Social Icons

Ijumaa, 10 Oktoba 2014

BASI LA DAR EXPRESS LILILOPINDUKA ENEO LA MAMBA MKOANI KILIMANJARO










Gari ya Dar Xpress lifanyalo safari zake Kati ya Dar - Rombo likiwa limepata ajali jana jioni eneo la Marangu _Mamba. Watu kadhaa walijeruhiwa

ANGALIA PICHA JAMBAZI ALIEKUWA ANAUWA WANAWAKE ARUSHA AUWAWA

 Mwili wa Jambazi hilo ukiwa umelazwa ndani ya gari la polisi mara baada ya kuwawa tayari kwa ajili ya kupelekwa mochwari
picha ya juu na chini  wananchi wa jiji la Arusha  waliojitokeza kuuangalia mwili wa  jambazi huyo atari aliowawa na polisi usiku wa kuamkia leo





 wananchi wakiendelea kushuhudia mwili wa jambazi hilo nje ya jengo la makao makuu ya polisi mkoani Arusha












 baadhi ya vitu vilivyokutwa kwa jambazi hilo zikiwemo silaha mbalimbali




 kamanda wa polisi akionyesha moja ya kifaa cha kufanyia tageti kabla ya kupiga kijulikanacho kwa jina laGlock Fab Defence moja ambacho jambazi hilo lilikuwa likitumia


Jambazi mmoja aliefahamika kwa jina la Ramathan Abudallah  alimaarufu kwa jina la Ramadhani Ndonga (37) mkazi wa  Moivo  ameuwawa baada ya kupigwa risasi katika majibizano na askari  wa jeshi la polisi.



Akizungumzia tukio hilo kamanda wa polisi mkoani Arusha Liberatus Sabas Alisema kuwa tukio hilo limetokea October 10  mwaka huu majira ya saa nane na dakika nne usiku   katika  kijiji cha  Moivo  kilichopo ndani ya kitongoji cha  Enaboishu wilayani Arumeru.



Alisema kuwa marehemu  Ramadhan Abdallh  aliuwa anatafutwa kwa muda mrefu na jeshi la polisi kwa kuhusika na matukio mbalimbali ya uhalifu ambayo yameshawahi kutokea ndani ya  mkoa huu pamoja na katika maeneo mbalimbali ya nchi hiii.

Alibainisha  kuwa kuuwawa kwa jambazi hili kumetokana na  juhudi na kutumia mbinu za kisasa za kiyupelelezi na kufika  nyumbani kwa mtuhumiwa (marehemu) ambapo askari polisi walimwamuru  ajisalimishe lakini alikaidi amri na kuanza kuwarushia risasi hali ambayo ilisababisha askari kujibu mashambulizi na kumsababishia  umauti kumfika.



“Mara baada yakupiga jambazi huyo polisi walianza kumpekuwa  mwili wa marehemu na alipatiana akiwa ba bastola aina ya Glock 19 yenye namba RLU976 iliotengenezwa nchini Austria ikiwa na magazine yenye risasi (14) ambapo alikuwa ameishika mkononi pamoja na maganda matano yarisasi  na  mbali na hapo polisi pia  walifanya upekuzi katika chumba cha jambazi hilo na kukuta magazine ingine moja yenye risasi (15) na magazine zingine mbili zenye uwezo wa kubeba risasi thelathini kila moja ,Radio call moja  yeye nembo ya ITSS/UNICTR  pamoja na pikipiki aina ya toyo power king rangi nyekundu yenye namba za usajili T507 BSU  pamoja na kofia ngumu”alisema Sabas
 

Aidha alibainisha kuwa  pia katika upekuzi huo wa ndani ya nyumba ya jambazi hilo pia walifanikiwa kupata pingu moja ,plate namba ingine ya pikipiki yenye namba za usajili T 805 CVD  ambapo alibainisha kuwa jambazi hili lilikuwa likibadilisha plate namba ya pikipiki kila mara  pamoja na  chomba maalumu cha kuwekea magazine pamoja na kufanyia tageti kabla yakupiga risasi (Glock Fab Defence moja),kifaa cha kusafishia bastola pamoja na koti kubwa jeusi.

Kamanda Sabas alitaja baadhi ya matukio ambayo jambazi hili lilishayafanya  kuwa ni pamoja na tukio  lililotekea Augast 6  majira ya saa tatu na nusu usiku maeneo ya kwa iddi ambapo mtuhumiwa  akiwa na mwenzake ambaye ajakamatwa walimpiga risasi ya shingo mwanamke aliyefahamika kwa jina la Shamimu Rashid aliyekuwa mkazi wa sakina wakati akijiandaa kuingina nyumbani kwake  ,hu ku tukio lingine likiwa limetokea Augast 21 saa 19:00 maeneo yaoasiti ambapo jambazi huyo akiwa na mwenzake kwenye pikipiki walimjeruhi kwa kumpiga risasi yam domo na kutokea kichwani  mototo aitwaye Christen NIckson mwenye umri wa miaka mitatu na nusu na kisha kufanikiwa kumpora TSH 2000 na baadae majeruhi kufariki dunia akiwa anapatiwa matibabu.



