemba, japo jeshi la polisi jijini London liliingia kati na kufanya uchunguzi wa kina na kubaini uharibifu uliokua umefanywa uwanjani hapo.
Kwa hatua hiyo mashabiki wanaodhaniwa kuwa ni wa Spurs, wamedhihirisha kulipa kisasi cha kuvunja makaro ya vyoo vya upande wa jukwaa walilokua wamekaa wakati wa mchezo wa jana, ambapo mambo yalimalizika kwa timu zote mbili kugawana point kufuatia sare ya bao moja kwa moja.
Hata hivyo uongozi wa klabu ya Arsenal, haujasema lolote kufuatia uharibufu huo, ziadi ya picha za tukio hilo kuanikwa hadhani katika mitandao ya kihabari pamoja na ile ya kijamii.
Arsenal pamoja na Spurs wamekua na uhasama wa kiushindani mkubwa katika soka, lakini katika miaka ya hivi karibuni, imeonekana mashabiki wa pande hizo mbili wamevuka mipaka na kuanza kuonyesha hali ya uvunjifu wa amani baina yao.
Klabu hizo mbili zote zina maskani huko kaskazini mwa jijini London, na zinapokutana kwenye michuano yoyote nchini England huwa kuna upinzani wa hali ya juu, japo wachezaji wanapomaliza mchezo huonyesha kupatana kwa kusalimiana na kukumbatiana tofauti na kwa baadhi ya mashabiki.

ALAMA ZA KUKUONYESHA KUWA MPENZI WAKO SIO MWAMINIFU (some signs of cheating)




 Mabadiliko katika tendo la ndoa:
Jambo hili laweza kujidhihirisha katika picha mbili tofauti. Kwa kawaida wapenzi huwa na mazoea fulani katika tendo la ndoa, kwa muda waliokaa pamoja kila mmoja humfahamu mwenzake kwa kiasi fulani. Inawezekana likawa jambo la kushangaza pale ambapo gafla unamuona mpenzi wako anapoteza kabisa hamu ya tendo la ndoa, au hata mnapokuwa katika tendo hilo humuoni akifurahia bali anakuwa kama anayelazimishwa au kutohamasishwa na chochote. Kwa upande mwingine unaweza ukakuta mpenzi wako anakuja na ujuzi wa gafla katika mahusiano yenu ya tendo landoa, hali yake ya kukutamani inazidi gafla, anahitaji mapenzi mara kwa mara na hata mnapokuwa katika tendo hilo anadhihirisha utaalamu wa tofauti na ule uliouzoea. Hali hizi mbili zifanyike tahadhari katika kukusaidia kuyatazama mahusiano yenu.

 Marafiki wa mpenzi wako kukukwepa:
Ni hali yakawaida kuwa karibu au kuzoeana na marafiki wa mpenzi wako, maranyingine mtawasiliana nao kutaka kujua aliko mpenzi wako au kinachoendelea kwao. Inabidi ujiulize sana pale inapotokea gafla wale marafiki wa mpenzi wako uliowazoea, uliokuwa unawapigia simu wakati wowote leo wana kukwepa, na hata simu hawapokei na maranyingine wakipokea hawakupi taarifa yakueleweka au wanakudanganya. Hii yote inawezekana wanamlinda rafikiyao, au wanakosa cha kujibu maana wanajua uhalisia wa kinachoendelea.

Kuzungumza sentensi za kutatanisha:
Kama nilivyosema awali, wapenzi wengi hujuana kwa mengi, 
ikiwemo pia namna ya kuzungumza au kuonyesha hisia. Unaweza kukuta katika mapenzi yenu mpenzi wako anaanza kuwa na sentensi ngumu na zisizo kuwa na msingi kwa mfano anasema “kwa jinsi hii sidhani kama tutafika” “mi siamini kama mapenzi yanadumu” “yani ndio maana watu wanashindwa kukaa na mpenzi mmoja” na maranyingine anaweza kukuuliza baadhi ya maswali moja kwa moja ili kukuona utajibuje. Sentensi hizi zina chanzo moyoni, kuwa macho.

 Kuzidi kwa tabia za kutoonekana au kuponyoka:
Yawezekana mpenzi wako alikuwa na tabia ya kuwepo nyumbani mida isiyokuwa ya kazini au wikiendi, muda mwingi alipenda kuwa na wewe na akiaga basi atasema anakwenda wapi na akimaliza hurudi mapema kwa sababu anakiu ya kuwa nawewe, mara gafla sikuhizi haagi anakwenda wapi, ukiuliza inawezakuwa vita. Anakuwa na vijisafari vingi na vijisababu visivyoisha vya kumuwezesha kuponyoka. Sehemu ya kwenda na kurudi lisaa limoja anaweza kuchukua nusu siku, kila ukiuliza atakwambia nakuja, niko njiani, kuna foleni, nimekwama, na sababu nyingine nyingi sana. Ukiona haya yanazidi ujue kuna la zaidi ya foleni, na hizo sababu zote zinazotolewa zinafunika jambo.

