Social Icons

Alhamisi, 4 Desemba 2014

Jumatatu, 1 Desemba 2014

Brahimi nyota wa BBC Afrika 2014

Yacine Brahimi ndiye mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa afrika wa BBC mwaka huu
Mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa Afrika BBC mwaka huu amepatikana. Baada ya maelfu ya kura kuhesabiwa, mchezaji wa Algeria na nyota wa Porto, Yacine Brahimi ndiye mshindi wa mwaka huu.
Hapajawahi kutokea katika miaka 23 ya historia ya shindano hilo kwa mchezaji bora kutoka Algeria kuishinda, lakini Brahimi amefanikiwa kutwaa tuzo hiyo baada ya mwaka uliokuwa na mbwembwe wa 2014.
Aliingiza bao la ushindi dhidi ya mabingwa wa Hispania Barcelona, bao lengine la kisasa katika ligi ya mabingwa wa ulaya na kisha kuwa katika msitari wa mbele wakati nchi yake iliposonga mbele katika michuano ya kombe la dunia.
Yacine Brahimi
Hio ilikuwa historia kwa Algeria kufika katika awamu ya muondoano katika dimba hilo.
Hii bila shaka ilikuwa nafasi nzuri kwa mashabiki wa BBC pamoja na wapenzi wa soka kumchagua kama mchezaji bora zaidi wa Afrika mwaka huu.
Aliwapiku wachezaji wengine nyota wakiwemo, Pierre-Emerick Aubameyang wa Gabon, Vincent Enyeama wa Nigeria, Gervinho wa Ivory Coast na hatimaye Yaya Toure - aliyenyakua ushindi mwaka jana.

MTI MKUBWA WAPIGA MWELEKA MCHANA HUU ENEO LA SEAVIEW



 Sehemu ya mashuhuda wa tukio la kuanguka mti mkubwa katika barabara ya Sea View,Upanga jijini Dar es Salaam.baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo wamesema kuwa chanzo cha kuanguka mti huo ni ukongwe wa mti huo.
 Sehemu ya magari yaliyoangukiwa na Mti huo mchana huu.


 Muonekano wa Mti huo.
 Mti huo ukiwa umeangukia ukuta.
 Baadhi ya wamiliki wa magari hayo wakijadiliana mara baada ya magari yao kuangukiwa na mti huo.
 hapo kwenye hiyo viti kuna watu walikuwa wamekaa lakini walinusurika.
Hawa ndio waliokuwa wamekaa kwenye hivyo viti.chanzo Issamichuzi blog
 Sehemu ya mashuhuda wa tukio la kuanguka mti mkubwa katika barabara ya Sea View,Upanga jijini Dar es Salaam.baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo wamesema kuwa chanzo cha kuanguka mti huo ni ukongwe wa mti huo.
 Sehemu ya magari yaliyoangukiwa na Mti huo mchana huu.


 Muonekano wa Mti huo.
 Mti huo ukiwa umeangukia ukuta.
 Baadhi ya wamiliki wa magari hayo wakijadiliana mara baada ya magari yao kuangukiwa na mti huo.


MVUA ILIYONYESHA BAGAMOYO YASABABISHA MAFURIKO



 Sehemu ya kituo cha mabasi Bagamoyo kikiwa kimejaa maji




Hizi ni picha tofauti zikienesha taswira ya mvua iliyonyesha Bagamoyo alfajiri ya leo na kusababisha mafuriko. Hayo ni maji yaliyojaa stendi ya mabasi ya Bagamoyo.

RAIS KIKWETE AMTEUA PROF MUSSA ASSAD KUWA CAG MPYA, KUAPISHWA KESHO


THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS


PRESIDENT’S OFFICE,
STATE HOUSE,
1 BARACK OBAMA ROAD,
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.

Telephone: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: ikulucommpress@googlemail.com
Website : www.ikulu.go.tz
Fax: 255-22-2113425

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Profesa Mussa Juma Assad kuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).

Taarifa iliyotolewa leo, Jumatatu, Desemba Mosi, 2014 na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue, inasema kuwa uteuzi wa Bwana Assad ulianza Novemba 5, mwaka huu, 2014.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa Bwana Assad ataapishwa kesho, Jumanne, Desemba 2, saa nne asubuhi, Ikulu, Dar es Salaam.


Kabla ya uteuzi wake, Bwana Assad alikuwa Profesa Mshiriki, Idara ya Uhasibu, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na anachukua nafasi ya Bwana Ludovick Utouh ambaye amestaafu kwa mujibu wa Sheria za Utumishi wa Umma.