Kamanda sabas alitumia nafasi hiyo kuwapongeza askari wake kwa kufanya kazi nzuri pamoja na kuwahaidi wananchi kuendelea kufanya uchunguzi na kuwabaini wahalifu wote na kuwachukulia sheria kali.



“arusha sio sehemu ya kuifadhi wahalifu ivyo tutajitaidi kwa hali na mali kuhakikisha tunawamaliza majambazi wote pamoja na wahalifu wote na napenda kuwaaambia wahalifu waache mapema maana sasa ivi tumejipanga vilivyo ,pia napenda kuchukuwa nafasi hii kuwaomba wananchi pia waendelee kuwafichua wahalifu  popote pale ili tuwaangamize kabisa”alisema Sabas



Mmoja wa wananchi ambaye alijitokeza kushuhudia maiti ya jambazi hilo Aliyejitambulisha kwa jina la Alaija Saro akiongea na libeneke blog hili alilipongeza jeshi  la polisi kwa kuweza kumuangamiza jambazi hilo kwani limekuwa likiwatia mashaka watu wengi na kuwanyima raha kwa jinsi walivyokuwa wanauwa watu.

ENGLAND YAISAMBARATISHA SAN MARINO 5-0

Timu ya England imefanikiwa kupata ushindi mara mbili katika michezo miwili ya kundi E ya kufuzu kucheza michuano ya bara la Ulaya ya mwaka 2016 baada ya kupata ushindi mnono wa 5-0 dhidi ya San Marino.
England alianza kuvuna magoli kupitia kwa mlinzi wake Phil Jagielka aliyefunga katika dakika ya 24 kwa mpira wa kichwa kabla ya Wayne Rooney kuongeza bao la pili kwa njia ya penalti katika dakika ya 43 kutoka na madhambi ya mchezaji wa San Marino Andy Selva.
Naye mshambuliaji Danny Welbeck alifanikiwa kutumbukiza goli la tatu kwenye dakika ya 49. Goli hili lilitokana na mpira wa pasi kutoka kwa mchezaji mwenzake wa Arsenal ambaye aliingia kipindi cha pili Alex Oxlade-Chamberlain.
Andros Townsend aliiongezea timu yake ya England goli la nne kwa mkwaju wa mbali kabla ya Alessandro Della Valle kujifunga mwenyewe kutokana na kugongwa na mpira uliopigwa na Rooney.
Matokeo ya michezo mingine: Belarus 0: Ukaraine 2, Macedonia 3: Luxembourg 2, Slovakia 2: Spain 1, Lithuania 1:Estonia 0, Slovenia 1: Switzerland 0, Liechtenstein 0: Montenegro 0, Moldova 1:Austria 2, Sweden 1: Russia 1.

Jumanne, 7 Oktoba 2014

RONALDO NA MPENZI IRINA KATIKA PATI LA KUSHEREHEKEA HAT TRICK YA 22 REAL MADRID

Cristiano Ronaldo amesherehekea hat trick yake ya jana Real Madrid kwa kumtoa kwa chakula cha usiku mpenzi wake, Irina Shayk
Shayk alikuwapo Uwanja wa Bernabeu jana Ronaldo akifunga hat trick ya 22 tangu atue Real Madrid
Ronaldo alifunga kwa mara ya 14 mfululizo mechi za nyumbani, Real Madrid ikiifunga Athletic Bilbao 5-0

Jumapili, 5 Oktoba 2014

WATU WAWILI WANUSURIKA KUFA ENEO LA MSIKITINI MBAGALA

Watu wawili namenusulika kifo baada ya kontena la kunde kudondoka kutoka juu ya gari la mizigo lililokuwa kwenye mwendo kasi, likitokea Mbagala rangi tatu likielekea Kariakoo jijini dar es salaam.Taarifa zinasema kwamba hakuna mtu aliyepoteza maisha wala kujeruhiwa katika tukio hilo, isipokuwa vijana wanaoishi maeneo hayo walianza kuzoa Kunde baada ya kontena kuanguka kabla ya polisi kufika.
 
Inalipotiwa kuwa chanzo cha ajali hiyo nikutofungwa vizuri kwa kontena hilo pamoja na bodi ya gari la mizigo husika.
 
Ajali hii imetokea leo maeneo la Msikitini kati ya Mtongani na Mission jijini dar es salaam.

Cheik Tiote aelezea ae kuhusu tuhuma za kuwa na wake wawili.


1412035570092_wps_25_Cheik_Tiote_of_Newcastle_
Hivi karibu gazeti la The Sun liliripoti juu ya tuhuma za kumhusu kiungo wa timu ya Newcastle Cheick Tiote na familia yake.