Tabia za kuficha fedha:
Ninafahamu fika kwamba suala la uwazi katika mambo yanayohusiana na fedha na matumizi ni tatizo kubwa kwa wapenzi wengi, wengi wamegombana na hata kuachana kuhusiana na jambo hili. Japokuwa hili ni tatizo kwa wengi lakini wako wapenzi ambao wamekuwa na tabia ya kuambiana kwa uwazi matumizi na mapato yao, hakuna kitu wamefanya kuhusu fedha zao pasipo kuambiana na hivi ndivyo mlivyozoeshana, mara ghafla mmoja anaanza kuwa na siri kuhusu fedha zake au matumizi yake, na wala hapendi kuulizwa ulizwa kuhusu suala hilo. Tabia hii ikidhihirika katika mapenzi yenu usichelewe kuchunguza maana kwa kukaa kimya unaweza kujikuta umechelea mwana na maji ya moto.


Jumamosi, 3 Oktoba 2015

AIBU...............Soka ya Tanzania iko chini zaidi Afrika mashariki

Image captionTaifa Stars
Licha ya kupanda nafasi nne hadi nambari 136,Tanzania imeorodheshwa ya chini zaidi na shirikisho la soka duniani FIFA katika soka ya Afrika mashariki.
Kulingana na orodha ya FIFA iliotolewa siku ya Alhamisi,Uganda imeorodheshwa ya 75,ikifuatiwa na Rwanda katika nafasi ya 93.
Uganda na Rwanda zimeshuka nafasi 4 na 15 mtawalia.
Burundi nayo imerodheshwa nambari ya 113 ikiwa ya tatu ikifuatiwa na Kenya katika nafasi ya 131 ikiwa nambari 4.
Image captionTaifa Stars
Taifa Stars ya Tanzania ambayo ililazimu sare ya 0-0 dhidi ya timu ya Super Eagles kutoka Nigeria katika mechi za kufuzu kwa kombe la Afrika inashikila nafasi ya 5 na ya mwisho katika Afrika mashariki ikiwa katika nambari 136 duniani.
Kwengineko orodha hiyo mpya inaonyesha kuwa Liberia na Afrika Kusini ndizo zilizofanywa vyema.
Mataifa hayo mawili yameorodheshwa ya 95 baada ya kupanda kwa nafasi 65 na 144 baada ya kupanda kwa nafasi 54 mtawalia.
Image captionTaifa Stars
Kulingana na Shrikisho la FIFA,Ujerumani inaongoza ikifuatiwa na Argentina kisha Ubelgiji nafasi ya 3 na Ureno katika nafasi ya nne.

Walimu wasitisha mgomo Kenya


Image captionKatibu mkuu wa chama cha walimu nchini KNUT Wilson Sossion
Mgomo wa walimu nchini Kenya hatimaye umesitishwa.
Walimu sasa watarudi shuleni ili kuendelea kufunza siku ya jumatatu.
Katibu mkuu wa KNUT Wilson Sossion amesema kuwa muungano huo hatahivyo hautaondoa kesi ambapo tume ya huduma za walimu TSC imekataa rufaa dhidi ya uamuzi wa mahakama wa kuwapatia walimu hao nyongeza ya mishahara ya kati ya asilimi 50-60
Hatua hiyo ya muungango wa walimu nchini Kenya KNUT inatokana na agizo lililotolewa na Jaji Abuodha mnamo tarehe 25 mwezi Septemba.
Mgomo huo ulikwamisha masomo nchini Kenya huku walimu wakitaka nyongeza ya mishahara pamoja na ile ya marupurupu.
Walimu sasa wanaitaka tume ya kuajiri walimu TSC kuwapatia mishahara ya mwezi Septemba baada ya tume hiyo kusema kuwa haitawalipa kwa kuwa walikuwa katika mgomo.
Hatua hiyo inatoa afueni kwa wanafunzi wa shule za uma ambao walilazimika kukaa nyumbani kwa kipindi chote cha mgomo huo.
Image captionWalimu
Jaji wa mahakama ya wafanyikazi Nelson Abuodha aliwaagiza miungano yote miwili ya walimu kuahirisha mgomo huo ili kutoa fursa ya majadiliano.
''Kwa maslahi ya watoto wetu katika shule za umma na haki zao chini ya katiba mpya,mahakama imeagiza miungano hiyo ya walimu kuahirisha mgomo huo ulioanza terehe mosi mwezi Septemba kwa siku 90,ili wanachama wake waanza kazi mara moja'',alisema jaji Abuodha.
Mda mfupi tu baada ya agizo hilo kutolewaserikali ilitangaza kuwa shule zote zitafunguliwa sikuya jumatatu na kufungwa mnamo tarehe 20 mwezi Novemba
 
 
Blogger Templates