Profesa Assad ni msomi, mwenye weledi, ujuzi na uzoefu mkubwa wa uhasibu na udhibiti wa fedha ambaye ana Shahada ya Uzamivu wa Uhasibu (PHD in Accounting) kutoka Chuo Kikuu cha Southampton, Uingereza mwaka 2001 na Shahada ya Uzamivu katika Udhibiti wa Fedha (MA in Financial Accounting) kutoka Chuo Kikuu cha Dublin City, Jamhuri ya Ireland mwaka 1991.

Profesa Assad pia ana Stashahada ya Kitaaluma ya Uhasibu (Professional Diploma in Accounting) kutoka Chuo Kikuu cha Dublin City mwaka 1990 na Shahada ya Biashara (Bachelor of Commerce) ya Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam mwaka 1988.

Pamoja na uzoefu wa kitaaluma, Profesa Assad anao uzoefu mkubwa katika eneo la uhasibu na ukaguzi. Alikuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wahasibu na Wakaguzi (NBAA) kwa miaka saba (2007 - 2014); ni Rais na Mjumbe wa Chama cha Wahasibu Afrika (Pan African Federation of Accountants) tangu mwaka 2012; na ni mjumbe wa Bodi kadhaa za Wakurugenzi nchini Tanzania.

Katika kumteua Profesa Mussa Juma ASSAD kuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Rais anayo imani kubwa kuwa elimu, weledi, ujuzi na uzoefu ambao Profesa Assad anao utamwezesha kutekeleza vema majukumu ya nafasi hiyo muhimu sana katika utawala bora wa nchi yetu.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.

1 Desemba,2014

WACHEZAJI WA SUNDERLAND WAKIWA WAMEVAA FULANA ZA KUITANGAZA TANZANIA KWENYE MECHI YAO DHIDI YA CHELSEA




Squad wear special warm-up t-shirts.
The players wore special t-shirts ahead of the home draw with Chelsea as part of the club's partnership with Tanzanian Tourist Board.

The Black Cats took to the field in the pre-game warm up sporting shirts emblazoned with the ‘Visit Tanzania’ logo as part of the partnership.
SAFC has already developed close links with Tanzania, through providing technical and practical support to the development of the football academy project, the first of its kind in the country.


The project will see thousands of youngsters benefit from a joined up approach combining football, education and community engagement, harnessing the knowledge and expertise of Sunderland AFC and its own successful Academy.  

PONGEZI KWA MSANII NASSIB ABDUL AKA DIAMOND KWA KUSHINDA TUZO TATU ZA CHOAMVA14


1976886_842456352442847_3553307454253637477_n
Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kama msimamizi na mratibu wa sekta ya Sanaa nchini linapenda kutoa pongezi za dhati kwa Msanii wa muziki wa kizazi kipya Nassib Abdul maarufu kama Diamond kwa kushinda tuzo tatu kwa mkupuo za CHOAMVA zinazoendeshwa na kituo maarufu cha luninga cha Channel 0 chenye makao makuu yake Afrika Kusini.
Tuzo alizoshinda Diamond ni pamoja na Most Gifted East African Artist, Most Gifted Afro Pop video na ile ya Most Gifted New Comer. 

Kushinda kwa Diamond katika tuzo hizo kubwa barani Afrika na kuwashinda wasanii wengine wenye ‘majina makubwa’ ni ishara kwamba muziki wetu unakubalika ndani na 
Baraza linatoa wito kwa wasanii na wadau wote wa muziki kuzidisha ubunifu, bidii na weledi katika kazi wanazozifanya ili wasanii wengi zaidi waweze kuchomoza katika tuzo na majukwaa mbalimbali ya kimataifa kwa lengo la kujitangaza na kukuza soko la kazi zao kimataifa.
Aidha, Baraza linaendelea kuwakumbusha na kuwasisitiza wadau wa muziki na Sanaa kwa ujumla hususan wakuzaji Sanaa (mapromota) kuendelea kujenga mazingira rafiki kwa wasanii wetu kufanya kazi kwa ubora na weledi lakini pia kwa upendo na furaha ili kujenga daraja zuri kwa wasanii wengi zaidi kung’ara kwenye ngazi za kimataifa.
Ni imani ya Baraza kwamba, ushindi huu wa kihistoria wa Diamond utakuwa chachu kwa wadau wote wa Sanaa nchini hususan wasanii katika kujituma na kuhakikisha hawaridhiki na mafanikio waliyonayo. 
Ni matumaini ya Baraza kwamba wasanii na wadau wote wa Sanaa wataendelea kutambua umuhimu wa kufuata sheria, kanuni na taratibu za uendeshaji sekta sambamba na kutambuliwa na Serikali.
Sanaa ni kazi, tuipende na kuithamini
 
 
Blogger Templates