Tiote, ambaye anavuna kiasi cha paundi £45,000 kwa wiki kupitia klabu yake ya Newcastle, ameripotiwa kufunga ndoa ya kimila na Laeticia Doukrou mwezi uliopita, japokuwa tayari ameshaoa mke mwingine aitwaye – Madah mwenye umri wa miaka 25.
1412061273983_Image_galleryImage_Tiote_with_wife_number_2_
Tiote na mke mpya
Kiungo huyo mwenye miaka 28, kwa sasa anaishi na Madah pamoja na watoto wao wawili katika jumba lao lenye thamani ya £1.5million Ponteland karibu na Newcastle, pia Tiote ana mtoto mwingine nje ya ndoa zake na mwanamke wa nje aitwaye Nikki Mpofu.
20_TIOTE_NUFC_SUN_EXC.jpg
Nikki Mpofu na mtoto wa nje ya ndoa wa Tiote
Wakala wa mchezaji huyo Jean Musampa amethibitisha kuhusu mchezaji kuoa mara ya pili, alisema: ‘Ninachoweza kusema ni kwamba ni kweli ameoa na hiyo ni ndoa yake ya pili.
‘Hiki ni kitu cha kawaida, Tiote ni muislam, sheria za kidini zinamruhusu kuoa hadi wake wanne, hivyo hakuna kibaya alichofanya.This is nothing unusual. He is a Muslim.’
Tiote pia anaripotiwa kuwaambai marafiki zake kwamba haoni shida kuwa na wanawake wengi, na hata nyumbani kwao Ivory Coast ameshwakuwa na mahusiano na wanawake wengi. Gazeti la The Sun limeripoti. 
Gazeti hilo pia limeripoti kwamba mahusiano kati ya Tiote na ‘hawara’ yake Nikki Mpofu yamefikia ukingoni baada ya miaka mitatu baada ya mwanamke huyo raia wa Zimbabwe kuchoshwa na ahadi za uongo za kuolewa na mchezaji huyo.

MHITIMU WA CHUO AVUA NGUO ZOTE JUKWAANI ALIPOITWA KUPEWA CHETI ZA KUMALIZA CHUO


Wasomi wanapokutana hasa katika zoezi la kutunukiwa cheti kama kielezo cha uhitimu wa ngazi fulani kuna vitu huwezi kuvifikiria kama vitatokea hata kidogo.
Katika Jack Britt High School, North Carolina, Marekani wanafunzi mmoja amewaacha hoi mamia ya watu waliohudhuria sherehe ya kutunukiwa vyeti (graduation) baada ya kupanda jukwaani kupokea cheti chake na ghafla akavua johon lake na kubaki na boxer.

Baada ya kuvua joho alinyoosha mikono yote miwili juu kama mwanamieleka anayetamba. Lakini haikuchukua round wanausalama wakamdhibiti na kumuweka chini ya ulinzi.
Kwa mujibu wa The Huffington Post, kijana huyo alinyang’anywa diploma yake na hivyo hakukabithiwa cheti.
Hata hivyo bado anahesabiwa kama mtu aliye maliza masomo yake na kuhitimu licha ya kuwa hana kielelezo cha elimu yake.
“Shule yetu imefanya jitihada kubwa. 

Hapo zamani watu waliohudhuria walikuwa wenye vurugu wakati wa graduation. Tumefanya jitihanda kuwafanya watu waheshimu wanafunzi. 

Huyu kijana amechagua kutoonesha heshima kwa wanafunzi wenzake.” Alisema Dr Frank Till, mwalimu wa chuo hicho

DIAMOND AND DAVIDO TO PUT BBA AFRICA IN REAL FIRE TO MARK ITS OFFICIAL OPENING TODAY!!!


Mateka Muingereza aachiliwa huru Libya

David Bolam
Mwalimu mmoja raia wa Uingereza ambaye alitekwa nyara nchini Libya mwezi Mei mwaka huu ameachiliwa huru
Wizara ya masuala ya kigeni nchini Uingereza imethibitisha kuwa David Bolam ambaye alikuwa akifanya kazi na shule moja ya kimataifa kwenye mji ulio mashariki wa Benghazi yuko salama salmin.
Haijulikani ni nani aliyemteka nyara,lakini inaaminika kuwa kundi moja la kiislamu.
Vilevile inaamimika kuwa kuwachiliwa kwake kulitekelezwa na makundi ya wansiasa wa eneo hilo na kwamba kikombozi kililipwa ili kumwachilia huru,ijapokuwa haijulikani ni pesa ngapi.
Mwandishi wa BBC ameambiwa kuwa shule aliyokuwa akiifanyia kazi ilitakiwa kulipa fidia.
Bolam tayari asharudi nchini Uingereza.

Ngome nyengine ya Al-Shabaab yaanguka

Mji wa bandari wa Barawe nchini Somalia ambao ulikuwa umetajwa kuwa ngome ya mwisho ya kundi la Al shabaab umethibitiwa na vikosi vya serikali vikisaidiwa na wanajeshi wa muungano wa Afrika.
Mji wa Barawe ulio umbali wa kilomita 200 Kusini Mashariki mwa mji mkuu wa Mogadishu umekuwa chini ya udhibiti wa wanagambo wa Al Shabaab kwa miaka sita.
Muungano wa Afrika unasema kuwa wanamgambo wamekuwa wakiutumia mji huo kama kituo cha kupanga mashambulizi dhidi ya mji mkuu Mogadishu.
Wapiganaji wa Al-Shabaab walianza kuondoka katika mji huo siku chache zilizopita.
 
 
Blogger Templates